Adeladius Makwega-MWANZA
Muziki wa Tanzania hasa ule wa dansi umejengwa na kujificha katika simulizi nyingi ambazo chache zimehifadhiwa katika maandishi, sauti na video huku simulizi zote za muziki huo zikijengwa katika kuta za studio za Redio Tanzania Dar es Salaam(TBC TAIFA) ambazo kwa hakika ilifanya kazi kubwa ya kuzihariri , kusisanifu, kuzirekodi na kuzihifadhi hadi leo hii nyimbo hizo katika hali yake ya ubora.
Siku ya leo Mwanakwetu ameamua kukusimulia juu ya wimbo Mwanakwetu wa ORCHESTRA SAFARI SOUND (OSS) wana OSS iliyokuwa katika kilele cha mafanikio yake mwaka 1983, wakati huo kiongozi wake alikuwa Fredie Ndala Kasheba ambapo alitambulisha rasmi mtindo wa Chunusi uliokuwa ukiaminika ni kijembe kwa washindani wao wakubwa ORCHESRA MARQUIZ DU ZAIRE waliokuwa wakitumia mtindo wa Ogelea Piga Mbizi
Wakati mpambano wa bendi hizo ukielekea kufanyika katika ukumbi wa DDC Magomeni Kondoa, OSS iliongeza mwimbaji kijana Skassy Kasambula aliyetokea kukubalika sana na kiongozi Ndala Kasheba.Tayari bendi ya OSS ilishaachia vibao hatari vilivyowagusa mashabiki na ilishavirekodi na kuanza kuyakata mawimbi katika vipindi vingi vya RTD.
Mwaka huo huo 1983 aliyeandika makala haya alikuwa na maka 6 hivyo siku hiyo alikuwa mdogo na hakuwepo ukumbini lakini waliyokuwepo wanasema ,
“Mpambano huo uliacha rekodi ya kujaza mashabiki wengi na kutokea patashika pale ndala Kasheba alipovunja gitaa kwa kulipiga chini na kuchukuwa Kombora la Nyuzi dazani kuendelea na burudani ukumbini.”
Katika Albam hiyo Iliyowakamata vilivyo wapenzi wamuziki wa dansi wa Tanzania siku hiyo, pamoja na nyimbo nyingine pia kulikuwa na kibao kiitwacho MWANAKWETU
Kibao hicho kilitungwa na Kasheba mwenyewe na kilikuwa kikiombwa hata mara tatu au zaidi katika dansi moja na vipindi vya RTD.Hii ilitokana na aina ya upigaji wa gitaa la nyuzi 12 la Kasheba ambalo katika albam hiyo lilipigwa tofauti na nyingine zilizopita.
Waliyokuwepo ukumbini wanasema
“Waimbaji Skassy na Kababa Nkomba walikuwa wakionekana kuchangamka sana pale jukwaani wimbo MWANAKWETU
Ulikamata mioyo ya mshabiki kama ulivyokuwa wimbo NYAMA YA NYANI.”
Waliokuwepo enzi hizo wanashuhudia kuwa wimbo huo na albam yake nzima jinsi zilivyopendwa kiasi cha kuitikisa bendi ya mahasimu wao Marquiz kuamua kusitisha maonyesho na kwenda kuweka Kambi Kisiwani Mafia walikorejea na mtindo wa ZEMBWELA.Hapo ndipo mtindo wa ogela piga mbizi ukafia kisiwani Mafia. Albam hiyo ilirekodiwa Februari 3, 1983 ikiwa na nyimbo nyingine kama MPAKAMANGA,SALAAM KWA MSIKILIZAJI, TATU SAID, NOEL MILELE NA MAHOKA.
Mwanakwetu anasema nini siku ya leo?
Kwa hakika wimbo Mwanakwetu unazungumzia masuala ya mapenzi ambapo wapendanao wawili waliachana na mpenziwe akaenda kuolewa kwingine, haya ndiyo maisha ya binadamu hasa vijana , huku kijana aliachwa akionekana kama kujuta juu ya mpenziwe. Kwa hakika mkomonzio wa wimbo huu unaonesha hali ua huzuni ambayo inambeba alichwa na anaombwa msamaha kusikitika pia na hilo hata anayeusikiliza pia linamkuta.
Mwanakwetu yooyooo,
Kumbe ni Mkataa pemaa,Sasa naliaaa.
Tumeachana juu ya Mama yooyoo.
Umeolewa Haraka ungesubiri kwanzaa.
Ugomvi wetu makosa yangu mimi eeee, Ulevi mpenzii Ushauri mbayaaa
Pombe na mawazo wivu hayo upoteza mapendo
Yamenipata kweli mimi najutaa
Kaa kando fikiria mamaa
Yamenipata leoo, kweli mimi najuuta
Nimekaa kando nasubiri Msamaha wakoo
Huyu ndugu mueleze ukweli
Njoo bado utazame watoto
Pombe na mawazo ya wivu hayo upoteza mapendo
Yamenipata leo Kweli
Kaaa kando fikiria mamaa.
Nimekaa mimi nasubiri msamaha wakoo
Huyu ndugu mueleze ukweli
Njoo bado utazame watoto
(Maneno yote juu rudia mara ya Mbili )
Bado nakuwaza kila siku nyumbani,
Nimekaa kila siku nakutazama nyumbani
Naoa aibu mbele ya wezangu mpenzi
Mimi ndiyo jikoni matembezi nimeacha
Nakuwaza mama yooyoo
Fikiria kila binadamu ana makosa bibi dunia hapa siyo mimi mtu wa kwanza
Wapo wengi wamegombana, yangu mimi ndiyo balaa
Mpenzi wangu njoo kando yooo yoo
Mpenzi wnagu kila siku ninakuwaza
Mpenzi wnagu ebu rudi nyumbani
Naona aibu mbele ya wezangu mpenzi
Mimi ndiyojikoni na matembezi nimeacha
(Mashairi haya yameandikwa kwa kuusikiliza wimbo huu na kama kuna makosa ya manenoni ni yangu mimi Adeladius Makwega.)
Mwanakwetu Upo?
Kumbuka wimbo Mwanakwetu ulisababisha Maquiz kubadilisha mtindo kutoka Ogelea Piga Mbizi Kuwa Zembwela.
Nakutakia siku Njema.
0717649257
Post a Comment