UTOSINI HADI UNYAYONI

 



Adeladius Makwega-MWANZA

Shule ya Sekondari Tambaza kati ya mwaka 1985-1994 ilikuwa na mama moja mwalimu wa somo la Basic-Mathematics aliyefahamika kama RMSK.BURUDA. Wajihi wa mama huyu ulifanana na wanawake wa mikoa ya Kanda ya Ziwa hasa WAJALUO lakini jina lake lilikuwa ni ngumu kutambua asili yake.

“Mama mmoja mrefu, mweusi, mnene, anajiamini, hana maneno mengi na mtulivu.”

RMSK. BURUDA alifundisha BASIC MATHEMATICS tangu kidato cha kwanza hadi nne huku akifundisha kidato cha tano na cha sita masomo ya jamii hiyo.Utaratibu wa Tambaza ulivyokuwa mwalimu anayeanza na kidato cha kwanza anafundisha somo hilo hadi kidato wanamaliza kidato cha nne, kama mwalimu husika ni mzuri basi darasa hili litafuzu na kama mwalimu husika ni galasa basi darasa hilo limepotea.

Kwa hakika RMSK.BURUDA ni jina ambalo Mwanakwetu analikumbuka mno maana alikuwa miongoni mwa walimu wachache wanaoshiriki kutunga vitabu vya BASIC MATHEMATICS vile vya kiada tangu kidato cha kwanza hadi cha nne na nina imani mama huyu pia alishiriki kutunga mitihani ya kidato cha nne. Hata leo hii msomaji wangu kama unabisha hilo la kutunga vitabu tembelea maktaba ya taifa angalia vitabu vya BASIC MATHEMATICS vya miaka hiyo katika utangulizi utaona majina yanayoshukuruliwa kwa kuifanya kazi hiyo utabaini RMSK. BURUDA limo.

Pale Tambaza kipindi hicho ilikuwa shule ya kutwa na kulikuwa na makundi mawili I&II. Hawa wakiingia asubuhi na wengine kuingia mchana. Walioingia mchana walipewa wali nyama maharage au ugali nyama maharage na wale waliyoingia asubuhi walipewa skonzi ya mkate.Utoaji wa vyakula hivyo ulikuwa bure kwa gharama ya serikali.Huu ugawaji wa skonzi ulikuwa ukifanyika dakika chache kabla ya wanafunzi kwenda mapumziko ya asubuhi na wakati huo pengine darasani kuna mwalimu anamalizia somo lake. Hapa wanakuja viongozi na dishi lenye skonzi 40 alafu wanazigawa darasani , sasa wanafunzi vijana hawakuwa wavumilivu skonzi zikiingia tu wanalivamia dishi zinamwagika na wengine wanakosa na wengine wanapata nyingi hasa wale wenye nguvu.


 

Siku moja RMSK. BURUDA anamalizia kufundisha,gafla ndugu Emmanue Changala aliingia na vingozi wenzake na dishi la skonzi darasani wanafunzi walivamia na hilo likaleta vurugu mno darasani na wagawa skonzi walivyotoka RMSK.BURUDA akawatazama wanafunzi wake wa kidato cha kwanza kwa jicho kali, alafu akasema hiyo tabia mimi siipendi na kuongeza maneno haya.

“Nyinyi mnadhani hatuwafahamu, tunawafahamu vizuri tangu utosini hadi unyayoni. Kwanza kwa majina ya koo zenu na pili wajihi wenu. Sura yako na jina lako utambulisho tosha, hayo mawili yanawakilisha ndugu zako na familia yako ambao hapa hawapo.

Mimi nawafahamu vizuri na mnatambua Mama Buruda huwa siongei sana nafundisha mahesabu yangu naondoka. Mnatambua mimi ninavyoheshimika siyo Tanzania tu hata Afrika Mashariki kwa namna nivyofundisha na kutunga vitabu vya hesabu.Sasa niwaambieni humu darasani mwenu yupo mwanafunzi mwezenu, baba yake tunatunga naye vitabu vya hesabu na mwanachama mwezangu wa chama cha hisabati Tanzania anaheshimika sana kama ninvyoheshimika mimi lakini yeye huyu mwezenu anagombea skonzi darasani, kweli jamani mnatutendea haki sisi wazazi wenu?”

RMSK. BURUDA aliendelea kupiga sindani kwa wahuni wa Tambaza wagombea skonzi, huku darasani wakijitahidi kumjua ni nani huyo ambaye baba yake mtaalamu wa Basic Mathematics nchini Tanzania? Siku hiyo hakujulikana na sina hakika kama alijulikana.


 

RMSK. BURUDA akapigilia msumari wa mwisho

“Jitahidini kuwalindia heshima wazazi wenu maana mna vitu viwili jina na wajihi. Naombeni mbadilike na mjirekebishe.”

Kengele ya mapumziko ilipigwa huku wanafunzi hao wa Tambaza kutoka darasani vichwa chini na kwenda kununua mihogo, karanga, chipsi na waliobahatisha skonzi wakanunua chai tu mikahawani na kuinywa jirani na maabara za shule hii ya umma.

 Mwanakwetu anasema nini siku ya leo?

Mwaka 2024 na 2025 ni mwaka wa chaguzi Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu, chaguzi hizo zinatanguliwa na kura za maoni za vyama vyote vya siasa ikiwamao chama tawala CCM. Kura za maoni CCM zina shida kubwa ya rushwa ya wazi wazi na jambo hilo mara nyingi linaachwa kama lilivyo na kama ni haki ndani ya CCM rushwa kufanyika.

Watu wakitania,

“Aaaahh wajumbe wamefanya kazi yao.”

Kazi gani waliyoifanya hao wajumbe ? Kama siyo siyo kuwaelewa vizuri watoa rushwa?Aah unajua CCM ikilifuatilia suala hlo itajiua yenyewe! Aaah CCM ni dude kubwa bwana, CCM lazima ilifuatilie suala hilo na tena kwa ukali zaidi na kwa hilo kiwe chama cha kupigiwa mfano.

Kwa bahati mbaya tuhuma hizo zinakihusisha chama ambacho kinakuja kushika dola na kuziongoza taasisi za ulinzi na usalama na hata taasisi zinazuia na kupambana na rushwa .

Mathalani-na kwa mfano tu Waziri anayeisimamia TAKUKURU kama taasisi hiyo inakuwa na taarifa kwa mfano tu za mhusika namna alivyoshinda kura za maoni na jamaa kawahonga wajumbe.


 

Je usimamizi wa taassi husika unaweza kufanyika vizuri baada ya uchaguzi? Hata anahitajika kiranja nayepinga rushwa kwa dhati.

Msomaji wangu unaweza ukafumbia macho kama hauoni lakini jamii inaona vizuri kama ilivyokuwa kwa RMSK. BURUDA kwa wanafunzi wale wa Tambaza wanaogombea skonzi.

“Nyinyi mnadhani hatuwafahamu, tunawafahamu vizuri tangu utosini hadi unyayoni. Kwanza kwa majina ya koo zenu na pili wajihi wenu. Sura yako na jina lako utambulisho tosha, hayo mawili yanawakilisha ndugu zako na familia yako ambao hapa hawapo.

Mimi nawafahamu vizuri na mnatambua Mama Buruda huwa siongei sana nafundisha mahesabu yangu naondoka.Mnatambua mimi ninavyoheshimika siyo Tanzania tu hata Afrika Mashariki kwa namna nivyofundisha na kutunga vitabu vya hisabati.Sasa niwaambieni humu darasani mwenu yupo mwanafunzi mwezenu baba yake tunatunga naye vitabu vya hesabu na mwanachama mwezangu wa chama cha hesabu Tanzania anaheshimika sana kama ninavyoheshimika mimi lakini yeye huyu mwezenu anagombea skonzi darasani, kweli jamani mnatutendea haki sisi wazazi wenu?”

Jamii inafahamu na vizuri na ndiyo maana RMSK BURUDA akaupigilia msumari kwa kusema maneno haya,

“Jitahidini kuwalindia heshima wazazi wenu maana mna vitu viwili jina na wajihi.Naombeni mjirekebishe.”

Kama watu wanafahamu basi ni wajibu wa CCM, chama cha Mwanakwetu kupambana na hiyo hali mapema ili jamii itambue kuwa uchaguzi huu hautakuwa na rushwa na mwarobaini wake ni huu kama kura maoni zinapigwa na wanachama wote basi kila tawi inapopigwa kura za maoni CCM iwe na wasimamizi wake lakini sanduku na daftari lenye orodha za majina ya wapigakura zikisimamiwa na Polisi, Idara ya Usalama na TAKUKURU na hao ndiyo wajumlishe kura na kukusanya taarifa za rushwa hadi ngazi ya taifa.


 

Hao watumishi wa umma wapewe posho yao vizuri. Wakiifanya kazi hiyo. Akaunti zote za benki za wagombea wa kura za maoni zisiruhusiwe kutoa pesa kwa vingi kipind chote cha kura za maoni .Nao madiwani na wabunge wanaomaliza muda wao malipo yao fedha zao za kumaliza muda wao wa uongozi yafanyike Januari ya mwaka mpya baada ya uchaguzi mkuu.

Hawa akina RMSK. BURUDA wapo wachache na yanayosemwa yatilie maanani ili wasiseme ,

“Haya mambo tangu enzi baba kafanya na mtoto anafanya maana Chilongwa Mbali na Chitendwa mbali.”

Mwanakwetu upo?

Kumbuka RMSK BURUDA anasema,

“Tunawafahamu Tangu Utosini Hadi Unyayoni.”

Nakutakia siku njema.

makwadeladius@gmail.com

0717649257


 


 





0/Post a Comment/Comments