MAPENZI DARAJA KUKAMILISHA MIPANGO

 



Adeladius Makwega-MBAGALA

Jonah Anguka ni mwandishi wa Kenya na Mkuu wa Wilaya wa zamani wa Nakuru, anayejulikana kama mtu pekee hadi leo aliyefikishwa kizimbani kwa mauaji ya Dk Robert Ouko, Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Kenya, ambaye aliuawa kwa kupigwa risasi Februari 13 1990.

“Anguka alihitimu kutoka Chuo Kikuu cha Nairobi mnamo 1977 kwa shahada ya sayansi ya kisiasa. Alifanya kazi katika utawala wa majimbo ya Kenya wakati huo, awali alipewa mafunzo ya kijeshi katika Kituo cha Mafunzo cha Embakasi General Service Unit (GSU)-Idara ya Usalama ya Kenya. Baadaye alifaya kazi katika nyadhifa mbalimbali kama ofisa wa wilaya kabla ya kuwa Mkuu wa Wilaya (DC) hapa Nakuru 1986. Kwa hiyo alikuwa sehemu ya shirika la usalama wa ndani na kijasusi la Kenya na kuwajibika moja kwa moja kwa Hezekiah Oyugi, wakati huo Katibu Mkuu, Mkoa na Ndani. Usalama.”

 

Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Kenya wakati huo, Dk Robert Ouko, aliuawa asubuhi ya tarehe Februari 13,1990, kwa kupigwa risasi ya kichwa, umbali mchache kutoka makazi yake huko Koru, karibu na Kisumu, kaskazini magharibi mwa Kenya. Mkewe wa Anguka, Bi Susan Ngeso Anguka inadaiwa alikuwa Msaidizi Binafsi wa Dkt Ouko katika Wizara ya Kigeni. Pia inadaiwa pia mama huyu alilima ardhi iliyo karibu na shamba la Dkr Ouko huko Koru.

“Je Bi Susana Anguka na marehemu(Msaidizi Binafsi wa Waziri) na Dkt Ouko(Waziri wa Mambo ya Kigeni) je walipokuwa shambani jirani walilima vyoteeee! na hata walipokuwa ofisini kazini walifaya vyoteee?”

 

Jonah Anguka alitajwa kuhuka na mauaji ya Dkt Ouko na watu watano tofauti. Mnamo Novemba 18,1991, katika Tume ya Kimahakama ya Uchunguzi wa mauaji ya Dkt Ouko, Msimamizi wa zamani wa Upelelezi John Troon ambaye aliongoza uchunguzi wa Scotland Yard (kwa ombi la serikali ya Kenya) kuhusu mauaji hayo, alisema kwamba,“Kuna uwezekano kwamba Bw Anguka. anaweza kuwa na ushiriki au ujuzi fulani wa mauaji hayo.”Troon alikuwa akihojiwa na Jaji Akiwumi, Jaji Gicheru na Bernard Chunga (Mwendesha Mashtaka wa Serikali) wakati wa Tume ya Kimahakama ya Uchunguzi wa kifo cha Dkt Ouko alipoibua kesi hiyo kwa uchunguzi zaidi wa Mkuu wa Wilaya Anguka. Anguka pia alitajwa na polisi wa Kenya katika sehemu ya kurasa sita ya Uchunguzi Zaidi wa Kifo cha Marehemu Dkt Robert Ouko' ambamo walieleza mambo kumi na nne ya kwa nini achukuliwe kuwa mshukiwa. Hatimaye, Jonah Anguka alitajwa kuhusiana na mauaji ya Dkt Ouko na mamlaka sita tofauti na watu binafsi.“Seke seke la kumtaja ndugu Anguka ni pamoja na kakake Dkt Ouko, Barrack Mbajah, kijakazi wa Ouko, Salina Were, na katika madai ya maandishi yasiyojulikana yaliyotumwa kwa polisi wa Kenya mnamo Desemba 1991 yenye kichwa ‘Nani Alimuua Dkt. R.J. Ouko na Kwa Nini?’ ”Jaji Aganayana baadaye alimwachia  huru Anguka, akisema,Na kwa kuzingatia muda wa tukio ambapo marehemu anadaiwa kuondoka nyumbani kwake (karibu saa 3.00 asubuhi) isingeshawishika kwamba baada ya kufanyiwa mazoezi ya viungo na Oddotte saa 12.30 asubuhi yeye (Anguka) angetoka nje ya nyumba akaenda kwa Koru, akamuondoa marehemu nyumbani, akampeleka mahali alipopigwa risasi na kisha kumfikisha eneo la tukio na kuuchoma moto mwili wake usiku huo huo, kisha kurudi nyumbani kwake na awe tayari kwa kazi saa 7.15 asubuhi…” 

Maprofesa Cohen na Odhiambo walibaini kuwa Anguka alikuwa katika eneo ambapo mwili wa Dkt Ouko ulipatikana ndani ya saa mbili baada ya kugunduliwa na polisi. Pia ndugu Anguka alikuwa nyumbani kwa Ouko Koru kujibu simu katika sebule ya Ouko wakati Susan Anguka, mkewe, alipopiga simu kutoka Wizara ya Kigeni kumwambia kwamba mwili umepatikana. Hata alikuwa wa kwanza kutangaza habari za kifo cha mumewe kwa Bi Ouko, isitoshe alikuwa katika uwanja wa ndege kukutana na timu ya Scotland Yard na alimtambulisha Msimamizi wa Upelelezi Troon kwa Hezerkiah Oyugi na kumwambia kuwa atasimamia zoezi hilo. Aliyekuwa Mbunge wa Kisumu Mjini Mashariki Gor Sunguh alisema“Kifo cha shahidi huyo kinaweza kuwa kielelezo cha mwisho wa uchunguzi na ufichuzi wa ukweli.”Gor Sunguh, ambaye aliongoz tume iliyochunguza kifo cha Ouko, anasema zaidi kuwa,“Mashahidi 100 kufikia sasa walitoweka katika mazingira ya kutatanisha.”Aongeza kuwa kama hili litafanya isiwezekane kwa Wakenya kupata ukweli zaidi. Hata hivyo, wengine wanahoji kuwa ukweli utajulikana, ikizingatiwa kwamba mashahidi wengi walizungumza mbele ya vyombo mbalimbali vya uchunguzi. Baadhi ya mashahidi walio hai hadi leo hii ni pamoja na aliyekuwa DC Jonah Anguka, Zablon Agallo ambaye alikuwa afisa wa Polisi wa Utawala, mlinzi wa Ouko Gordon Okoth, Phillip Ogutu (mlinda lango), Eric Ouko na James Onyango K'Oyoo na Mashahidi wengi wamekufa katika mazingira ya kutatanisha. Kwa sasa Jonah Anguka anaendelea kuishi California, Marekani, ni mwanachama hai wa jumuiya ya eneo hilo na mchangishaji wa miradi ya kijamii katika eneo la Magharibi mwa Kenya.MwanaKwetu anasema nini siku ya leo?Katika kadhia hii yalisemwa mengi mojawapo ni kuwa Jonah Anguka alikuwa Mkuu wa wilaya siku a tukio hilo na gari lake lilioneka kuweka mafuta mengi, je mafuta haya yalitumika kwa safari za wapi?

“Inawezeka vipi gari ya umma kuwekwa/kubugia  mafua mengi bila ya kuwa na kazi fulani/kazi maalumu? Lakini Mungu bahati Jonah Anguka aliwataja  Rais Danie Moi, Waziri wa zamani wa Kenya marehemu Nicoluos Biwaott kuwa ndiyo waliofanya mauwaji hayo katika kitabu chake cha Absolute Power: The Ouko Murder Mystery, Pen Press, London, 1998, ISBN 1-900796-01-5

Kikubwa mauwaji ya masuala ya kisiasa yanaweza kuambatanishwa na masuala ya maslahi ya kifedha na mapenzi kama kisingizio tu lakini kubwa ni siasa kujificha nyuma yake, 


 ANGUKA& FAMILY

 

ndiyo maana mauwaji ya Dkt Ouko haya yalikuwa ni machache yaliyoibuka;Oyugi – kwa sababu aliogopa kufichuliwa na Dk. Ouko katika ufisadi, Mbajah - kakake Ouko ambaye mke wake alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na Dk. Ouko, Omino – mpinzani wa muda mrefu wa kisiasa wa Dk. Ouko jimboniGondi - mshauri wa kifedha wa Oyugi na alifukuzwa kutoka kazini ikidaiwa kwa uchochezi wa Dkt Ouko. Jonah Anguka – Mkewe Susan Anguka alidaiwa alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na bosi wake yaani Dkt Ouko na ha kuzaa naye watoto wawili wa mwisho ambapo na mgogoro wa mwisho na wakili wa Oyugi

 


Mwanakwetu Upo?

Kumbuka;

“Migogoro Mapenzi Daraja Kukamilisha Mipango ya Watu”

Nakutakia siku njema.

makwadeladius@gmail com
 0717649257




 

 

0/Post a Comment/Comments