MSIMKATIE MAMA LAKE TAWI

 


Adeladius Makwega-MWANZA

Msomaji wangu huu ni wasaa mwingine wa kukualika katika makala ya katuni ambayo ni mkusanyiko wa katuni nne zilizochaguliwa na mtayarishaji wetu na kuwa sehemu ya ujenzi wa makala haya siku ya leo.

Kuyaanza makala haya Mwanakwetu anapia kipenga chake akiwa amekamata katuni inayowaonesha jamaa wawili wapo katika mashindano ya mbio ya riadha, jamaa mmoja mavazi yake ni kijani na jamaa mwingine mavazi yake ni mekundu, mbio znapoanza huyu mwenye mavazi mekundu fulana yake maarufu kama kaawoshi inakamatwa na kiatu kikubwa kama buti la polisi na hicho kitendo kinampunguzia kasi mkimbiaji huyu mwenye jezi nyekundu hivyo hivyo mkimbaji mwenye kijani anausogelea ushindi.

 Huyu mkimbiaji mwenye kijani ni chama tawala hivyo lazima shinde hizo mbio za siasa kwa mpinzani wake mwenye jezi nyekundu. Kwa hakika bila woga katuni hii inakemea vyombo vya Ulinzi na Usalama kuacha kuvipunguza nguvu vyama pinzani na hukoni kuvipa nguvu harama vyama tawala na hilo halipaswi kuwa jukumu la vyombo hivyo.


 

Mwanakwetu anaivuta katuni ya pili ambayo inamuonesha mpinzani akiomba kura kwa wapiga kura wake huku huyu mpinzani kumbe anaungwa mkono na chama tawala na kumbe hata baadh ya huduma anapewa na chama tawala. Mwanakwetu anasema kama chama pinzani kinapewa chochote lazima kiwe rasmi kwa mujibu wa sheria kama vile ruzuku ambayo ipo kwa mujibu wa sheria iliyopitishwa na Bunge. Utoaji wa fedha zozote kwa siri kutoka kwa vyama tawala kwenda chama pinzani au kwa mtu mmoja hiyo ni hujuma maana yake huo ni hujumu uchumi. Inawezekana isiwe hujuma kama mchango huo umeombwa hadharani kwa kidugu kufanikisha jambo fulani katuni hii inalikemea hilo na lisifanyike.

Katuni ya tatu sasa ipo viganjani mwa Mwanakwetu, Hapa kuna jamaa kavaa kofia kaziba surayake na yupo juu ya tawi analikata na kuna mama ambaye yupo kando ya tawi hilo, huyu jamaa hajulikana sura yake janadume limevaa sarawili na huyu mama kavaa viatu vyake vya koooo , gauni zuri na kichwani kama atakuwa na hijabu au kilemba

lakini mama hajulikania sura yake, sasa hili janadumu linakata tawi ili mama anguke bila aibu, sasa mama akiaanguka fedhea itakuwa kwetu sote.Kwa hakika huyu jamaa aliyejificha sura anamfutia balaaa mama kando, sasa kwanini huyu jamaa anayekata tawi hasivui  kofia yake, alafu alikate hilo tawi? Mwanakwetu anamshauri mkata tawi avue hiyo kafia alafu aendelee na kazi yake, lakin kazi hiyo haina tija kwa Mwanamme kumkatia tawi Mwanamke.

Mwanakwetu anaivuta katuni ya nne na ya mwisho ambapo kunaonekana watu watatu mmoja kavaa suti, mwingine kavaa sare kama askari na mwingine kavaa misurupwete.


 

Maneno yanasemwa na mvaa suti MNYONGE- Askari anauliza unamaanisha anaitwa MNYONGE AU NIMNYONGE? Kando huyu jamaa yupo juu kigoda tayari kutundikiwa KITANZI kamba ya kunyongewa ambaye tayari askari huyu anayo mkononi. Kwa hakika katuni hii imechorwa na Mtanzania Masoud Kipanya Katuni imefanya Mwanakwetu kukumbuka mambo kadhaa kwa Tanzania, kwanza hukumu ya KUNYONGA hadi kufa ni hukumu halali kwa mujibu wa Sheria za Tanzania , hapa kwetu hukumu hii imeshatekelezwa kwa vipindi vinne wakati wa Mjerumani, wakati

Mwingereza, wakati wa Mwalimu Julius Nyerere na wakati wa Ali Hassan Mwinyi, Ambapo baadhi ya wanaopinga Mwalimu kupata hadhi ya Utakatifu Katika Kanisa Katoliki,huu  uteketelezaji wa kipindi cha utawala wake hukumu hiyo imemchafua mno Mwalimu Nyerere ikidaiwa baadhi ya Marais Wakatoliki wa Tanzania baadaye hawakufanya hivyo. Utaratibu wa kunyonga kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mujibu maelezo yaliyotolewa na Jaji Mstaafu Joseph Warioba katika Tume ya Rushwa ya mwaka 1996 alisema maneno haya;

“Mtuhumiwa akisha tenda kosa, kesi inapelekwa mahakamani hadi hukumu ya kunyongwa , anapewa nafasi rufaa alafu akishindwa rufaa yake au asipokata rufaa, faili la KUNYONGWA anapelekewa RAIS, Bwana /Bibi mkubwa akiruhusu Shughuli hiyo inakwenda kutekelezwa na Jeshi La Magereza Tanzania.Mara nyingi Jaji aliyehukumu hivyo hualikwa siku ya tukio hilo.”

Ndiyo maana baadhi ya Wakatoliki wanaopinga Mwalimu Nyerere kuingizwa katika mchakato kuelekea utakatifu wanapinga vikali. Je Mwalimu alikuwa hajui msimamo wa kanisa lake juu ya hukumu ya kifo? Mbona aliweka mkono wake kunyongwa kwa watu kati 1-8 ?Katika utawala wake? Kwa hakika hilo tuliachie Kanisa Katoliki kumpima ndugu yetu Juius Nyerere juu ya hiliBasi msomaji wangu hizo ni katuni nne za leo; ya kwanza ni ile mbio ya chama tawala na wapinzani inayorudishwa nyuma na askari, katuni ya pili ni ya mpinzani anahongwa na chama tawala , katuni ya tatu ni ya yule jamaa aiyeficha sura akikata tawi alilolikalia huyu mama na katuni ya nne ni hii ya mnyonge. Basi kwa katuni hizo nne ndiyo na mimi natia nanga ya makala ya kutuni siku ya leo.

 

Kumbukeni  sana-

“Msimkatie Mama Lake Tawi”

Nakutakia Siku Njema.

makwadeladius@gmail.com

0717649257

 


 



0/Post a Comment/Comments