VIJIWENI KUNAENDEKA

 



Adeladius Makwega-MWANZA

Msomaji wangu huu ni wakati mwingine wa kukualika tena katika makala ya katuni, haya yakiwa makala ya uchambuzi yenye katuni nne ambapo zinachaguliwa katika kundi la katuni tele, zinaelezewa kama zilivyo, kisha zinahitimishwa kwa uchambuzi wake kulingana na jicho la mtayarishaji wa makala haya.

Kwa kuyaanza makala yetu siku ya leo, hapa ninaikamata katuni moja inayomuonesha baba aliyekaa katika kiti na watoto wake wakimparamia, naye mama akiwa mjamzito kando , familia hii ni karibu ya watu 10; watoto saba, baba, mama na ujauzito wa familia hii. Huyu mwanaume anasema, mke wangu nasikia, hivi vyandarua tunavyolalia vinapunguza nguvu za kiume? Maneno haya yanasemwa na baba huyu mbele ya watoto wake. Mke wa jamaa huyu anasema- hivi wewe ni mzima kweli?

Katika hili mchoraji wa katuni hili anaibua mambo kadhaa kwako wewe unayeitzaama.Mwanak anakwambia kuwa uwoga na tahadhari nayo ni akili, pia mchoraji wa katuni hii anaibua dhana kuwa kunapotolewa baadhi maelekezo ya afya mathalani hili la matumizi ya vyandarua kujikinga na mbu anayesababisha malaria zipo imani zinaweza kuambatana na maagizo haya, ambapo mara nyingi serikali inatakiwa kujibu hoja mapema na kueleza ukweli hili kampeni husika kufanikiwa na lazima agizo litekelezwe lakini nyuma ya hilo wawepo wadau wengine wanaosaidia kuondoa upotoshaji wa aina yoyote ile. Kwa mfano,

“Wakati wa UJAMAA suala la uchangiaji wa damu lilihusishwa na MUUMIANI ambao ilidaiwa wanawauwa watu na baada ya kuwanyonya damu na kuwagonga mihuri makwapani na hiyo damu ilikuwa inauzwa  bei kubwa kumbuka hii ilikuwa imani na wengine hadi kesho hili wanaliamini.Katika uzushi huu matajiri wengi wa zama hizo walipewa tuhuma za UUMIANI.Kwa sehemu hoja hii ilijibiwa lakini kwa  sehemu hoja hii haikujibiwa na ndiyo maana hadi kesho wapo wanaoamini hivyo.”

Sasa ninaikamata katuni ya pili ambayo inaonesha jamaa wanne, wawili wa katika mazingira ya starehe, naye mwanaume kama anaongea katika simu, mke wangu nimekamatwa nipo kituo cha polisi. Huyu mwanamke anayepokea simu anajibu kuwa mume wangu nipo hapa naelekea kanisani kusali na dada. Mwanakwetu anaitazama katuni hii na hapa mchoraji wake anauliza kati ya mume na mke nani muongo zaidi.Kwa hakika katuni hii inajieleza vizuri naye Mwanakwetu hana cha kuongeza.

Sasa ninaikamata katuni ya tatu ambayo inaonesha jamaa mmoja yupo ndani ya nyumba yake na huyu ni kijana anayatoa maneno haya- kwa hali sasa ishakuwa tete vijiwe sasa basi. Mwanakwetu anapoitazama katuni hii anajiuliza mengi kulikoni tena vijiweni hakuendeki? Je huyu kijana alikimbia nini

Mwanakwetu baadaye alibaini ni wakati ule wamsako wa dawa za kulevya na vijana vijiwe walivioa vichungu.

Msomaji wangu Mwanakwetu akiwa anayatarisha makala haya alimkumbuka Agness Gerald Waya ambaye alikuwa binti mrembo mzaliwa wa Mbalizi Mbeya malkia wa video mbalimbali za muziki aliyevuma sana mwaka 2017 katika wimbo MASOGANGE wa mwanamuziki Bell 9 kutoa video yake wimbo huu uliopakuliwa katika ulimwengu wa muziki mwaka 2011. Maneno ya wimbo huu ni haya

Upo mbali na Masogange
Njoo uutulize mtima wangu
Upo mbali na Masogange eh

Miaka mingi imepita bebii, ila mi sijakuona
Miaka mingi imekatika ma, ila mi sijakuona
Kile kidonda changu cha mapenzi, moyoni bado hakijapona
Nitapata afadhali mi, endapo we nikikuona
Kama warembo mi nawaona wengi, tabia zao mi naona noma
Najaribu shinda vishawishi, nisije mi kukupa ngoma

Bado nakupenda wewe, wapi ulipokwenda
Bado nakupenda wewe, wapi ulikokwenda
Ndo maana nakuimbia popote ulipo sikia bebii, urudi nyumbani
Nakuimbia popote ulipo sikia mami, tuishi kama zamani

Mapenzi yanautesa moyo we, mapenzi yanaumiza moyo we
Mapenzi yanautesa moyo we
Njoo unipoze roho

Mapenzi yanautesa moyo we, mapenzi yanaumiza moyo we
Mapenzi yanautesa moyo we
Njoo unipoze roho

Toka longi taime ego we, nakusaka mrembo we
Nakusaka bebii, nijue upo wapi mama

Wasiopenda kuona mimi nawe, tunapeana rili lavu ni wengi
Hawapendi kuona mimi nawe, kila siku twapeana mapenzi
Wasiopenda kuona mimi nawe, twapendana mai babii ni wengi
Hawapendi kuona mimi nawe, kila siku twapeana mapenzi

Chochote watachokuambia, usiwasikilize
Nakusihi mami puuzia, moyo wangu usiumize
Chochote watachokuambia, usiwasikilize
Nakusihi mami puuzia, moyo wangu usiumize

Endapo ukiwasikiliza, moyo wangu utaumiza
Endapo ukiwasikiliza, utaniacha mi kwenye kiza
Endapo ukiwasikiliza, moyo wangu utaumiza
Endapo ukiwasikiliza, utaniacha mi kwenye kiza haya

Upo mbali na masogange, njoo uutulize mtima wangu
Upo mbali na masogange, njoo uutulize mtima wangu

Mapenzi yanautesa moyo we, mapenzi yanaumiza moyo we
Mapenzi yanautesa moyo we
Njoo unipoze roho

Mapenzi yanautesa moyo we, mapenzi yanaumiza moyo we
Mapenzi yanautesa moyo we
Njoo unipoze roho

Upo mbali na Masogange, njoo uutulize mtima wangu
Upo mbali na Masogange

Upo mbali na Masogange, njoo uutulize mtima wangu
Mapenzi yanautesa moyo we, mapenzi yanaumiza moyo we
Mapenzi yanatesa moyoni, mapenzi yanatesa rohoni

Mapenzi yanautesa moyo we, mapenzi yanaumiza moyo we
Mapenzi yanautesa moyo we
Njoo unipoze roho

Mapenzi yanautesa moyo we, mapenzi yanaumiza moyo we
Mapenzi yanautesa moyo we
Njoo unipoze roho

Wewe, toka long time ago
Nakusaka mrembo nijue uko wapi mama ah
I lavu yuuu

, i nidi yuu !

Kwa hakika msomaji wangu Agness Gerad Waya aliyebatizwa jina MASOGANGE baada ya kuonekana katika video hii , baadaye binti huyu alifanya video kadhaa huku baadaye alikamatwa na kupata misukosuko ya tuhuma za madawa ya kulevya hapa Tanzania na baadaye huko Afrika ya Kusini. Safari ya maisha ya MASOGANGE iliendelea kuyumba na mwisho Agness Masogange alifariki dunia mwaka 2018 mwaka mmoja baada ya kucheza hiyo video ya Masogange.

 

Sasa msomaji wangu ninaikamata katuni yangu ya nne ambayo inaonesha chupa ya maji safi iliyotupwa chini baada ya matumizi. Chupa hii inaonesha kuwa tunafanya matumizi ya chupa za maji lakini tunatakiwa kuzingatia namna ya kuzitupa baada ya matumizi ili kutunza mazingira.


 

Mwanakwetu Upo?

Kumbuka tu hizo ni katuni nne zilizoijenga makala ya katuni siku ya leo, ya kwanza ni ile ya familia ya watu 10, ya pili ni ile ya mke na mume nani muongo zaidi, katuni ya tatu ni ile ya kijana aliyejificha ndani ya nyumba yake akiogopa vijiwe baada ya msako wa wauzaji na watumiaji wa mihadharati na katuni ya mwisho ni hii ya utunzaji wa mazingira, basi hadi hapa ndipo na mimi naufunga huu ukurasa wa makala ya katuni siku ya leo.


 

Kumbuka

“Vijiweni kulikuwa hakuendeki Je sasa Vijiweni Kunaendeka?”

Nakutakia siku njema.

makwadeladius@gmail.com

0717649257



 

0/Post a Comment/Comments