VIONGOZI TEKELO WA WASIOJULIKANA

 

 

Adeladius Makwega-MBAGALA

Mwanakwetu siku ya leo mezani kwake ameshika utafiti wa Shahada ya Uzamivu (PHD) ya Dkt Simeon Mesack juu ya Mauwaji ya Wachawi Nchini Tanzania ambapo utafiti huu ulifanywa chini ya usimamizi wa Chuo Kikuu cha Minnesota nchini Marekani, kazi iliyofanywa na Mtanzania mwenzetu.

Kwa hakika msomaji wangu itakuwa jambo zuri kama nitaeleza kwa namna nilivyomfahamu Dkt Mesack.

 

“Kwa hakika Adeladius Makwega ameandika&kutayarisha makala kadhaa juu ya utamaduni wa Mtanzania katika maudhui mbalimbali tangu mwaka 2006, huku akiwasiliana na wasomi wengi wa masuala ya mila na utamaduni mathalani Dkt Fares Ilomo, Profesa Elias na wengine wengi ambao wamefanya kazi za utafiti zakutukuka katika utamaduni wa Mtanzania. Kwa hakika wasomi hawa wengi wao wanamfahamu Mwanakwetu kwa jina namawasiliano ya barua pepe na simu za mezani na mikononi si kwa kukutana nao uso kwa uso, japokuwa kundi dogo la wasomi hao wanamfahamu Mwanakwetu kwa wajihi mathalani Dkt Ilomo. Msomi mpya aliyewasiliana na Mwanakwetu hivi punde ni huyu Dkt Simeon Mesack ambaye alisoma kazi mojawapo ya Mwanakwetu juu ya Wasumbwa na Kamchape Wao na hilo likafanya ampigie simu Mwanakwetu na kuzungumza naye mambo kadhaa na Mwanakwetu kuomba andiko la Dkt Mesack ambalo Mwanakwetu anakuletea sehumu ya visa ndani ya andiko hilo ambalo lilimpatia Simeon Mesack PHD yake mwaka 1993.”

 

Katika andiko hili Mwanakwetu alikutana na kisa hiki ambapo Dkt Simeon Mesack mwenyewe anakisimulia.

 

Mwaka 1982/3 nilikuwa Mwenyekiti wa CCM, (Chama Cha Mapinduzi-CCM) tawi la Kijiji cha, Changanyikeni, kilichopo kilomita mbili kutoka Chuo Kikuu cha Dar-es-Salaam ninakofundisha. Muundo wa kijiji hiki si wa kawaida kwa sababu kadhaa hilo linasadifu hata jina lenyewe. CHANGANYIKENI. Jina Changanyikeni lilitokana na asili ya watu wake kwa mchanganyiko, hasa miongoni mwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, wafanyakazi walioweka makazi hapo na baadhi ya watu waliofika hapo kutafuta fursa kando ya taasisi hii ya elimu. Kunajumuisha mchanganyiko wa asili mbalimbali za kikabila, zaidi ya haya nusu ya wakazi ni watu wenye elimu nzuri, baada ya shule ya msingi na baadhi kuwa na digrii za Chuo Kikuu.

 


Kwa kweli, wengi wanafanya kazi kwenye Chuo Kikuu cha Dar-es-Salaam (kama mimi). Matokeo yake tawi la CCM lilikuwa la kipekee kwa kuwa na wajumbe wote wa Kamati za chama na walikuwa wahitimu wa chuo kikuu. Wakati mmoja, nililazimika katika kikao cha CCM kujadili imani iliyopo kwa baadhi ya watu kwamba kijiji kilikumbwa na uchawi na kushughulikia hilo hitaji mahitaji endelevu ya baadhi ya wakazi kwa mganga, kwa kualikwa kijijini ili kuwatambua ‘kunusa’ wachawi.

Uharaka wa hali ilikuwa kwamba mtaalam mmoja, Bwana Tekelo, alikuwa tayari anaifanya kazi hii katika kijiji cha jirani na kwa hiyo ilitolewa hoja kwamba hatupaswi kukosa fursa. Kamati yetu iliundwa na wanachama saba na walio wengi wangeamua suala hilo. CCM ilijadili faida na hasara za kumpigia simu mtaalam, na kwa hakika kumlipa kama ishara ya makubaliano yetu. Mwishowe, kura zilipigwa na kuwa maamuzi yalikuwa tusimualike Bwana Tekelo. Uamuzi huu ulimaanisha mambo kadhaa. Kwanza, tuliepuka kugawanya kijiji kwa mistari ya waumini na wasioamini uchawi. Pia ingesababisha kuwinda wachawi na kuuwawa.

Bwana Tekelo alikuwa chanzo cha msuguano kati ya serikali na waganga wa jadi waliokuwa wakipiga kelele kwa utambuzi rasmi wa mazoea yao. Bwana Tekelo hatimaye alizuiliwa kufanya mazoezi na mamlaka za serikali katika Wilaya ya Bagamoyo ilifanya hivyo pia, kwa sababu alionekana kuwa tishio kwa maelewano katika eneo hilo. Hiki kisa cha kufurushwa kwa Bwana Tekelo huko Bagamoyo kiliripotiwa pia na gazeti la Mzalendo Disemba 12, 1992.

 


Mwanakwetu anasema nini siku ya leo?

Kwa hakika msomaji wangu umeona namna tawi la CCM la Kijiji cha Changanyikeni lilivyofanya maamuzi ya busara ya kutomualika Bwana Tekelo kwenda kuwasaka wachawi katika eneo la Changanyikeni kwa kuwa haya mambo yalikuwa ni dhahania tu, hakukuwa na ushahidi wa kisayansi ndani yake, eneo kando ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Katika kisa hiki msomaji wangu kumbuka Dkt Simeon Mesack alikuwa ndiye chairman- Mwenyekiti wa CCM wa Tawi la Changanyikeni mwka 1982/83 wakati huo, hilo Mwanakwetu hana hakika hata leo kama Tawi la CCM Changanyikeni wanayo kumbukumbu hiyo. Wakati kisa hiki kinatokea chama kilikuwa kimeshika hatamu, ajenda katika chama inajadiliwa na chama kinafikia maamuzi ya kutomulika Bwana Tekelo,  viongozi makini wa CCM wasomi walitumia elimu yao vizuri na kukataa kuleta migogoro isiyo ya lazima, migawanyiko isiyo na lazima katika Kijiji cha Changanyikeni wakati huo.



Mwanakwetu anatambua kuwa Chama Cha Mapinduzi CCM kina mahusiano mazuri na viongozi wa dini na hata Waganga wa jadi, pamoja na machifu. Je viongozi wa CCM na Serikali leo hii wanajifunza nini katika kisa hiki? Akina Simeon Mesack na wenzake walikuwa watu wa Karatasi ya Litimasi yaani Nyekundu Buluu na Buluu Nyekundu. Kwa sasa Tanzania ina changamoto mbili za mauwaji wa Kishirikina na Watu Wasiojulikana huku haya yote yakifanyika wakati mmoja.Huku vifo na miili ikiokotwa maeneo kadhaa.Hoja ya mauwaji ya kishirikina na Wasiojulikana yana ushahidi wa kutokea, hivyo kuwasaka wanaofanya haya lazima kufanyika na kutowasaka wnaofanya hivyo kuna athari kubwa kwa taifa la tanzania.Tanzania lazima imsake Bwana?bibi Tekelo aje kutoa majibu ya haya yote na wahusika wachukuliwe hatua mara moja.Swa li ni ni Je huyo Bwana& Bibi Tekelo ni nani?Kwa hakika CCM na viongozi wa Serikali hivi sasa ndiyo Bwana &Bibi Tekelo Wasiojulikana.

Mwanakwetu anaamini kuwa wasiojulikana Tekelo wao ni Viongozi wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama na kutowakamata na jamii kushugulikiwa itakuwa ni kuleta migawanyiko katika jamii.Viongozi Watimize wajibu wao katika hili na si vinginevyo. Wawe makini , hawapaswi kuwa mabubu katika hili lazima wahusika wa matukio ya ajabu ajabu wajulikane na wachukuliwe hatua .




Mwanakwetu Upo?

Kumbuka-

Viongozi Ndiyo Tekelo Wasiojulikana.

Nasema-Ahlan wa Sahlan.

 

makwadeladius@gmail.com

0717649257






0/Post a Comment/Comments