MAJENGO SERIKALI YAZINGATIE HUDUMA ZA DHARULA


 Adeladius Makwega-MWANZA

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo nchini ndugu Methusela Ntonda amesema kuwa majengo yote ya serikali ambayo yanajengwa na yatakaliwa na watu wengi kama vile mabweni yanatakiwa kuzingatia kuwekwa huduma za dharula kwani makazi ya watu wengi huduma hizi ni za muhimu ni siyo jambo la mjadala.

Hayo yamesemwa na Serikali Agosti 27, 2024 Katika Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya (MCSD) ambapo Naibu Katibu Mkuu Ntonda akiwa amekita kambi kukagua miradi kadhaa ya serikali iliyopo chini ya Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo(MCSD) iliyopo Kwimba mkoani Mwanza.

“Unashagaa jengo limewekwa nondo tele katika madirisha na milango, hapa najua patawekwa madirisha ya kuvuta ya vioo. Ukiweka nondo tele dharula ikitokea inakuwaje? Haya yazingatiwe ili wanaokuja kuishi humu wasitamahuke kabla ya dharula haijatokea, hili lazima lizingatiwe katika mradi huu na miradi yetu yote.”

Naibu Katibu Mkuu Ntonda aliongeza kuwa milango na madirisha yahakikishwe yawe bora kwa kiwango chake, kama ilivyo katika michoro ya jengo hilo la bweni la wanachuo ambalo lipo katika hatua za mwisho kukamilka katika chuo hiki kinachotoa Astashahada na Stashahada kadhaa za michezo nchii Tanzania. Katika ziara hiyo Naibu Katibu Mkuu Ntonda alipokelewa na Mkuu Chuo hiki ndugu Richard Mganga ambapo Idara ya Maendeleo ya Michezo nchini iliwakilishwa na Dkt Ado Komba ambaye ni Mkurugenzi Msaidizi.


 

Ziara hii ni safari kifungua mimba ya Naibu Katibu Mkuu Methusela Ntonda hapa MCSD tangu ateuliwe na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan hivi karibuni.




 

0/Post a Comment/Comments