SINTOWAACHA NYINYI YATIMA

 



Adeladius Makwega-MBAGALA

Kwa hakika kwa umri wangu huu, mimi Mwanakwetu ni miongoni mwa watu wachache waliyosikiliza hotuba nyingi za Mwalimu Julius Nyerere ambazo zimewahi kuhifadhiwa. Msomaji wangu unaweza kutilia shaka hilo lakini hilo msomaji wangu leo ndiyo nakwambia na ndiyo ukweli. Miongoni mwa mambo ambayo inaonekana sana Julius Nyerere alipigia kelele ni Ukabila na Udini ambapo hata mwalimu Nyerere aliwahi kutuhumiwa kwa haya mambo mawili.

Kumbuka msomaji wangu kutuhumiwa siyo kufanya jambo lakini pia swali ni kwaniNI utuhumiwe ? Je ni husuda, je hila, chuki au nini dhidi ya utawala wako? Ukiwa mtawala wa ngazi ya juu ukituhumiwa tu hapo shida inaanza na imani dhidi yako inapungua na hata ukijitetea kiasi gani wachache wanaweza kuamini katika huo utetezi.

Ndani ya maisha ya mwanadamu  haya mambo mawili ya dini na kabila ni mzizi wa kufaya baadhi ya watu wasimame na wewe na wengine waanguke, hilo msomaji wangu mimi nakubaliana nalo mia kwa mia maana kwa uzoefu wangu katika maisha hilo nimejifunza tangu nikiwa kijana mdogo. Kwa hakika msomaji wangu tambua haya mambo yapo na yanatumika mia kwa mia .

Nakuomba nikuulize swali dogo tu kwanini msululu wa Marais wa Tanzania Tangu Uhuru Nyerere 1964-1985(Mkristo) Mwinyi 1985-1995(Muisilamu), Mkapa 1995-2005(Mkristo) Kikwete 2005-2015 (Musilamu) na Magufuli 2015- (Mkristo) ambaye alitarajiwa amalize 2025, Swali la kujiuliza kwanini isingekuwa Waisilamu wawili wanaongozana au Wakristo wawili Waongozane?Msomaji wangu hilo halionekani na vigumu kuwa hivyo au tuseme hivi waongoze wapagani kadhaa hilo abadani.


 

Msomaji wangu natambua sasa tupo pamoja-nakumbuka nikiwa chuo kikuu jamaa mmoja akasema;

“Makwega tukimchagua pagani jamaa wa Makanisa na Misikitini watatunyima kura.”

Nikamuuliza ndugu yangu huyu;

“Je kama ikifika siku mkamchagua Mkristo jamaa Misikiti wakigoma si mtashindwa uchaguzi mchana kweupe? Je hali itakuwaje? Hamuoni hapa kama hapa mnaujenga udini?Nyinyi pia wadini, lakini wadini wa siri siri ”

Jamaa huyu akasema ;

“Makwega ungeenda kusoma Political Science .”

Mwezangu huyu siku hizi ni Profesa, natambua kwa makala haya pengine swali hili atakutana nalo kutoka kwa kwa wanafunzi wake na atalijibu-PROFESA ANDAA MAJIBU MAPEMA maana wasomaji wa makala haya ni watu kati 7000-13,000 lazima watakuwepo wanafunzi wako. Msomaji wangu nakwambia kweli kabisa udini  na ukabila katika siasa ni mkubwa mno, lakini binadamu ana desturi ya kubekwa lakini vitendo vinakupa majibu, swali ambalo Mwanakwetu analijibu je kati ya DINI & KABILA kipi kipo juu ya mwenzake? Kulijibu swali hilo ndiyo inayajenga makala haya siku ya leo. Msomaji twende taratibu wangu wewe tilia maanani visa hivi viwili vya kweli ambapo Mwanakwetu shahidi kuona shahidi kushuhudia.


 

Kimoja ni cha 2019-2023 na kingine cha 2001-2003.

“Mwaka 2019- 2023 nilikuwa nasali Parokia ya Chamwin Ikulu Jimbo Kuu Katoliki la Dodoma, Katika Maisha yangu nimebatizwa Parokia ya Nansio Murutunguru Ukerewe-Jimbo Kuu Katoliki la Mwanza, Komuniyo na Kipaimara nimepata Parokia ya Mbagala Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam nyumbani kwa baba, lakini nimesali majimbo mengi kwa sababu shule &kazi;Tunduru Masasi, Kigoma , Iringa, Mbeya, Same, Arusha Moshi, Tanga, Dodoma, Mwanza, Cologne na majimbo mengine niliyoyasahau ya Tanzania na ughaibuni.

Nikiwa parokia ya Chamwino Ikulu Paroko alikuwa Padri Paul Mapalala ambaye alikuwa Msukuma na nadhani hakuwep Parokia hiyo hapo awali, alihamishiwa hapa baada ya eneo hilo kuwa na mwamko mkubwa wa kisiasa, kimaendeleo na makao makuu ya nchi ya Tanzania, . waamini Wakatoliki wengi kwa Dodoma ni wahamiaji na wachache wenyeji maana Dodoma ni ngome ya Kanisa la Anglikan, tangu ujio wa Wamisionari. Padri Mapalala alikuwa Padri mtulivu sana, waamini walikuwa wakisema na Padri ambaye ni mwanajeshi lakini ,Mwanakwetu hilo hakulihakikikisha lakini nadhani ni ule ujirani wa Padri Mapalala na marehemu Rais John Magufuli aliyefariki 2021 kama ilivyokuwa kwa Padri Makubi wa Parokia ya Oysterbay Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam,

Padri Mapalala alikuwa na mahubiri mafupi sana na ndiye Padri niliyemfahamu maishani mwangu kuwa na mahubiri mafupi,hata mke wangu ambaye ni mjuzi wa asuala ya kimahakama aliwahi kuniuliza mbona stori ni ndefu wakati amehubiri kidogo?Nikawa nampa majibu kuwa japo maombi na matangazo kanisani Kwa kipindi chote sikuwahi kushuhudia akihubiri kwa dakika 30. Kwa hakika mara zote ninapokuwa kanisani huwa narekodi mahubiri, maombi na matangazo ambayo nayatumia kutayarisha makala mbali mbali na ripoti mbalimbali za dominika na sikukuu za kanisa, nia ni Uinjilishaji katika vyombo vya habari na mitandao ya kijamii ambapo nilijifuza haya nikiwa RTD na DW KISWAHILI. Padri Mapalala alipokuwa na jambo la kusisitiza alikuwa anasema kwenye mahubiri kidogo au wakati wa matangazo, ‘Jamani sasa watani wangu Chamwino ni eneo lenye mchanganyiko wa watu tuendeshe parokia yetu kisasa’ muda mwingine waamini wanaguna, Padri huyu Siyo Padri ya mambo ya kidunia, hawa waamini wezangu wenyeji wanaguna nini?.Ukiwauliza nini hawana majibu, Mwanakwetu akabaini hawa waamini wakidhani yeye ni Msukuma kumbe mie wala siyo wa Mwanza mie natokea Dar es Salaam na kibaya zaidi wakisikia zile ripoti za Jumapili redioni na kwenye magazeti na mitandaoni wanatambua huyu ni ndugu yake, anampaisha Msukuma mwenzake. Kumbe mimi huyo Padri hanifahamu wala mimi simfahamu, wala namba yake ya simu sina. Mie naandika na kutayarisha ripoti za kanisa tu nikimkuta Padri mgeni haya, iwe katekista twende kazini awe Sista mie naripoti tu . Baadaye mie Mwanakwetu nikapata barua ya uhamisho kazini kwenda Mwanza.Nikafaya maandalizi yangu vizuri ya kwenda Mwanza inanibidi niwaage Wakristo wezangu kwenye jumuiya, nikaenda jumuiya nikasali, wakati wa matangazo nikanyoosha mkono, Mwenyekiti wa Jumuiya Kijana mmoja makini sana, akasema  Mwenyekiti wa UWAKA una nini? Nikasimama, nikawasalimu kisha nakusema mimi nawaaga,nimepata barua ya uhamisho nimehamishiwa Mwanza-Mama mmoja akacheka akasema Mwenyekiti wa UWAKA unaondoka na Paroko wako? Nikashituka kumbe na paroko naye anahama? Wakanisalia pale na kunishukuru-Wakisema Makwega na huko Mwanza usisahau kanisa lako, nikasema sawa. Wakati tunatoka nikamuuliza yule mama aliyesema naondoka na paroko wangu nikamuuliza kwanini umesema vile? Kwani Padri nayeye anahama? Mama huyu akajibu akasema yule ni Msukuma mwenzako na wewe unarudi kwenu Mwanza?Je mnakwenda naye Mwanza ? Nikamjibu mama mimi nakwenda Kwimba Mwanza sifahamu Paroko anahamia wapi? Mimi nina chofahamu yule paroko wetu hata kabila lake silifahamu, wala namba yake ya simu sina zaidi ya huduma zake kwangu za kiroho.

Mama huyu ni mfugaji mzuri wa kuku wa kisasa,nikamwambaia hapa Dodoma mimi ni nyumbani maana nimezaliwa hapa na mama yangu ni Mgogo lakini baba yangu Mpogolo.

Padri Mapalala ninamfahamu kama Padri tu anayenipa huduma za kiroho, mama huyu anacheka narudia tena na hata namba yake ya simu mie sina.Mama huyu mfuga kuka anasema yule ni ndugu yako kila siku anatajwa yeye katika vyombo vya habari na mitandaoni, mimi namjibu  mama hapana. Nikawa namwambia mama huyu kuwa mimi kuwa ninamrushewana Bwana Yesu.Baadaye nikaenda Mwanza. Baadaye Parokia hii nilibaini ilipata paroko mwingine ambaye hakuwa Mgogo bali Muhehe.Kila nilipokutana huyu mama namtania na ehee MDALA (mama) mmepata Paroko Mgogo?Mama anacheka, nikawa MTANI MKUBWA WA MAMA HUYU nikawa nasema  mama pelekeni watoto seminari ili muweze kuchagua vizuri mapadri-mie mwenzetu sijawahi kusalishwa na padri Mpogolo.Nikawa namwambia Jamii ya Wakatoliki Wagogo mlitamani kupata Padri Mgogo sasa katoka Msukuma Kaja Muhehe alafu atakuja Padri Mpogolo hapa haji Mgogo.Kwa hiyo Kila nikienda Parokia ya Chamwino Ikulu huyu mama jirani lazima nimtafute haya mama vipi umeshapeleka kijana seminari? Mama wa watu anacheka na husuda ya Padri wa Kigogo.”

Sasa msomaji wangu nikupeleke katika kisa cha Pili cha mwaka 2001-2003 kumbuka hiki cha Parokia ya Chamwino Ikulu ni kisa cha kwanza naodha ni mama mfugaji wa kuku.

“Mwaka 2001-2003 Kipind hichi Mwanakwetu nilikuwa nasoma Chuo cha Ualimu Kasulu Stashahada ya Ualimu huku nikiwa Rais wa Serikali ya Wanachuo, mwaka 2003 nakaribia kumaliza chuo kikafika kipindi cha uchaguzi wa viongozi wa wanachuo, vijana wengi wakachukua fomu kugombea nafasi hiyo, miongoni mwao alikuwa Mwenyekiti wa Wakatoliki, lakini kabla ya uchaguzi huo, uchaguzi uliotangulia yaani 2002 yaani niliyoshinda mimi ulikuwa mgumu sana maana niligombea na kijana wa Kisukuma anayeitwa Majondo Miligwa. Wakati huo chuo hiki wanachuo wengi walikuwa wanatokea Mwanza, Shinyanga na Kigoma ndiyo kusema Waha na Wasukuma walikuwa wengi huku Waswahili tulikuwepo wachachemno, hapa Mwanakwetu nilishinda kwa kuwa kadhaa na nilikuwa maarufu kwa sababu ya nilikuwa mwandishgazeti la kila wiki la chuo- stori katika gazeti la chuo ulikuwa mtaji wa Mwanakwetu. Ngome ya Wasukuma ilikuwa inashinda kabisa lakini Mwanakwetu nikawazidi keti kwa umaarufu wangu wa awali. Mwaka 2003 watu wamechukua fomu zimejazwa, zikarejeshwa majina mawili yakatajwa lakini yule mwenyekiti wa Wakatoliki jina lake halikurudi, hapo Mkuu wa Chuo Alphonce Mbonigaba na wakufunzi wanatambu sababu, majina yaliyorejeshwa yakawa la Mkatoliki Mmoja na Mlutheri Mmoja. Huyu Mlutheri alikuwa Muha wa Kigoma, mtu mzima , mtumishi wa serikali anajiamini, kama askari fulani hivi- sasa ni marehemu na huyu Mkatoliki alikuwa anatokea  Mbeya+Iringa kama sijakosea.Kumbuka Mwanakwetu Mkatoliki kumbuka pia yule mwenyekiti wa Wakatoliki jina lake limekatwa-limepigwa mkasi,  kesho uchaguzi , Mwanakwetu nikawa najiepusha sana kuchagua upande,watu 500-800 linaweza kutokea balaa lakini watu wanataka nisema- Mwanakwetu akawa bubu wa muda watu wanasema MC KAWA BUBU- kama Mzee Zakaria Kuhani wa Mungu.Majira saa 1 usiku tunasali TYCS,tukafika darasani tukasali vizuri tukamaliza ibada, sasa wakati wa matangazo umefika, Jamani kesho tuna uchaguzi, mnaomba kushiriki huo uchaguzi lakini wako wenzetu wanaogombea nawaombeni tumualike Adeladius Makwega ambaye ndiye Rais wetu na kiongozi wetu wa sasa anayemaliza muda wake, nafasi yake baada ya kesho atachaguliwa mwingine , sasa kaka Makwega aseme neno. Mwanakwetu kasakiziwa mbuyu wenye meno watafune, aseme neno abadilishe upepo na ukifanya utani watu wanaweza kuuwana mwisho unatiwa hatiani.Nikiwa nasimama nikawasalimu TYCS Mapendooo!Jamaa Wakajibu Daimaaaaa! ‘Jamani kweli tuna uchaguzi, naombeni itakapo pigwa kengele ya kwenda bwaloni, kesho kukicha tukapige kura, natambua wapo hapa walijitokeza kujaza fomu kugombea nafasi hiyo lakin majina yao hayakurudi kwa sababu zinazofahamika na Uongozi, haya mambo Mungu ndiye mpangaji lakini wapo ambao majina yao yamerudi, natambua mnasoma nao, mnaishi nao kila siku mabwenini na madarasani hapa hapa chuoni, jamani mkapige kura, uamuzi ni wenu, mimi binafsi ninawashukuru Wakatoliki wezangu hadi hadi hapa nakwenda kukabidhi majukumu ya watu hakukuwa na mgomo wowote ule wala mtu kufukuzwa natambu yupo aliyefariki marehemu Eliudi Mwakalili tu Mungu ailaze roho yake maali pema peponi,jamani Mungu awabariki.sana TYCS Mapendoooooo-Daiiimaaaa.”

Kumbuka tupo chumba cha sala nikasema Tumsifu Yesu Kristo  Wakajibu milele amina yakapigwa makofi mengi sana, hapo hapa Mwanakwetu nikabaini jambo. Kiongozi wa Kwaya TYCS alikuwa dada yangu mmoja anaitwa Esperansia Rubandanya akaanzisha wimbo huu-Sitawaacha nyinyi yatimaaaa naja kwenu mioyo yenu ijae furahaaaa .


 

Tukasali nakukimbilia na kutoka kuelekea mabwenini, siku-Njiani wana TYCS wanasema Mwenyekiti Umekuwa Popo, siku ya uchagzu ilifika zikapigwa kura katika vijana wale wawili wa Mbeya+Irnga na Kigoma yule wa KIGOMA alishinda kwa kura nyingi. Katika hesabu za Wakatoliki walikuwa wengi na wengi wao walikuwa Waha. Kwa hakika wengi walioshuhudia haya wapo hai watakuwa mashahidi wa haya yaliyoandikw.

 


Mwanakwetu anasema nini siku ya leo?

Kwa hakika shabaha ni moja tu nakueleza katika chaguzi na mambo kadhaa ya maisha ya binadamu upo Udini upo ukabila rejea kisa cha Padri Mapalala Parokia ya Chamwino Ikulu na rejea huu uchaguzi wa Rais wa Serikali ya wanachuo chuo cha ualimu Kasulu mwaka 2003, kiukweli binadamu hatuambiani ukweli , hatuifungui mioyo yetu.Dunia tunakaa kipindi kifupi sana tuambiene ukweli na ndiyo maana nimekusmulia juu ya visa hivyo.Binadamu wengi ni aakabila sana alafu ndipo udini unafuata/

Mwanakwetu Upo?

Kumbuka

“Sintowaachi Nyinyi Yatima”

Nakutakia Siku Njema.

makwadeladius@gmail .com

0717649257

 




 



 



 

0/Post a Comment/Comments