OLIMPIKI 2024 TANZANIA IMEBORONGA

Adeadius Makwega-MWANZA

Kenya inashikilia nafasi ya kwanza barani Afrika katika michezo ya Olimpiki ambayo imekamilika jijini ParisOlympics2024. Kenya ina medali 11 kwa ujumla mbili za fedha, tano za shaba na nne za dhahabu na inashikilia nafasi ya 17 duniani. Nchi yako imefanya vipi iwapo iliwakilishwa kwenye Olimpiki ?”

Agosti 11, 2024 Mwanakwetu alikutana na swali hilo katika ukurasa wa RFI–KISWAHILI  ukiwauliza wasikizaji na wafuatiliaji wake. Kwa hakika Mwanakwetu kama kama msikiiizaji na mdau wa RFI KISWAHILI analijbu swali hilo kama lilivyo.Hapa hakuna ubishi na wala hakuna kufichana,

“Tanzania imeboronga katika michezo ya Olimpiki iliyomalizika jijini Paris maana tumeambulia patupu na hata kutaja namba za wachezaji wetu walizoshika na hata kuyataja majina ya wachezaji waliyotuwakilisha huko inakera na kututia aibu.”

Matokeo mabovu ya kila mara ya wachezaji wetu yanauzi mno na yameondoa hamasa ya kila Mtanzania kushabikia michezo ya ndani. Ambapo kwa asili Watanzania ni wapenda sana michezo.


 

Kwa hakika kwa nyakati tofauti Mwanakwetu amekuwa mshangiliaji na hata mchezajii wa soka, japokuwa alikuwa anapiga madochi, cha mno katika madochi hayo yaliweza na lengo ni kufunga magoli mengi, maana Raha Mchezo Ushindi.

Nikiwa mdogo nilisimuliwa haya, wakati timu inapokuwa inajiandaa na mashindano mashabiki, wapenzi na viongozi wanafanya mambo kadhaa ya kiimani kuelekea kuutafuta ushindi.Wakati wachezaji wakijifua katika maandalizi kadhaa. Mathalani kama timu pinzani imepata penati golini ili mpiga penati huyo akose kuna imani hii.

Ashakumu si matusi,

Mashabiki wanashika kende zao kwa mikono miwili.”

Mshiko huo unaachiwa baada ya penati kupigwa na mpigaji kukosa.Wakati mashabiki wengine kadhaa wanabaki kwa mganga wakiwa wamekaa jikoni huku wameyashikilia mafiga matatu kila mmoja ameshikilia figa moja, mmoja akichoka mwingine anampokea kulishikilia figa hilo hadi mechi inakwisha.Had mechi imekamilika na ushindi umepatikana.Mashabiki wengi wanakuwa pamoja na timu wao walitakiwa kuvikunja vidole vyao kwa kuvipandashia juu ya kingine hilo likiaminika kuipa uimara timu kushiriki mashindano hayo uwanjani kwa ufanisi mwanzo mwisho.


 

Kama hilo halitoshi, mashabiki wengine wanaweka vijiti katika nywele zao ambavyo vinakuwa vijiti maalumu kutoka mti maalumu ulifanyiwa dawa maalumu ya timu kupata ushindi.Timu uwanjani pia kundi kubwa la mashabiki wanaendelea na hekaheka uwanjani kushagilia timu mwanzo mwisho.Haya mambo yanafanyika na mara nyingi timu ilirudi na ushindi wote mshangilio ulikuwa wa wote wachezaji viongozi, waweka vijiti,wakunja vidole,washika mafiga na washika ashakumu si matusi wote wanashangilia.

Mwanakwetu anasema nini siku ya leo?

Swali ni je,

“Kwa sasa Tanzania kuna jitihada za pamoja za kuutafuta ushindi ?”

Kwa sasa Tanzania imekuwa bingwa wa kukosa medali katika mashindano kadhaa ya kimataifa na kwa hakika walio wengi tunaamini viongozi wanaosimamia mchezo wanayafanya haya mambo manne;

“Wanaweka vijiti kichwani, wanakunja vidole, wanashika mafiga na wanashika ashakumu si matusi lakini wanafanya hivyo kulinda nafasi zao tu na siyo kuutafuta ushindi katika michezo.”

Kwa hakika shabaha ya makala haya nikuonesha njia ili Tanzania ifanikiwe katika michezo kuna wajibu wa kila Mtanzana kutimiza wajibu wake katika kuyafikia malengo hayo bila kujali ni nani. Viongozi wa mchezo watambue kuwa kulinda nafasi zao kutatokana na mafanikio ya michezo kwa kuwapanga Watanzania kuyafikia malengo haya kwa kuibua vipaji tangu vya watoto wadogo na kuvikuza.Dhana ya ushirikinani imetumika tu kujenga dhana ya pamoja katika kufanikiwa kimichezo .


 Mwanakwetu anawajibu RFI Kiswahili kuwa Tanzania imefanya vibaya, Tanzania imeboronga katika olimipiki ya 2024 na viongozi wa mchezo Tanzania wanawajibu wa kujipanga vizuri wa waache kuweka vijiti kichwani, waache kukunja vidole, waache kushika mafiga na waache kushika ashakumu si matusi kwa nia ya kuwasahaulisha  matokeo mabovu ya olimpiki  2024 ili kulinda nafasi zao, bali hayo yafanyike kuutafuta ushindi.

Mwanakwetu upo?

Kumbuka,

“OLIMPIKI 2024 TANZANIA IMEBORONGA”

Nakutakia siku njema.

makwadeladius@gmail.com

0717649257




 

 

 




 


 


0/Post a Comment/Comments