MUNGU NDIYE MPONYAJI WA KWELI-PADRI MASANJA

Adeladius Makwega-MWANZA

Wakristo wameambiwa kuwa jumapili ya 23 ya mwaka B wa Kanisa ya Septemba 8, 2024 wanaalikwa kutafakari namna Kristo Yesu alivyohubiri habari njema kisha alivyowaponya watu maana miujiza haikuanza leo lakini miujiza ya Kristo Yesu ilikuwa thabiti maana Mungu ndiye mponyaji wa kweli.

Haya yamehubiriwa na Padri Samsoni Masanja katika Kanisa la Bikra Maria, Malkia wa Wamisionari, Parokio ya Malya Jimbo Kuu Katoliki la Mwanza.

“Hivi sasa wapo wachungaji wengi, wapo mitume wengi na wapo manabii wengi Je uponyaji wao unatoka kwa Kristo Yesu? Yesu aliwaponya watu waliofahamika katika jamii aliyokuwapo wakati huo, siyo uponyaji wa kutafuta nani ameponywa? Tutambue Mungu ndiye mponyaji wa kweli.”

Padri Masanja alisisitiza jamiii yetu iwe makini na hili suala la miujiza ya utata na inaipotosha jamii,I naidhulumu jamii ambalo hilo siyo kusudio la Mungu.

 Kwa hakika misa hiyo ya kwanza ya dominika hii hadi inamaliza saa moja unusu ya asubuhi hali ya hewa ya Malya na viunga vyake kwa juma nzima ni jua la kadili, huku sasa msimu wa kilimo unakaribia kuanza maana wakulima wanakusanya na kuyachoma majani na miti mashamba, eneo hili likipambwa na moshi na huku majivu ya majani yaliyoungua yakionekana mashambani, mbolea zikitawanywa ili kutayarisha majembe la wa kukokotwa na ngombe na trekta kulima mashamba haya ambapo sasa umekaribia msimu wa kilimo cha mahindi, karaga, maharage, alizeti na mazao mengine.





 


0/Post a Comment/Comments