SIASA ZA NDUMILA-KUWILI

 


Adeladius Makkwega-MBEYA

Nilipokuwa nasoma Stashada ya Ualimu Chuo cha Ualimu Kasulu kati ya mwaka 2001-2003 tulifundishwa mbinu bora za kufundishia ambapo kama mwalim unaweza kufundisha kwa kutumia nyimbo na hata visa mkasa, njia hizo zinasaidia mwanafunzi kuelewa jambo kwa haraka na kulikumbuka milele.

Natambua wale niliyosoma nao ualimu KACCU 2003 watakuwa mashahidi maana darasa zima wapo hai tukiongozwa na kaka yetu mkubwa Profesa Albart Idaya Sheka na dada yetu mkubwa Bi Mkwimba Mhondo.

“Profesa Sheka na Mwalimu Mhondo walikuwa wametuzidi umri huku wakituongoza pale tulipokengeuk.”

Kwa wale wana KACCU- 2003 natambua kuwa Eliud Mwakalili ambaye tulianza naye mafunzo ya ualimu Julai 2001 alifariki Disemba 2002 katika ajali ya Lori alilokuwamo yeye akisafirisha viazi vyake mviringo toka Mbeya kwenda sokoni Dar es Salaam ili apate karo ya chuo cha ualimu wakati wa likizo ambapo marehemu Mwakalili alikuwa akijisomesha mwenyewe.

Rashid Ally na Serarini Sawa ambao walikuwa marafiki wa Mwanakwetu wakati wa uhai wa Eliud Mwakalili walikuwa wakimtania marehemu Mwakalili kuwa hana pesa na masikini hadi kumuimba katika wimbo huu,

“Mwakalili naye mtu, Japokuwa hana kitu.”

Haya yalikuwa maneno yaliyopachikwa nasisi katika wimbo wa Tunda Special wa Mwinjuma Muumini.

“Masikini naye mtu, japokuwa hana kitu.”

Msomaji wangu hayo yote ninayoeleza tangu awali ni rejea tu ya maisha ya Mwanakwetu wakati akisoma hiyo stashahada ya ualimu Wilayani Kasulu mkoani Kigoma wakati huo, kubwa kwako msomaji ni kukubeba hapo ulipo hadi katika visa mkasa ambavyo leo natamani ujifunze jambo kutoka kwa Mwalimu Bora –MwAnAkWeTu.

“Mwanakwetu hapo ni mwanachuo wa Chuo Kikuu Tumaini Iringa hiyo ni mwaka 2005 yu darasani na mhadhiri anayefundisha kozi ya Communication Skills Profesa Frola Kasumba kaingia anafundisha kimombo kwa wanachuo wa Shahada ya Sanaa ya Habari. Profesa Kasumba ni mwalimu tangu shule ya msingi, mama huyu anazo mbinu kadhaa na kufundishia. Msomaji wangu unaweza kuwa  daktari wa falasafa na hata profesa  hu darasa unposimama watu hawakuelewi-watu hawawei kusea wakiogopa kufelishwa tu-Wewe up mbele unajiongelesha  kumbe unaongea mwenyewe.Hapo umekosa mbinu za kufundishia. Prefesa Kasuba anasomesha darasa lenye wanachuo zaidi 61 hukuanawafahamu kwa majina yao.

Akiwa anafundisha akamuulizi binti mmoja wa kichaga yupo wapi? Binti akajibu nipo huku nyuma. Profesa Kasumba akamuuliza binti huyu mbona umehama hapa mbele ambapo unakaa siku zote? Binti wa kichaga anajibu kuwa hapo mbele leo kuna baridi kali. Profesa akauliza kwani kukiwa na baridi ndiyo unahama? Kukiwa baridi binti yangu ukitoka chumbani kwako unavaa mavazi ya kupambana na baridi kama vile makoti na masweta mazito mazito maisha yanaendelea, huku ukiwa palepale. Hapo darasani watu wapo kimya wanamsikiliza Mama Kasumba anapiga sindano za moto kwa wanafunzi wake ambapo wengi walikuwa rika ya watoto wake wa kuwazaa labda isipokuwa kwa wanachuo wawili tu ; Estom Sanga na Jean Mhalila.

‘Unajua nyinyi bado wa wadogo, mkimaliza chuo mnakwenda kazini, sasa leo upo kazini hapo unakaa kidogo unahamia kazi nyingine . leo huko na mume huyu kesho una mume mwingine hilo halikubaliki maisha yanahitaji utulivu na uvumilivu maana nyinyi wote ni viongozi. Tabia ya kuhamahama inaweza kuhamia hata katika mambo yetu yale(mapenzi) ’

Hapo darasani watu wanacheka, somo likafundishwa kwa saa nzima na baadaye Profesa Kasumba kuondoka zake.”

Msomaji wangu hicho ni kisa cha kwanza na cha kweli na kwa hakika BAJ 2008 walisoma na Mwanakwetu watakumbuka kisa hicho na watakuwa mashahidi labda tu kwa Profesa Flora Kasumba mwenyewe atakuwa amesahau maana anafundisha wanachuo wengi na sasa mzee.

 


Nakuomba msomaji wangu nikuhamishie katika kisa mkasa cha pili,

“Binti mmoja alimaliza chuo kikuu vizuri, wazazi wake masikini mno mama mchoma vitumbua na baba fundi cherehani. Binti huyu wazazi wake walikuwa wakiishi pwani ya taifa la Afrika Mashariki wao hawakuwa wenyeji wa Pwani bali walihamia kutafuta maisha eneo la vibanda mikoa ya pwani, alipohitimu chuo kikuu akatamani angie katika siasa za upinzani. Binti huyu alipokelewa vizuri maana alikuwa mchangamfu na muongeaji mzuri akapata vyeo vingi huko huko upinzani.Kiongozi wa hiki chama cha upinzani walikuwa wanatoka naye eneo moja kwa asili, hivyo hilo lilimpa nguvu huku akivutiwa hulka ya kiongozi huyu wa upinzani namna anavyoongea na vyombo vya habari na anavyofanya siasa zake hadharani,umma na binti huyu wakila yamini kuwa huyu kiongozi wa upinzani ni mtu sahihi na mkombozi wa wanyonge.

Ulipofika wakati wa uchaguzi mkuu huyu binti kwa kuwa alikuwa msomi, anaaminiwa sana, kabila moja na kiongozi wa upinzani na huku akiwa na vyeo kadhaa akachaguliwa waende wakachukue mzigo sehemu fulani, ambapo kiongozi wa upinzani yeye angeenda ingeleta shida. Wakatoka hadi hapo sehemu wakakaribisha vizuri na kukabidhiwa sanduku la fedha. Binti huyu akashangazwa na mambo manne, mbona hii ofisi tuliyoingia ni ya chama tawala na huyu kiongozi aliyotukabidhi mzigo ni kiongozi wa chama tawala na kwanini tukabidhiwe fedha hizi kwa mficho? Hapa kuna upinzani wa kweli? Binti huyu akatilia shaka akakaa kimya, wakarudi hadi kwao wakakabidhi mzigo ambao ulikuwa fedha nyingi.

Waliokwenda kuchukua ule mzigo wakapewa pesa kila mmoja na ahadi baada a uchaguzi mkuu watapewa nafasi. Binti akachukua zile fedha akaenda kufungua duka ambapo bab yake fundi cherehani akawa anauza huku anashona na mama yake akamuongezea mtaji vitumbua.Moyoni binti akasema hapa hakuna upinzani wa kweli.

Akawaeleza wazaz wake huku kwenye hizi siasa nimejifuza hiki na hik mim sitoendelea tena natulia zangu zikitoka az serikalini niombe na kuachana kabisa na siasa baadaye zilitangazwa kazi za serikali katika taifa hilo aliomba na kupata akawa mtumishi wa serikali katika mojawapo ya safari zake za kimataifa anakutana na Mwanakwetu na ndipo alipomsimulia kisa hiki cha vyama vya upinzani Afrika.”

Mwanakwetu anasema nini siku ya leo? 


 

 

Katika kisa cha Profesa Flora Kasumba kuna maneno haya;

“Unajua nyinyi bado wadogo, mkimaliza chuo mnakwenda kazini, sasa leo upo kazini hapo unakaa kidogo unahamia kazi nyingine, . leo huko na mume huyu kesho una mume mwingine hilo halikubaliki maisha yanahitaji utulivu maana nyinyi wote ni viongozi. Maana tabia ya kuhama hama inaweza kuhamia hata katika mambo yetu yale(mapenzi) ’

Katika Tanzania ipo shida ya wanasiasa kuhamahama vyama vyao hili Mwanakwetu anaona halina maantiki yoyote ile, hili siyo jambo la kupigiwa mfano.


 

Jambo hili lazima likemewe kwa wanasiasa wetu na ndiyo maana Mama Kasumba aliwaambia BAJ 2009 kuwa;

“…kwani kukiwa na baridi ndiyo unahama? Kukiwa baridi binti yangu ukitoka chumbani kwako unavaa mavazi ya kupambana na baridi kama vile makoti na masweta mazito mazito maisha yanaendelea…”

Hili kila wanasiasa wetu wawe wa chama tawala au vyama vya upinzani wajifunze, hoja hii inaonekana zaidi katika kisa cha pili ambapo binti huyu aliyemaliz chuo kikuu na kujiunga na upinzani anachukizwa na Siasa za Undumila Kuwili. Kikubwa vyama vyote vya siasa viepuke kuwa vikaragosi wa vyama vingine maana jamii inaona. Vyama vyote vya siasa vipewe fedha za uendeshaji wake maana uimara wa chama pinzani ndiyo uimara wa chama tawala.Vyama pinzani vikiwa dhaifu na chama tawala kitakuwa dhaifu na viongozi wote watakuwa dhaifu na mwisho wa siku jamii haitokubaliana na hilo.


 

Mwanakwetu upo?

Kumbuka,

“Uimara Chama Pinzani Uimara Chama Tawala-Tuepuke Siasa za Undumila Kuwili.”

Nakutakia siku njema.

makwadeladius@gmail.com

0717649257






 

 

0/Post a Comment/Comments