ZINGATIENI USAFI WA MOYO-KANISA KATOLIKI

 


Adeladius Makwega-Mwanza-TANZANIA

Kanisa Katoliki limesema kuwa wakati wa ugonjwa wa Korona dunia nzima ilitambua umuhimu mkubwa wa kunawa mikono na hilo halikuwa tu kumlinda mtu binafsi bali jamii nzima, kunawa mikono ni utamaduni mzuri wa usafi unaofuatwa na binadamu tangu kale, lakini katika domnika ya leo hii Kristo Yesu anatuambia wajibu wetu katika kuzingatia usafi wa moyo.

Haya yamehubiriliwa na Kadinali Luis Antonie Tagle Mkuu na Kiranja wa Propangada Fide ya Kanisa Katoliki Ulimwenguni anayeshugulikia Uinjilishaji wa Watu, katika JesCom TV katika mahubiri yake ya dominika ya 22 ya mwaka B wa Kanisa.

“Yesu anatuuliza tunadhani kwa kuosha mikono mwanadamu anakuwa safi moyoni ? Usafi wa binadamu unatoka ndani ya moyo ambapo mambo mabaya yanaweza kuwepo na huu ndiyo usafi Mwenyeenzi Mungu anauhitaji.”

Akiyataja mambo mabaya yanayomfanya binadamu asiwe msafi moyoni mwake, moja baada ya nyingine katika Kanisa la Bikira Maria Malkia wa Wamisionari Parokia ya Malya Jimbo Kuu Katoliki la Mwanza Padri Samson Masanja aiisema,

“Mawazo mabaya, uasherati, wizi, uuaji, uzinzi, tamaa mbaya, ukorofi, hila, ufisadi, kijicho, matukano, kiburi, upumbavu na mengine mengi.”

Kadinali Tagle awali akipuliza kipenga cha kuanza mahubiri yake aliwakumbusha Wakristo ,

“Katika somo la kwanza Musa aliwasisitiza wana wa Israeli kuzishika Amri Kumi za Mungu, maana hizo amri hazikutoka kwake binafsi bali kwa Mungu, wasiongeze wala wasipunguze kitu. Binadamu anatabia ya kuchukua na kufuata mambo anayoyataka tu, hilo hapana. Katika somo la pili tunakumbushwa kushika neno la Mungu na kuwa na matendo mema kwa kuwasaidia wajane na makisikini.”

Akimalizia mahubri yake katika Kanisa la Bikira Maria, Malkia wa Wamisionari Padri Masanja aliupigilia msumari wa mwisho,

“Hivi leo tunaweza kujiuliza yapo mambo mengi ambayo tunayafanya pengine kwa desturi, pengine kwa mazoea na p engine kwa utamaduni lakini ni mambo ya kawaida kabisa wala hayatugombanishi, wala hayatuchonganishi, wala hayatufanyi kukosa urafiki na wenzetu, lakini yote yanayoleta ugomvi, chuki yanayofanya tusisameheane haya yanatokea moyoni mwetu, mioyo yetu itajaa uuaji, ugomvi, ufisadi kama hatuzifuati Amri za Mungu. Haya mambo kila mmoja ajiulize hayapo moyoni mwake? Neno la Mungu leo hii linatutaka tutoke katika uchafu wa moyo na tuwe safi.”

Kwa hakika msomaji wangu siku ya leo makal haya mafupi yanejaribu tu kupita nawewe katika sehemu ya mahubiri ya Kadinali Luis Antonie Tagle ambaye yupo Vatikani akisimamia ile Idara ya Uinjilishaji wa Watu lakini pia kwa sehemu kile kilichohubiriwa a Padri Samson Masanja ambaye ni Paroko wa Parokia ya Malya Jimbo Kuu Katoliki la Mwanza nchini Tanzania ambapo Misa hii ya dominika ilimalizika majira ya saa 2 kamili asubuhi, ikiwa misa ya kwanza ya Septemba 1, 2024. Nje ya kanisa hilo eneo la Malya na viunga vyake, kwa juma zima hali ya hewa ni ya kawaida lakini nyakati za usiku kuna joto kidogo.

 

makwadeladius@gmail.com

0717649257













 

0/Post a Comment/Comments