Adeladius Makwega-MWANZA.
Kwa hakika Mwanakwetu kuna siku aliambiwa juu ya sheria na maisha ya mwanadamu tangu Musa kupewa amri Kumi za Mungu na ujio wa Yesu Kristo.
“Tangu Mungu alipowapa Waisraeli Sheria ya Musa, historia imefafanuliwa kwa kushindwa. Agano la Kale linarekodi hivyo, linaomboleza na kufundisha juu ya kushindwa huko, lakini Yesu mwenyewe siku moja alikuwa kwenye eneo akihubiri habari njema. Huenda wale waliokuwa wakisikiliza Mahubiri ya Mlimani walitarajia Yesu atangaze kulegeza Sheria. Labda walitumaini angepunguza Amri Kumi hadi sita. Hata wangetarajia nini, Yesu hakuja kutoka mbinguni na kuomba msamaha kwa ajili ya Sheria ambayo hawakuweza kushika. Badala yake, aliithibitisha Sheria.
Kuna vigezo viwili katika maandiko vinavyoamua kwa nini Sheria ni jinsi ilivyo. Ya kwanza ni, “Kila atendaye dhambi, huvunja sheria; kwa hakika, dhambi ni uasi (1 Yohana 3:4). Sheria inawakilisha shabaha tunayokosa tunapotenda dhambi. Paulo anafafanua kwamba lengo hili ni mbali na la kiholela na kigezo cha pili: "Kwa maana wote wamefanya dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu" (Warumi 3:23). Kwa pamoja, mistari hii inaonyesha kwamba Sheria ya Mungu na utukufu wa Mungu ni sawa na kitu kimoja. Hapa ndipo Sheria inapoingia. Mungu alitoa Sheria ili kudhihirisha tabia yake kwa sababu kwa kufanya hivyo, hii inadhihirisha jinsi tunavyopaswa kuwa. Sheria haisemi, “Usiibe” kwa sababu kuiba sio fadhili, ingawa ni hivyo, lakini kwa sababu Mungu si mwizi ina maana kwamba sisi tulioumbwa kwa mfano wake pia hatupaswi kuiba.
Madhara ya matakwa ya Sheria huwa ya juu sana, yanayodai sana, yasiyo na akili ya kusema kibinadamu ni kwamba inafichua kushindwa kwetu kama wanadamu. Sheria haitufanyi tu kuwa wenye dhambi bali pia inafichua pale tunapokosa alama ya jinsi tulivyoumbwa kuishi. Mungu haonyeshi kushindwa kwetu au kutufedhehesha au kutia pua zetu kwenye uchafu bali ili kwamba tunapotambua dhambi zetu, ili atusafishe na kutubadilisha.”
Haya ni mambo ya kiroho katika dini ya kikristo . Katika ulimwengu wa maamuzi inaaminika ili kufikia maamuzi yoyote yale lazima huyu muamuzi atayafikia maamuzi yake kwanza kwa kuyatengenezea mazingira yakeya kuamua kwa kuangali sheria husika inasemaje katika shauri hilo, pili mazingira ya tukio hilo yalikuwaje hadi kosa husika linafanyika? Mwisho hekima ya muamuzi ikoje katika jambo hilo? Tamati ya hayo yote ndipo uamuzi wa shauri hilo unafikiwa.
Kwa hakika suala la sheria mwanadamu mara zote anakuwa mshindwaji, hata kama kosa limefanyika . Je yule aliyefanya anatambua kuwa amekosea, anajutia hilo kosa hilo? Kwa hiyo yoyote anayeketi katika kiti cha kufanya maamuzi ni jambo la msingi kuwa makini kwa kuzingatia haya mambo matatu ili maamuzi yake yafikiwe vizuri kwa faida ya jamii. Hoja siyo sheria tu peke yake hapo hapana, ndiyo maana katika dini kuna msamaha, msamaha ni hekima.
Mwanakwetu kwa nini anayasema haya yote siku ya leo ?
Kwa sasa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linaongozwa na Msomi wa Sheria Dkt Tulia Ackson na ndiyo mara ya kwanza kwa Bunge letu la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuongozwa na msomi mkubwa kama yeye. Swali la kujiuliza je Bunge hili ni Bunge Bora? Je Watanzania wanavutiwa na Bunge hilo?Je mijadala yake ina mvuto? Watu wengi wanasema waziwazi kuwa bunge hili siyo bora na halina mvuto na wanaonadi hilo wanakwenda mbali wakisema kwa kupanga orodha kabisa.
“Bunge bora lilikuwa lile la mhe. Samweli Sitta, likifuata na la Adam Sappi Mkwawa, likaja la Pius Msekwa, likaja na Anna Makinda, alafu la Job Ndugai na la mwisho linaloburuza mkia ni la Dkt Tulia Ackson.”
Katika hili Mwanakwetu anaona kuwa Dkt Tulia yeye mwenyewe anadhani analiongoza Bunge hilo vizuri, akichagizwa na nafasi za kimataifa alizo nazo sasa. Kwa hakika Dkt Tulia yeye mwenyewe atambue anaichezea shilingi chooni, akumbuke yeye kwa namna alivyo anacheza karata moja ya kusimamia sheria na kanuni tu ambapo kwa mtindo huo hawezi kufikia viwango vya marehemu Samweli Sitta ambaye alikuwa hodari wa kuzicheza karata tatu. Kwa Dkt Tulia hii tabia atambue inaweza hata kuhatarisha Cham Cha Mapinduzi kuamini kuwa yeye ni mtu sahihi kwa nafasi hiyo hapo mbeleni.
Nafuu ya Bunge hili kwa sasa ipo kwa Naibu Spika mhe. Musa Azzan Zungu ambaye yeye anaweza kuzicheza karata tatu ile ya sheria/kanuni, mazingira na hekima kwa hiyo kidogo inaweza kusaidia kufika kwa kuchechemea 2025 na pengine hiyo ikampa nafasi Musa Azzan Zungu kukalia kiti hicho hapo baadaye.Jambo hili sasa linazungumzwa wengine wakisema kuwa CCM haikupata muda wa kutosha kujitathimini wa kukalia kiti cha Uspika baada ya Job Ndugai kuvibwaga vibuyu hadharani.
Haya yote yanaibuka baada ya matukio ya watu wanakufa kiongozi wa Bunge hatoi nafasi ya mjadala, watu wanapotea spika anazima mjadala wa kutekwa bungeni? Spika haoni umuhimu wa mjadala huo? Hilo likinadiwa halikubaliki.
“Pale angekuwepo marehemu Samweli Sitta angeruhusu mjadala huo na wabunge wangejadili hata kama ungedumu hadi saa sita hadi kingeeleweka , hapa ardhini wanakwenda watu-ardhini wamelala watu.”
Wadau mbalimbali wanajadili hoja hizi kwa kina .Maneno ni mengi lakini kwa hakika wenye kujua hatima ya haya yote ni CCM wenyewe, kwake Dkt Tulia atambue sheria/kanuni ni maandishi ambayo hayawezi kupata uhai na kuwa na sifa za binadamu kumtetea , binadau wanatetea hao binadamu wenzao walifariki kupteaau kukumbwa na mabaya, sheria na kanuni zako zimepigwa na kiyoyozi bungeni.
Mwanakwetu upo?
Kumbuka
“Dkt Tulia Dada yangu Acha Kuicheza Karata Moja.”
Nakutakia Siku Njema.
0717649257
Post a Comment