MJUMBE ANAYEANDIKIA MKONO WA SHOTO

 



Adeladius Makwega-MBAGALA

Oktoba 3, 2024 Mwanakwetu alikuwa anajiandaa kuyatayarisha makala ya katuni, akiwa anaweka mambo yake sawa na tayari keshachagua katuni zake nne alipigiwa simu na bwana mmoja , ndugu yake na rafiki yake akimsalimu, huku akimpa taarifa kuwa huko Mbagala kulikuwa na msiba kwa Bwana Mkubwa anayefahamika kama SABU KILINDO alifiwa na mtoto wake kwa ajali ya bodaboda mkoani Dooma, hivyo mazishi yamefanyika Mbagala.

Jamaa huyu akasema,

“Watu wengi wa Mbagala walikuwapo isipokuwa Makwega, Watu wakawa wanaulizana Makwega yupo wapi?”

Mjadala ukawa na utani na visa vingi vya zamani vyenye vituko kedekede, majibu yakatolewa Makwega yu Mwanza anakunywa maziwa ya ng’ombe za Wasukuma.

Msibani kulikuwa na watu wengi wa idara tofati za serikali- jamaa mmoja akasema  mnamjua Makwega ? Jamaa wakajibu aaaaaaaha Makwegaaaa tumesoma naye na  tumekua naye alikuwa anakaa pale, jamaa aliyeuliza swali akatoa simu yake janja akawaonesha picha ambayo wapo watu kadhaa, akawauliza yu wapi hapa pichani? Jamaa akajibu huyu hapa mwenye matege, stori zikawa nyingi msibani.. Jamaa wakaiomba picha hiyo na kutumiwa kwenye simu zao, watu wakazika na kuondoka zao huku Mbagala Mangaya

 


 

Miongoni mwa jamaa waliyotumiwa picha hiyo ndiye anayeongea na Mwanakwetu kwenye simu , tukaongea mengi juu ya msiba huo na mambo mengine ya Mbagala, alafu akanitumia picha hiyo na kuagana naye.

Picha hii ya mwaka 2018 inaonekana watu 13 na nilipoitazama nikakumbuka mengi huku nikiwaona ,

“Mh Martine Shigella, Injinia Zena Said, kuna Amiri Mkapanda hawa wana nafasi kubwa Serikalini kwa sasa nikamuoa na jamaa mmoja kutoka vyombo vya Ulinzi na Usalama  mkoa wa Tanga wakati huo.”

Nilitamani kumjua aliyewapa picha hii lakini sikumfahamu kwa maana picha hii walitumiwa kwa Brootooth.


 

Katika picha hii watu wote 13 ninaweza kuwasimulia kwa kurasa hata tano kila mmoja lakini nikasema ngoja nimtazame mtu mmoja ambaye yupo nyuma ya Injia Zena Said- ni mweupe sana, huyu jamaa alikuwa miongoni mwa wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Tanga wakati huo,

“Jamaa mmoja mpole, mwaminifu, mtiifu , mkweli na mchapakazi ambaye anaandikia mkono wa shoto lakini uungwana wake ukifanya na kazi utauoni mithili y mtu anayeandikia mikono yote kila siku; Huku makazinikkuna watu wengine anakungoja ukosee hili uharibikiwe siyo huyu jamaa , yeye anakwambia mapema kabla haujakosea na kuonesha njia ya kupita”

Msomaji wangu nilikumbuka nikiwa Lushoto jamaa huyu alinipigia simu Mkurugenzi eehh hawa jamaa wa Mwenge kunakitu hakijakaa sawa, ebu fanya hivi na vile kama alivyoshauri mama yangu hapo , mambo yawe sawa mdogo wangu sawa nikajibu sawa-Kweli Mwanakwetu alitekeleza hivyo na mambo yakawa sawa.


 

Kwa hakika msomaji wangu kwa leo yatosha, kesho nayo ni siku. Nikasema nikusimulie juu ya picha hii ya mwaka 2018 Lushoto Mkoani Tanga-Nikiwa nyumbani kwangu nikaamua kuyatayarisha makala haya

 

Mwanakwetu Upo?

Kumbuka,

“Mjumbe Anayeandikia Mkono wa Shoto .”

La hawla Wala Quwwata.

makwadeladius@gmail com

0717649257

 


 

NB La hawla Wala Quwwata.-maana yake There is no Power and no strength except with GOD-Hakuna mwnye uweza na nguvu zaidi ya Mungu


 

 

0/Post a Comment/Comments