WATU WANATENGENEZA UTARATIBU

 

 

Adeladius Makwega -Kinole-Morogoro

Mwaka 2021 Mwanakwetu alikuwa Kinole mkoani Morogoro ambao Wazari ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ya Tanzania wakati huo  Innocen Bashungwa alikuwna anazinduzi wa mnara wa Matangazo ya  kisasa wa TBC, Mwanakwetu alikuwa miongoni mwa maafisa.wa wizara waliokuwepo.

Ukiweka kando ziara hiyo Mwanakwetu aliandika makala haya.

Kama nilivyodekeza katika matini ya awali kuwa ushahidi mkubwa ambao ulimtia hatiani Saddam Hussein na kunyongwa akiwa na wenzake katika mauwaji ya Dujaili kwa sehemu kubwa ulikuwa ni sehemu ya nyaraka alizotumiwa au kusaini yeye juu ya tukio hilo pamoja na sauti ya mawasiliano ya simu sehemu ya maagizo yake kwa walio chini yake pamoja na mkanda za video ambazo ulirekodiwa na wasaidizi wake ambao aliambatana nao siku ya Julai 8 1982 katika ziara hiyo.


 Jaji Mkuu wa Zamani wa Iraki Awadh .

Swali la kujiuliza je kwanini Saddam Hussein alifanya ziara hiyo hapo Dujaili katika mji mdogo uliokuwa na watu 75,000 na siyo miji mingine mikubwa kama Mosul na Baghdad iliyokuwa na idadi kubwa ya watu? Jibu lake ni kwamba eneo hili lilikuwa ngome ya wanamgambo cha Daawa ambacho kilikuwa na ushirika na Irani ambayo wakati huo tayari vita vilishaanza baina yao.

Kunyongwa kwa Saddam Hussein kulifanyika Disemba 30, 2006.Huku Disemba 13, 2006 Barzan Hassan ambaye alikuwa ni ndugu wa Saddam Hussein ambaye pia alikuwa mkuu wa Usalama wa Taifa hilo, Awad Bandar ambaye alikuwa Jaji Mkuu wa Mahakama ya Mapinduzi ya Iraki walisindikizwa mpaka katika chumba maalumu tayari kwa kunyongwa ambapo iliaminika kuwa wangenyongwa pamoja na Saddam Hussein siku hiyo lakini saa nane baadaye mamlaka ya Iraki iliamua kuwa Saddam Hussein anyongwe peke yake. Huku waliosalia yaani Barzan Hassan ambaye alikuwa Mkuu Usalama wa Taifa wa Iraki na Awad Bandar aliyekuwa Jaji Mkuu walinyongwa Januari 15, 2007.

Hoja za leo juu ya mauwaji ya Dujali ni zipi?

Mosi, katika mji wa Dujali ulikuwa na watu 75,000 mpaka leo hii idadi ya watu wa mji huo ni haijafikia 150,000 ndiyo kusema ni mji mdogo sana kwa Dar e Salaam ni sawa ni Kata ya Mbagala na Kata Mbagala Kuu kwa pamoja, lakini ni mji ambapo ulipaswa kutazamwa kwa umakini katika siasa za Iraki. Inavyoonekana Saddam Hussein alilitambua hilo na ndiyo maana alifanya ziara Dujaili lakini hesabu zake zilikosewa kwa kutazama kwamba kwa kutumia nguvu za kijeshi, sheria za taifa hilo na mamlaka yake angeweza kuwamaliza na kuwashinda lakini ikiwa kinyume na mauwaji hayo kuupa nguvu kubwa Mji Dujail na hata wanamgambo wa Chama cha Daawa.

Kwa kosa hilo tu Chama cha Daawa kilitumia karata hiyo vizuri kwa kuwatumia wanachama wote waliotese,kuumizwa, kushuhudia, kunyanyaswa na kufariki katika matukio ya Dujaili kama mashahidi na mashujaa na jambo hili liliongeza chachu kwa wale wanachama cha Daawa waliokimbilia uhamishoni.

Kwa wanasiasa wawe makini sana maana hapa funzo kubwa ni kuwa kila eneo katika taifa lolote lisidhalauliwe kwa udogo wake na misimamo yao iwe ya kisiasa au jambo lolote maslahina jamii hiyo, maeneo yote yatiliwe maanani sawa.


 Tareq Aziz.

Chama cha Baath kilikuwa ni chama cha Kisoshalisti japokuwa Sunni wengi walikiunga mkono huku Saddam Hussein akiwashirikisha hata Wakristo na Shia  ndani ya Chama cha Baath, hapa alifanikiwa sana mathalani Waziri wake wa Mambo ya nje Tareq Aziz kwa kuwa alikuwa Mkatoliki na mjuzi wa lugha ya Kiingereza aliweza kutengeneza mahusiano mazuri na Vatikani na mataifa ya Ulaya na ndiyo maana Saddam aliweza kudumu sana katika utawala wake huku akishinda vikwazo vingi mathalani vita vyake na Irani kwa miaka karibu sabaa, mgogoro wake na Kuwaiti na Vita vya Ghuba ya Kwanza na hata vya pili. Funzo hapa ifahamike kuwa nchi ni mali ya kila mmoja wetu ni jambo zuri na muhimu kushirikisha watu kutoka kila kundi ili watumie ujuzi wao kulijenga taifa.

Chama cha Daawa chenye Shia wengi kilisabisha hali ilizidi kuwa mbaya kila miaka ilivyokuwa ikisonga mbele kwa kuwa mgawanyiko huo ulikuwa ni kibiriti tosha kuimaliza Iraki taifa lenye Waisilamu wengi. Suluhu ingekuwa kama Saddam Hussein angekubali ndani ya serikali yake kuwapa nafasi Shia hapo chama cha Daawa kingekosa muelekeo. Hili na hata Shia wakati wa Saddam wangekuwa wanaota hata kupata urais na lingepunguza harakati za wanamgambo na hilo lingewezekana kwa kuwa chama cha Baath hakikuwa chama cha kidini.

Tatu Saddam Hussein alipaswa kuliongoza taifa hilo kwa haki kabisa na suala lile lakushambuliwa yaani mapinduzi yaliyoshindwa kule Dujaili asingelifanya kama alivyolifanya kwani hilo ndilo lililogharimu utawala wake.

Nne Saddam Hussein aliamini katika mawazo yake na mawazo wa baraza lake la chama cha Baath tu, mazungumzo na chama cha Daawa yalionekana kama kusalimu amri lakini hiyo ingekuwa suluhu na hata wao kuwaingiza kidogo kidogo katika serikali ya Baath wakitokea huko huko chama cha Daawa na wao wakaona kuwa ni sehemu ya utawala wa taifa hilo. Funzo ni kuwa mazungumzo baina ya watu na watu, kundi na kundi na vyama na vyama ni jambo la maana sana, yanaweza kusaidia kuepusha balaa kwa wakati mwingine mbeleni.

Tano Saddam Hussein aliamini katika katiba, sheria na kanuni alizozitengeneza mwenyewe na chama chake kwani mtazamo wa nje ni kuwa katiba, sheria na kanuni zilikuwepo kwa manufaa ya kumlinda yeye. Funzo ndiyo katiba, ndiyo sheria lakini kumbuka wanaongozwa ni binadamu wanaweza wakawa na mahitaji fulani nje ya sheria na nje ya katiba mambo haya ni vizuri kuyafanyia kazi na ndiyo maana hizo katiba na sheria zinabadilishwa.


 Barzan al Tikrit Mkuu wa Usalama wa Taifa za zamani wa Iraki.

Ndiyo maana kumtia hatiani Saddam Hussein ilitengezwa mahakama nyingine kulishughulikia shauri la Saddam Hussein na wenzake katika Mauwaji ya Dujaili ili kuyakamilisha matakwa yao. Funzo ni sawa katiba ni sawa sheria lakini kubwa kuhakikisha haki inapatikana kwa wote na usifanye ubaya ukitegemea hayo sheria na katiba kumlinda mtu yoyote hili ni gumu.

 

“Mimi ndiye niliyefanya maamuzi haya kama mkuu wa nchi mbona mnawauliza wengine, kwamba watuhumiwa wote walipelekwa katika mahakama ya mapinduzi na hakuna aliyekuwa na uwezo wa kupinga kama mimi niliamua hivyo?”

Maneno haya yanaonesha kuwa Saddam Hussein alitambua mamlaka yake aliyokuwa nayo kisheria na kikatiba kuwa alikuwa na kinga kumbe kinga inawekwenda na maji maana jamaa walitengeneza utaratibu mpya wa kumtia hatiani. Msomaji tambua jamii ikiwa na jambo lao wanatengeneza utaratibu ndiyo hizo mahakama maalumu.

Viongozi wajitahdi kusimama katika haki kwajamii zote unazoziongoza kwa kuzishirikisha kila jambo.

Mwanakwetu upo?

Kumbuka

 

“Watu Wanatengeneza Utaratibu-Mauwaji yaliyompeleka Saddam Hussein Kitanzini.”

 Nakutakia siku njema.

 

makwadeladius@gmail.com

 
0717649257




 

0/Post a Comment/Comments