Adeladius Makwega-MWANZA
Kiranja na Mkuu wa Propaganda Fide wa Kanisa Katoliki Ulimwenguni anayeshugulikia Uinjiiishaji wa Watu Kadinali Luis Antonie Tagle amesema kuwa Mweenyenzi Mungu tangu enzi na enzi amewaamini vijana katika udogo wao na kuwapa majukumu makubwa kiasi kwamba majukumu hayo waliyopewa vijana yakawa chachu ya kumkomboa mwanadamu, hivyo dunia inawajibu wa kuwaamini vijana katika huo huo udogo na vichache walivyo jaliwa na Mungu.
Haya yamehubiriwa na Kadinali Tagle katika mahubiri yake ya Dominika ya 17 ya mwaka B wa Lituriia a Kanisa Julai 28, 2024 yaliyorushwa na JesCom TV.
“Je unaafiki kuwa vijana wanayo nafasi kubwa katika kazi ya ukombozi? Mathalani Daudi alitawazwa mfalme wa Israeli akiwa na umri wa miaka kumi na tano, huku Selemani mwenye busara nyingi alikuwa mfalme akiwa na miaka Ishirini mwanzo mwanzo. Naye Nabii Yeremia alikuwa kijana tu pale alipochagulia kumsemea Mungu-Naye Mwenyeenzi Mungu alimwambia asihofie udogo wake maana hatomuacha.
Hata na Bikira Maria alipofuatwa na malaika na kuelezwa mpango wa Mungu alikuwa binti mdogo na akaafiki. Jamani hata katika injili ya leo kijana mwenye mikate mitano na samaki wawili -chakula chake kinabarikiwa na kuwalisha watu elfu tano huku vikisalia vyakula kadhaa. Kwa hakika vijana wanayo nafasi maalumu katika fikra na moyo mwenyeenzi Mungu.”
Katikati ya mahubiri yake Kadinali Tagle alitolea mfano ya taswira mbili jamii yenye njaa, kiu huku watoto wakifa kwa utapia mlo na huku kukiwa kundi kubwa la watu wenye vyakula tele wakila na kusaza. Akisema hao wanaosaza chakula na kutowajali wenye kiu njaa na utapia mlo wanatenda dhambi mbele za Mungu.
Sambamba na mahubri ya Kadinali Tagle nako katika Kanisa la Bikira Maria Malkia wa Wamisionari , Parokia ya Malya Jimbo Kuu Katoliki la Mwanza Padri Norbert Renatus Bukombe akihubiri katika misa hiyo alisema kuwa Injili ya dominika ya leo Yesu hakuombwa msaada kuwalisha makutano bali yeye mwenyewe alitambua hitaji hilo maana alikuwa na moyo wa huruma na upendo kwa watu je nasi tunatambua mahiaji ya jamii bila kuombwa?
“Leo hii tunakumbushwna sisi tuwaonea huruma wenzetu, muujiza wa kuwalisha watu elfu tano ni muujiza wa kugawana na kila muhitaji na huku kila mmoja akichangia kidogo kidogo tunaweza kuwa na nguvu zaidi katika kutatua changamoto za jamii zetu.
Tukumbuke kauli mbiu ya Kanisa la Kisinodi- Ushirika, Ushiriki na Umisionari. Leo tunakumbushwa kila mmoja anapaswa kushiriki kama Yesu alivyowashirikisha wanafunzi wake na ile jamii waliyokuwa nao pale mkutanoni na sisis tushirikishane.”
Kwa hakika katika Kanisa la Bikira Maria Malikia wa Wamisinari ndipo aliposali mwandishi wa ripoti hii hali ya hewa ni baridi nyakati za asubuhi kwa eneo la zima la Malya na viunga vyake na jua la kadili nyakati za mchana.
Huku jamii ya Wasukuma ikiendelea na sherehe mbalimbali kama vile harusi zinazoambatana na shamrashamra na ngoma za asili maana msimu wa mavuno ndiyo unapunga mko kwa kwaheri na kuukaribisha kwa heshima na taadhima msimu wa kilimo.
Post a Comment