VIJANA KWA WAZEE KILA MMOJA AJIFUNZE KWA MWENZAKE-KADINALI TAGLE

 

Adeladius Makwega-MWANZA.

Kiranja wa Propaganda Fide ambaye anashugulikia Uinjiishaji wa Watu wa Kanisa Katoliki Ulimwenguni Kadinali Luis Antonie Tagle amesema kuwa dominika ya 18 ya mwaka B wa Kanisa (Agosti 4, 2024) Yesu mwenyewe anasema yeye ndiye Mkate wa Uzima na chakula kisichoharibika, huku akisisitiza vijana wajifunze kwa wazee nao wazee wajifuze kwa vijana.

“Maneno ya Yesu yanalenga kutufundisha wafuasi wake kutazama ishara ambazo amekuwa akifanya, kama vile kulisha watu 5000 hadharani. Katika kumfuata Yesu, tunachopaswa kutamani kupokea si chakula kiharibikacho, bali chakula kidumucho hata uzima wa milele. Chakula hiki kidumucho hata uzima wa milele ni Yesu mwenyewe na tunashiriki kwa njia ya sakramenti ya Ekaristi Takatifu.Kwa lishe inayotokana na tangazo la Neno lake, tunapokula mwili na damu yake, ambayo ni ushirika wetu nayeye. Hebu twende kwa Yesu, ndugu zangu, kwa shauku zote kwa ajili yake yeye ambaye ni mkate ushukao kutoka mbinguni na kuupatia ulimwengu uzima.”

Akiendelea kuhubiri katika luninga ya Jescom inayorusha matangazo ya misa za kila siku Kadinali Tagle aliongeza kuwa

 

“Jumapili iliyopita (dominika ya 17 ya mwaka B) nilidokeza majukumu maalumu ya vijana katika kazi ya Mungu ya ukombozi wa mwanadamu. Hapo Mungu aliwaita vijana kuwa viongozi, kuwa wachungaji na wake wasemaji wake. Tuliona mifano namna Mungu huyu huyu alivyowaita vijana mathalani Bikira Maria kuwa mama wa mkombozi wetu Yesu Kristo. Hata kwa Yesu mwenyewe baadhi ya miujiza yake na mafundisho yake yanaonesha namna alivyokuwa jirani na vijana. Vijana wanatakiwa kuishi maisha ya Uchu Mungu na ndiyo maana hata Baba Mtakatifu Fransisko na watangulizi wake Benedikt wa XVI na Yohane Paulo II walitilia maanani hilo.

 

Baba Mtakatifu Fransisko anasisitiza kuwa kikubwa si kusombwa na maisha ya kidunia yanaoneshwa katika runinga na vyombo vya habari kama vile utajiri, jambo la msingi ni kumuabudu Mungu wa kweli kama tanavyojifunza katika mafundisho ya Yesu na maisha yake. Katika kulikamilisha hilo vijana na watu wazima wanahitajika kushirikiana .”

Kadinali Tagle alimalizia mahubiri yake kwa kuupigilia msumari mwisho kuwa vijana wajifunze kwa wazee na wazee kwa vijana kwa vijana.Akidokeza kua vijana kujifunza kwa watu wazima siyo kwamba wanajifunza mambo ya kale bali wanajifunza na kupata uzoefu wa maisha na namna wazee walivyokabiliana na changamoto mbalimbali maishani mwao nyakati zao.

 













 

0/Post a Comment/Comments