TANZANIA TUPO SALAMA

 


Adeladius Makwega-MBAGALA

Kati ya mwaka wa 2013-2015 Mwanakwetu alishiriki katika mazishi ya misiba mitatu ya koo tatu za Kisambaa halisia; msiba wa kwanza ulikuwa eneo la Bumbuli ambapo Mzee Hemba alifariki dunia , hii ni familia rafiki na Mwanakwetu- hivyo alikwenda kuzika, siku hiyo wakati wa kwenda alipanda gari ndogo hapo Soni hadi Bumbuli na kupanda Bodaboda hadi mlimani jirani na KKKT Usharika wa GOSHENI, kwaya Gosheni huwa inaimba na wakati huo KKKT DKMs inaongozwa na Askofu Stephern Munga, wakati anarudi Lushoto siku hii Mwanakwetu alidoea usafiri wa gari la Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto Tanga maana mtoto wa mzee Hemba alikuwa na mtoto wake Mfamasia wa zahanati ya chuo hiki cha mahakama siku hii Mwanakwetu alipanda Land Cruzer 1hz rangi ya udogo,

Safari za Mwanakwetu kuzika hazikuia hapo pia alishiriki mazishi ya mama mmoja Mwinjilisti ambaye alifariki huko Arusha Mjini, usafiri wa kwenda na Kurudi Mwanakwetu Mdowezi alidoea gari la Baba Askofu Mstaafu Joseph Jali na safari za maziko zikaongezeka na msiba wa tatu Mwanakwetu alikwenda kuzika Mazinde-Mombo ambapo nadhani dada wa Baba Askofu Mstaafu Jali alifariki dunia. Wakati wa kurudi Lushoto Mwanakwetu alidoea usafiri wa Mchungaji Mwinuka maana wakati huo Rev Mwinuka alikuwa Katibu Mkuu wa Dayosisi ya KKKT-DKMs.

Mwanakwetu pia anakumbuka;

“Siku moja kabla ya mazish ya msiba huu akiwa Mazinde Mombo, Baba Askofu Mstaafu Jali alitutafutia nyumba ya kulala ambapo wababa wote tuliotoka Lushoto tulilala sebuleni katika nyumba moja baada ya kutandikiwa magodoro, nyumba hii nadhani ni ya miongoni mwa watumishi wastaafu wa vyombo vya Ulinzi na Usalama na Mshariki wa KKKT Mombo. Siku ya mazishi tulikunywa chai hapo hapo na baadaye kurejea nyumba yenye msiba alafu Kanisani na kisha kuzika makaburini ambapo makaburini Mwanakwetu aliumwa na nyuki. Baada ya mazishi haya ndipo akadoea ile gari ya Mchungaji Mwinuka.”

Maisha yaliendelea na kipindi chote cha misiba hiyo mitatu Mwanakwetu alikuwa akitokea Dar es Salaam mtumishi wa RTD. Kwa hakika hata matangazo ya vifo ya misiba hii Mwanakwetu alimpigia tu simu mtu wa matangazo na kutuma malipo na yakatangazwa.


 

Mwaka mmoja baadaye yaani 2016 akawa mtumishi wa  Halmashauri ya Lushoto, akiwa kazini huku ikitokea misiba mingi ambayo siyo sehemu ya simulizi hii lakini mapema mwaka 2018 huko kata ya Ngwelo binti mmoja mwalimu wa Shule ya Msingi alijinyonga.

“Matukio ya kujinyonga yakitokea kwanza Jeshi la Polisi Tanzania na Matabibu wanatimiza wajibu wao, alafu ndipo,kisha mnakabidhiwa mwili kwa maziko.”

Msomaji wangu kumbuka Mwanakwetu ndiye mwajiri.

“Utaratibu tuliyojiwekea kwa kuwa Halmashauri ya Lushoto inamiliki Karakana ya UfundiSelemala basi fundi ambaye mtumishi wa Halmashauri hii jukumu lake akifa Mkristo ni kuchoga jeneza maridadi na akifa Muisilamu unachongwa ubao vizuri na kama maiti ya mbali kama Zanzibar na maeneo mengine kwa Waisilamu linatengenezewa jeneza la kusafirishia mwili maana kila kitu kilikuwepo kwa gharama ya Serikali, ile pesa ya mazishi 500,000/- familia inapewa kama ilivyo na kwa walimu vyama vyao; CHAKAMWAKA na Wakongwe CWT wanaweka nguvu na misiba ya walimu katika Halmashauri haikuwa ya aibu na kizuri zaidi wakati huo Wilaya ya Lushoto ilipata Katibu wa Tume ya Walimu Mwalimu Hemba aliyejituma sana na Katibu wa CWT (W) hawa jamaa walikuwa ni watu waliojali utu kwa wanaowaongoza-MUNGU AWABARIKI sana”

Kwa Mwanakwetu hafahamu walipo hawa viongozi kwa sasa. Maiti ya mwalimu wetu aliyejinyoga ikapelekwa hospitali ya Wilaya ikadungwa dawa huku hospitalini wakiongea,

“Jamani hii maiti fanyeni upuuzi wote lakini huyu aliyekufa ni mtumishi wa Makwega, ole wenu maiti iharibike, mtumjua kama anatokea Mbagala au wapi.”

Gari nyingine likatumwa kuchukua vifaa vya mwalimu aliyejinyonga vikapelekwa karakana vikisimamiw ana na mtumishi wa halmashauri hii Stephern Shemdoe na mdogo wa marehemu, huku kusubiri magari kuambatana kwenda kuzika kwao Mazinde Mombo. Hawa watumishi wa Hospitali ya Wilaya kulikuwa na kijana anayeitwa Maganga yeye alikuwa mfamasia na mzaliwa wa Mbagala Sabasaba anamfahamu Mwanakwetu kama kaka yake miaka mingi. 

 

Yeye ndiye aliyeyasema maneno hayo wakiwa kazini ambapo waliokuwepo wakamsimulia Mwanakwetu baadaye.Msomaji wangu nakwambia ukweli katika mambo ya watu ya umma huwa sina utani. Msiba huu ulikuwa na na kelele nyingi kwa namna alivyofariki na hata tulipofika Mazinde hali ilikuwa tete.

“Huyu binti mwalimu alikuwa Mkatoliki mzuri, Parokia yake Ngwelo walishangaa kilichotokea na walituma maelezo yao kwa familia na kwa Parokia anapozikwa, hata maiti ilipofika Mazinde Paroko wa eneo hili alikuwepo.

Huyu binti kwa mama alizaliwa mwenyewe lakini kwa baba yake alikuwa na kaka yake mmoja ambaye alikuwa anaishi naye mdogo akisema Shule ya Msingi Ngwelo huko huko Ngwelo ambaye kaka yake ndiye alikuwa jirani na dada yake hadi anafariki, japokuwa alikuwa mdogo. Kwa bahati mbaya mwalimu huyu wazazi wake wote walishafariki dunia.

Tukiwa na maiti tayari kulifayika vikao virefu, vurugu mwisho wa siku  tulikubaliana yote isipokuwa tu hoja ya huyu kijana wa kiume ambaye alikuwa akikaa na mwalimu wangu ataenda kukaa wapi?. Kikubwa inavyoonekana koo za baba na mama wa huyu mwalimu zilikuwa ni koo jirani katika maisha ya zamani na mapenzi ya utotoni ndipo akazaliwa huyu mwalimu wangu.

Baba wa huyu mwalimu Mpare na mama wa huyu mwalimu ni Wanyaruanda ambao asili walifka Tanga kulima Mkonge wakati wa mkoloni.Huu ukoo wa mama mwalimu wangu ulikuwa ukoo wa Kikatoliki na ulikuwa na mtawa wakike(Sista) alihudumu Kurasini Dar es Salaam kpindi hiki Askofu wa Jimbo Katoliki a Tanga ni Antony Banzi, lakini lakini akini utawa  wa sista huyu , utawa sista huyu haikuwa grisi ya kuulanisha mgogoro bali michango yake kikaoni iliongeza  kutu katika chuma chakavu siku hiyo .”

Kikao kikaomba kisubiri ndugu mmoja afike ilikuyamalizia maamuzi.


 

Kumbuka msomaji wangu Mwanakwetu hapo ndiye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Lushoto- Nikasema ngoja nikawasalimu watu ninaowafahamu hapo Mazinde Mombo Tanga.

Kwa namna nilivyokuwa napenda kuvaa Suti ya samawati ya giza, shati jeupe na viatu vyeusi siku zote, sikutaka watu wanitambue kwa haraka maana wananiona katika runinga vipindi ya miradi ya maendeleo vijijini, sikutaka jamii ya Mazinde inijue. Nikaingia ndani ya gari nikavua koti, nikabaki na shati jeupe nikalikunja mikono, nikavaa na miwani ya giza nikavaa na yepo yepo , nikamuaga dereva bwana mimi ninazunguka zunguka na kikao ni saa saba mchana , dereva akasema twende na gari mkuu, nikamjibu hapana nataka ninyooshe miguu-Hapa nilifanya hivyo kuzuia dereva huyu wa serikali kutambua kuwa kama mimi ni mwenyeji hapa Mazinde-Mombo, nikatoka nikaenda kwanza kwa ile nyumba ambayo tulilala wakati wa msiba wa dada wa Mzee Jali.

Hapa nikaribishwa na mke wa mwenye mji huku akihudumia kuku, kanga na bata  wake wengi-Ahhh Baba mkwe umekuja? Habari za Lushoto-nikamjibu ni nzuri, Mzee yupo wapi mama? Mama akajibu ametoka ? Lakini kwema? Nikamjibu ni kwema, nimekuja kuzika hapa kuna mwalimu amefariki.


 

Hapo sikukaa sana nikaaga na kwenda kwa familia ya pili ambapo ni ile nyumba iliyokuwa na msiba Mazinde ambapo wakati wa kurudii nilidoea kupanda gari la Mchungaji Mwinuka.

Hapa nikamkuta shemeji yake Mzee Jali, huyu mzee mfupi sana alikuwa ananipenda kwa kuwa sauti yangu alikuwa anaisikiliza RTD awali. Hapa nikamueleza nipo msibani na aliyefariki ni mwalimu wangu nipo kuzika, nimekuja kukusalimu akaniuliza mgogoro msibani umeisha ? Nikamjibu kuwa saa saba nitakuwep hapo kuumalizia, kunandugu yao anatokea Dar es Salaam.

Kwa faida ya msomaji wangu nakuomba mfahamu huyu mzee, yeye aliwahi kuwa miongoni mwa mameneja wa mashamba ya chai na baadaye meneja wa mashamba ya mikonge na alifanya kazi kwanza mashamba ya chai Bumbuli alafu mashamba ya Mkonge, kwao ni Tamota Korogwe. Mzee huyu akasema maneno haya;

“Mkurugenzi wewe ni mwanet na umeoa binti yetu -Haya mashamba ya chai a mkonge yalileta makabila ya kila aina katika maeneo ya Tanga, Kilimanjaro na hata Morogoro na haya makabila yalikuja na mambo yao mazuri na mabaya- hapa unapoona wapo Wamakonde, wapo Wangoni, wapo Wahehe, wapo Wabenna, Wapo Waha, Wapo wa Malawi wapo Warundi na wapo Wanyaruanda wengi tu, hawa wageni ukiwajumlisha idadi yao wanaweza hata kutuzidi Wasamba , Wapare na hata Wambugu ambao ndiyo wenyeji.

Shida mojawapo ya Warundi na Wanyaruanda wanajua kujenga urafiki na wenye nafasi hata wakanti mkonge hawa walikuwa jirani na wazungu mno na kitu cha pili huwa hawana msamaha hata kama Ukristo unawafundisha hilo , wenzetu hawana msamaha na hawarudi nyuma.

Migogoro yao haishi tangu enzi hilo tunalitambua hilo. Warundi na Wanyaruanda wengi baada ya eneo lao kuwa taifa wapo waliyorudi na wapo waliobaki na kuzaliana nasi unaweza kudhani ni Wapare na Wasambaa lakini wenyeji hizo koo tunazitambua kwa kuwaona na majina ya koo zao-Koo za Kisambaa zote zina muundo wa majina yake She-Mbilu, She-Lutete, SheDaffa,Magogo,She-Kilindi,She-Kifu na kadhalika na koo hizi zina simulizi tele, wale wahamiaji koo zao hazina simulizi za asili simulizi zao zipo tu baada ya uhuru lakini siyo za asili .”

Mwanakwetu alikuwa ugali kwa Shemeji wa Mzee Jali kisha kurud msibani kumalizia kikao na ili kushiriki maziko.


 

 

Njiani Mwanakwetu kumbuka anatembea kwa miguu gafla akakutana na Margereth Maufi(Mtinda) huyu ni dada wa Mwanakwetu mzaliwa wa Mbagala ambaye alikuwa miongni warembo wa Mbagala enzi hizo na mwanafunzi wa Zanaki sekondari na mwaka huo ailkuwa Mwalimu Halmashauri ya Korogwe Vijijini, kumsalimu na yeye akienda  kuzika,Mwanakwetu kisha kuingia kikaoni.

Hapo kikaoni yalizungumzwa mengi kikubwa binti huyu alizikwa na ibada ikiongozwa na mtu wa kawaida huku yule kijana mdogo wake aliyekuwa anakaa naye tulirudi naye Lushoto baadaye walipatikana nduguze na kumpatia uhamisho akaenda kumalizia masomo yake huko huko nadhani Tanga Mjini.

Nyuma ya pazia huyu kijana wakati tunarudi Lushoto alituambia kuwa

“Dada yake alikuwa na changamoto moja mshahara wake wote kila akipokea ulichukuliwa na mama zake wadogo kisa wamemsomesha na jambo hilo lilimkera mno.”

Mwanakwetu alifika Lushoto Mjini na kuendelea na majukumu 

 Mwanakwetu anasema nini siku ya leo?

Makala haya yanashabaha tele kubwa ni kutoa elimu kwa umma, pili Tanzania inapotazama migogoro ya Rwanda Burudi unaweza kuamini kuwa sisi tupo salama Mwanakwetu nakwambia hilo siyo kweli jamii ni hii hii tunapakana kwa mipaka tabia zile zile na watu ni walewale na ndugu tabia zile zile, shabaha ya tatu ndugu na hata wazazi somesheni watoto wenu vizuri lakini siyo jambo zuri kuwapoka mishahara yao yote ndugu zenu/ watoto wenu wakishapata kazi eti analipa pesa tulizomsomesha hilo hapana.

Mwanakwetu UPO?

Kumbuka

“Usidhani Tanzania Tupo Salama; Msije Kuwapoka Mishahara Yao”

Nakutakia siku njema.

makwadeladius@gmail com

0717649257






 

0/Post a Comment/Comments