Adeladius Makwega-MBAGALA
Nakualika tena katika makala
ya katuni siku ya leo, kumbuka haya ni makala ya uchambuzi wa katuni kama
katuni mbalimbali zilivyochorwa na kuzingatiwa na wachoraji kutoka vyombo
mbalimbali vya Tanzania na Ulimweguni kote. Kumbuka tu uteuzi wa katuni hizi
nne ndiyo huwa mwongozi wa makala haya.
Kwa kuanza kupiga kwata
la gwaride la mwendo wa pole pole, Mwanakwetu anaikamata katuni ya mwanzo kabisa
ambayo inamuonesha mtoto wa Kipanya ambayo ni katuni iliyochorwa na Masoud
Kipanya ikimuonesha kipanya mtoto akitazama ubao wa kubadilishi fedha ukinadi
kuwa Dola moja ya Kimarekani kwa siku hiyo iliuzwa kwa shilingi 2800/- za
Kitanzania.
Mchoraji wa katuni hii
anaonesha kuwa kijana Kipanya akishangazwa na hali hiyo kwa kuonesha kuwa
sarafu ya Tanzania inarudi chini huku sarafu ya Marekani ambalo lilikuwa Koloni
lezetu chini ya Uingereza ikipanda kwa kasi.
Katuni hii inampeleka
Mwanakwetu katika tafakari kubwa juu ya hali ya ubadilishaji wa fedha ya shilingi
ya Tanzania, hivi ilikuwaje hali hii kutoka Dola moja kuwa Shilingi hizo tele?
Kwa hakika kwa hali ya Tanzania jinsi miaka inavyosonga ndivyo hali ya kubadilisha
fedha inavyozidi kuwa chini na fedha yetu zinavyozidi kudolola.
Swali ni je mdololo wa fedha ya Tanzania ukilinganisha na fedha za mataifa kama Uingereza, Marekani na hata Euro ya Ulaya unatokana na nini? Jibu lake ni kuwa zipo sababu kadhaa zinazosababishwa na mdololo huo wa fedha yetu.“Kuna mambo mengi ambayo yataathiri kiwango cha ubadilishaji wa fedha za kigeni. Kwanza, kuna mambo ya kiuchumi kama vile sera za serikali za fedha , viwango vya riba, ziada, nakisi na urari wa malipo na viwango vya biashara, viwango vya mwenendo wa mfumuko wa bei, Pato la Taifa, viwango vya ajira, mauzo ya rejareja na viwango vya uzalishaji kwa taifa.”Kwa hakika hizo ni baadhi ya hoja chache, Mwanakwetu angeweza kuelezea hayo yote lakini kwa faida ya msomaji wake ebu ngoja aelezee Pato la Taifa linavyosababisha viwango vya ubadilishaji fedha vya taifa kulala dolo
“Data chanya za kiuchumi, kama vile ukuaji mkubwa wa Pato la Taifa, zinaweza kuongeza mahitaji za sarafu, na kuifanya kuthaminiwa. Kinyume chake, data dhaifu za kiuchumi zinaweza kusababisha kushuka kwa thamani wawekezaji wanapotafuta njia mbadala zenye matarajio bora.”Kwa leo msomaji wangu katika gwaride la makala ya katuni juu ya katuni hii ya Alwatan Masoud Kipanya ya viwango ya kubadilisha fedha vinatoa nafasi ya kwenda mbele kushoto kulia na naikamata katuni ya pili ambayo inaonesha jozi moja ya viatu vikubwa vyeusi ambapo kwa kando kuna picha ya Mwalimu Julius Nyerere tangu alipozaliwa 1922 na kufariki 1999 katika sehemu ya kuingiza nyayo za mvaaji viatu hivyo kuna picha za watu kadhaa zinazofanana na Rais Ali Hassani Mwinyi (2), Benjamin Mkapa(3),Jakaya Kikwete(4), John Magufuli(5) na Samia Suluhu Hassan(6). Katuni hii imechorwa na Said wa Michael wa Shirika la Utangazaji la Ujerumani -DW KISWAHILI ambapo dhana kubwa inayojengwa ni kuwa marais wote watano baada ya Mwalimu Nyerere wameshindwa kuvivaa na kuwatosha viatu vya Mwalimu Nyerere.
Mwanakwetu anaitazama katuni hii kwa kina na kwa hakika dhana iliyochorwa ni sahihi kwa hoja chache mathalani ya miaka aliyokaa madarakani Mwalimu Nyerere yaani miaka 24; Mwanakwetu anaona kuwa dhana hiyo siyo sahihi isipokuwa usahihi wake ni kwa dhana ya pili kwa kuwa Mwalimu Nyerere alipigania uhuru wa Tanganyika.
Mwanakwetu anaona usahihi wake ni kuwa ebu tuwatazame marais hao mmoja baada ya mwingine wakati wa utawala wao.“Ali Hassani Mwinyi vyovyote utakavyomuona katika mambo mengine lakini alijitahidi kwa uwezo wake kuwa karibu wa wananchi na kusikiliza hoja zao na kuondoa dhana ya utawala wa Mwalimu Nyerere akiwa kiongozi ambaye ilikuwa vigumu kumfikia. Ali Hassan Mwinyi kila wakati alikuwa akisikiliza matatizo ya mtu mmoja mmoja Ofisi Ndogo ya Chama Cha Mapinduzi pale Lumumba ambapo hilo lilimpa heshima tele Mzee Mwinyi.”
Kwa awamu ya Tatu serikali ya Mzee Benjamin Mkapa ilijitahidi mno kuwekeza katika miunndo mbinu ya elimu ya msingi na kuhakikisha watoto wa Kitanzania wenye sifa za kwenda shule wanakwenda shuleni hata kwa lazima huku madarasa na vyumba za walimu na ofisi za shule kadhaa zilijengwa nje nzima, haya yalifanyika vizuri chini ya mpango wa MEMKWA.
Kwa upande wa serikali ya awamu ya nne yenyewe ilipokea vizuri kijiti kutoka serikali ya aw amu ya tatu na kuboresha vizuri elimu ya sekondari chini ya MESS na kujenga shule kadhaa za Kata ambapo hilo limeongeza idadi kubwa ya watoto wa Kitanzania kutoka kaya masikini kupata elimu ya juu hadi vyuo vikuu huku vyuo vikuu kadhaa vya umma na binafsi vikianzishwa.Sambamba na hilo pia maboresho ya miundombinu kama vile barabara, reli ,vivuko vya baharini na maziwani, viliboreshwa sana.Nayo Serikali awamu ya tano iliboresha mno Miundo mbinu hasa barabara na hata ujenzi wa reli bora za kisasa huku miradi kadhaa iliibuliwa na kufanya miradi kadhaa ya serikali kuwa midomoni mwa watu. Kwa hakika sasa twende kwa serikali ya awamu ya sita huku hali ikoje?
Kwa sasa Mwanakweetu kutoa maoni yoyote dhidi ya serikali ya awamu ya sita kwa kuilingansihwa na awamu ya kwanza ni vigumu maana bado inaendelea na majukumu yake tuipe muda hadi 2025 hapo itakuwa wakati sahihi kuona cha kutiliwa maanani. Kwa hakika awamu ya 2, 3, 4, 5 zimefanya kazi kubwa sana kwa taifa hili na huku ukilinganisha idadi ya Watanzania ya 1964 na ya mwka 1985, 1995, 2005 na 2015 watanzania tukizaliana kila uchao.
Sasa Mwanakwetu anaikamata katuni ya tatu ambayo inamuonesha mama mmoja ambaye ana umbo zuri akiwa nywele zake nzuri amepiga dawa maridadi nadhani hii ni TCB RELAXER, Mwanakwetu akiwa katika gwaride la mwendo wa haraka anamuona mama huyu nywele zake mawimbi ni moja kwa moja siyo mkeka, Mwanakwetu anayatamani mawimbi haya ya mama huyu ayashike lakini Mwanakwetu kibali cha kuyashika mawimbi ya nywele hizo hadi amtafute alwataan Masoud Kipanya, hiyo ni Safari ya Kutoka Mwanza hadi Dar es Salaam, kikubwa mawimbi yamekaa vizuri, Mwanakwetu mawimba kama haya ndiyo uchawi wake. Mama huyu amemvutia mno Mwanakwetu, msomaji wangu, mama huyu umbile lake ni kama la Miss Bantu habari zile za ustadhi Kipozeo.
Mama huyu anaonekana ameshuka katika ndege, huku akiwa na vifurushi kutoka Ughaibuni. Kwa kando mama huyu yupo Kipanya na mwanawe wanasema-Tukiendelea na ziara za nje kujifunza. Akimaanisha ndivyo watu wanavyorudi na vifurushi wakienda kujifunza huko Ughaibuni. Hapa kinachomaanisha kuwa wenzetu wanaopata bahati ya safari hizo za kujifunza namna wanavyonufaika. Katuni hii inaonesha kuwa kinachofuatwa si mafunzo bali manunuzi ya vifaa kwa ajili yao binafsi tu.Mwanakwetu anaona kuwa mchoraji wa Katuni hii anaibua hoja ya gere kwa wanaokwenda huko, Mwanakwetu anasema sasa ni wakati sahihi tumpatie Masoud Kipanya Sfari hiyo ili asituchere wale tunaokwneda sana ughaibuni na kurudi na vifurushi.Sasa Mwanakwetu anaikamata katuni ya nne ambavyo ni kimataifa hapa amechorwa mama mmoja ambaye amevalia nguo za kijeshi huku akiwa ameshika rungu moja machachari mno,mama huyu amrvaa kijeshi, mama huyu anajitazama katika kioo huku kiunoni anaonekana mama mmoja ameva suti maridadi na hijabu moja nzuri nadhifu inayomvutia Mwanakwetu.
Mchoraji wa katuni hii amepachika jina la Samia katika kombati za, huyu mama mwenywe sare za kijeshi kwa hakika sura yake inashabiana nay a Rais Samia Suluhu Hassan.Kwa hakika mchoraji wa katuni hii amechora picha inashabiana na Rais Samia Suluhu Hassan, kwa kumuonesha katika taswira mbili tofauti moja kama kiongozi mwenye aiba ya kijeshi na pili kiongozi w a kiraia. Swali ambalo mtayarishaji wa makala haya anajiuliza je inakuaje huyu mchoraji wa katuni hii anaonesha taswira hizo mbili za Rais Samia huku akitambua Rais Samia ni kiongozi wa kiraia nah uku uongozi huo wa kiraia unampa nafasi ya kuwa Amiri Jeshi Mkuu. Kwa hakika Mwanakwetu yu njia panda ipi ni sura halisi ya Rais Samia?Hii yenye magwanda na au taswira ya ndani ya kioo ile ya kiongozi mwenye suti maridadi ?
Kwa hakika kitendo cha mchoraji wa katuni hii kuzionesha hizo taswira mbili kinaonesha wazi kuwa mtazamaji wa katuni hii anayo nafasi ya kuamua ipi ni taswira halisi ya Rais Samia? Kwa hakika mtayarishaji wa makala haya taswira anayoitamani si hii ya rungu bali nib alii hii inayoonekana katika kioo.Rais samia akiwa amevalia suti maridadi na hijabu yake huku akibeba sanamu ya mwenge.Mwanakwetu anaibeba katuni hii kama ilivyo kwa msomaji wake kuamua taswira halisi ya Rais Samia,lakini pia Rais Samia mwenyewe anao wajibu wa kujipima Ipi ndiyo taswira yake Halisi?Basi msomaji wangu siku ya leo nilikuwa na katuni nne ya kwanza ni ile ya viwango vya kubadilisha fedha, ya pili ni ile viati vikubwa vya Mwalimu Nyerere, ya tatu ni ile ya mama mwneye nywele za mawimbi na vifurushi mkononi na ya nne ni ile ya taswira mbili za Rais Samia. Mwanakwetu Upo?Basi hadi hapo ndiyo napiga saluti ya mwisho ya makala haya ya katuni siku ya leo Kumbuka“Taswira Halisi ya Rais Samia.”Nasema,“Ahlan Wa Sahlan.”
makwadeladius@gmail.com
0717649257
Post a Comment