Adeladius Makwega-MBAGALA
Mwanakwetu nilikuwa nasali katika Parokia moja ya Kanisa Katoliki hapa hapa Tanzania, kama ujuavyo huwa naandika na kutayarisha ripoti na makala kadhaa zenye maudhui ya Kanisani kila dominika. Katika Parokia hii niliyokuwa nasali, vifaa vya mawasiliano kanisani havikuwa madhubuti, sauti ya Padri ilikuwa hasikiki vizuri kama ingerekodiwa kanisani, kwa hiyo kama narekodi nikiwa kanisani kwa kutumia mashine yangu ya MALANZI sauti ilikuwa hafifu mno, hivyo nikawa na utaratibu kila wimbo kabla ya Injili ukianza sina budi kutoka nje ya kanisa kwenda kuweka mashine yangu katika Spika moja ya nje ya kanisa ili, ili kuyarekodi mahubiri vizuri. Siku moja nikiwa narekodi mahubiri haya ya Padri katika misa hii, mara akaja kijana mmoja kachelewa na, na huku akihema sana nadhani alikuwa mgeni wa eneo hilo, hapa misa imeanza saa 12.00 asubuhi na yeye kafika nadhani 12 .59 akafika akanisalimu, kwa kuwa narekodi nikamsogeza kando ili MALANZI isirekodi haya mazungumzo yetu na yasiharibu rekodi ya mahubiri ya padri , kijana akawa ananiuliza maswali mengi, misa inaanza saa ngapi?
Zipo Misa ngapi? Je misa hii amechelewa? Nikawa najibu, kijana akasema kwa kwa kuwa amechelewa na Padri anamalizia mahubiri ngoja angoje misa ya pili ambayo nilimwambia inaanza saa mbili za asuhuhi. Nikaagana naye mie nikarudi kando ya spika huku narekodi mahubiri maana mashine yangu ya MALANZI ni zaidi shilingi Milioni 2 na laki tano za Kitanzania sasa sina pesa ya kuinunua mpya hivyo nakuwa nayo jirani kama ulinzi isipotee. Padri akahubiri, akamaliza na mimi kurudi kanisa kusali hadi Ibada hii ya sisa inamalizika, misa ilipoisha nikawa natoka narudi kwangu, huyu kijana akawa anaingia kanisani misa ya pili kama aivyonuia pale awali. Moyoni nikasema huyu kijana kweli ni Mkristo.Nikawa namtafakari njiani hadi nikafika kwangu.
Baada ya majuma kadhaa kila jumapili kijana huyu nikawa namuona kanisa maana akawa anawahi nadhani alishatambua ratiba za misa nilizomwambia. Huyu kijana nadhani na yeye akawa ananitambua kwa sura hasa kule kurekodi mahubiri na nilivyo mpokea kwa mara ya kwanza, maisha yakawa yanaendelea.
Siku moja nilikuwa nasafiri , nikasema ngoja nitatoe pesa nikaenda kutoa pesa kwa wakala hapo stend , hapo nikakutana naye , akanisamu nikaitikia, hapo hapo akaninunulia soda, akiniuliza mzee habari? Nikamjibu salama akaniuliza wewe ni mwandishi? Nikamjibu ehee mimi ni mwandishi, ni mtangazaji na mtayarishaji vipindi. Kijana akauliza tofauti ya haya mambo matatu ya mwandishi , mtangazaji na mtayarishaji vipindi ni nini?Nikawa namjibu ,kumbuka Mwanakwetu ni na tena mwalmu bora ;
“Mwandishi unaweza ukawa unaandika katika gazeti, mitandao, hata redio na , runinga ;kwenye redio na runinga, wewe umeandika anasoma mwingine. Mtangazaji unaweza kukitangaza alichoandika mwenzako au kama unao uwezo wa kuandika na kukitangaza unafanya- nikamwambia mimi naweza kukisoma alichoandika mwezangu na hata nilichoandika mwenyewe na kikatangazwa vizuri tu nikamalizia na mtayarishaji vipindi viwe vya runinga au redio huyu anatarisha kila kitu ili kukamilisha kipindi alafu mtu mwingine anakuja kuyatangaza kwa kuyasoma neno kwa neno lakini yeye mwenyewe kama anao uwezo anatayarisha na kuyasoma na kuw tayari kutangaziiwe kwenye redio, mitandaoni na hata katika runinga .Kijana nikamwambia mimi ninafanya yote.”
Kijana akasema kumbe wewe ni hodari ,Mwanakwetu nikacheka , alafu akaniuliza upo serikalini? Nikamjibu ndiyo, akaniuliza swali lingine unanikumbuka nikasema ndiyo wewe tunasali wote, kijana akatoa ishara ya dole gumba. Nakuomba msomaji wangu nikwambie kitu;
“Unapoongea na mtu anayekupenda kwa moyoni unaweza kuona na hata kuhisi pale unapoongea naye mtu huyo na hata kama unaongea na mtu hatari Mungu amempa mwanadamu uwezo wa kuhis hilo, macho ya mwanadamu hayawezi kumficha mtu mwenye hila.”
Kwa wale ambao hawafahamu hili nitumie lugha nyepesi waswahili wanasema MACHALE ambapo kuna hisia juu ya jambo fulani mathalani unapita msituni, nywele au mwii unaweza kusisimka alafu ukakutana na mnyama mkali, haya ndiyo machale kwa kimombo hii habari nadhani inaitwa Intuition. Huyu kijana hakuwa kijana mbaya, alikuwa kijana mwema na kijana mzuri anayeheshimu dini yake lakini mijitu mibaya inaweza kumshawishi kufanya mabaya, kijana kama huyu lazima kumlinda kwa gharama yoyote ili abaki katika mikono salama. Jukumu hilo linatakiwa kusimamiwa na wakubwa kazini, dini yake na hata watu wanamzunguka na tunatakiwa kuomba Mungu asikutane na mijitu, miharamia,mifirauni au hii mijitu isiyojulikana. Kwa hiyo wazazi tunatakiwa kuwa makini watoto wetu tunaowasomesha lakini wanakwenda kutumia elimu yao na watu wa namna gani? Wazazi wezangu tuwe makini. Siku hiyo nikapanda basi kuelekea ninaposafiri.
Maisha yanasonga, siku moja ikawa umefika msimu wa kulipia karo za wanangu shule zmefunguliwa vijana wanaokwenda shule kila mmoja baba ada baba ada baba karo, kwa hiyo nikatoka kwangu hadi kwa wakala, nikafika pale kwanza nikatoa kadi yangu nikatoa pesa, wakala akataka kunipa pesa zangu , nikamwamb a hapana pesa hizo nalipa karo kaa nazo kwanza nalipa ada za wanangu, nikaaza kuandika wee makaratasi mengi mara nimekosea akaunti, mara napiga simu kibao, wakala ananicheka akisema
“Duu Baba una watoto wengi, hiyo pesa unayolipa mtaji wangu wa biashara hapa nilipo .”
Wakati najibu haya maswali ya huyu wakala, mtu kando ambaye na yeye alikuwa mteja akaniangalia usoni nakunisalimia mzee Shikamoo!, Nikamjibu marahaba, msomaji wangu kumbe ni yule kijana niliyekutana nae maeneo kadhaa Mkatoliki mwezangu. Kijana huyu akasema,
“Afadhali uiangaikie pesa alafu uwe uwe na watoto wa kuwalipia karo, wengine wana pesa lakini hawana hata watoto wa sumuni,watoto wa dawa wa kuwalipia karo.”
Nikawa nawaitikia lakini mawazo yangu yalikuwa katika kuandika vizuri hizi ankara kifani za benki ambazo nakala naenda kuwapa wanangu. Nilipomaliza hii kazi nikatoka narudi kwangu kumbe mbele yupo huyu kijana tukawa tunaongea maana kulikuwa na msafara wa viongozi, hapa nikamuuliza huyu kijana na wewe kazi yake unafanya wapi ?Akasema yeye yupo katika mradi mmoja mkubwa sana ambao ni mali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lakin yeye ameajiliwa na hii kampuni ya kigeni ambayo ni mkandarasi, nikamuuliza mnaendeleaje na kazi? Akasema kazi yao ni nzuri haina shida na wanapata pesa nzuri, huyu kijana ni msomi mzuri, nikawa namuuliza changamoto kazini na changamoto kutoka serikalini na viongozi wetu? Kijana akacheka.
“Labda changamoto kwa miradi mingi mikubwa ni kwa maeneo ambapo miradi hii inafanyika mzee hakuna uelewa wa viongozi wa maeneo husika katika kufuatilia miradi hii na kuzitambua fursa wakati miradi inaendelea.”
Kijana huyu anaongea vizuri sana hapa Mwanakwetu nikafurahi mno, kijana akasema.
“Serikali imeweka mradi mkubwa, ukitazama kitabu cha wageni hajawahi kufika Diwani wala Mbunge- ukifuatiliwa utaona tu Katibu Mkuu, Waziri, Naibu Katibu Mkuu, Katibu Mkuu, Waziri, Katibu Mkuu Waziri sana Mkuu wa Mkoa na Mkuu wa Wilaya kidogo Mkandarasi Mshauri . Mathalani mradi wa bilioni 50 ukipiga mahesbu yote hapa jamii yenye viongozi wajanja CSR katika mradi wa bilioni 55 inaweza kwenda kwa jamii kando ya mradi hata kufikia hata milioi 500 ukijumulisha na ajila za vibarua wanapata maendeleo ya kulibadilisha eneo.Yaaani kama mbunge mjanja anakuja mwenyewe na mwenyekiti wa Halmashauri wanaomba hata kujengewa manteki ya maji, shule na hata barabara ipigwe lami. Haya makampuni ya wageni yanakaa kimya lazima yapigiwe kelele kama hakuna kelele ni kosa.”
Kijana anaogea Mwanakwetu kimoyomoyo akawa anasema je viongozi wetu wanaochaguliwa wanayatambua haya ni sehemu ya majukumu yao? Au wanatumia nafasi wanapopata kukamilisha mambo yao?
Je watu wanaochaguliwa wanayo mikakati yoyote ile ya namna ya kufanya mambo kama haya? Kijana akasema kama wanayo mikakati ni ya kushinda uchaguzi tu lakini siyokufanikisha mambo kama haya, haya ni mambo yanayohitaji muda, mipango na akili.
“Kaka Afrika mradi mkubwa unakamilika eneo linashindwa hata kuwekewa lami ya utambulisho wa kijiji hata ya KM 3. Kaka waambieni ndugu zetu changamkie hizi fursa na hata sisi kwenye taasisi hizi tupo ni Watanzania wenzenu, changueni watu wenye mpango na siyo kuchagua mtu wa kuja kukalia kiti tu.”
Mwanakwetu alipomaliza mazungumzo haya kumbuka siku hii kulikuwa na msafara wa viongozi mrefu sana na mvua kubwa inanesha na msafara ulipoisha na mvua kukata alivuka barabara kuelekea kwake.
Mwanakwetu anasema nini siku ya leo?
Jamani kikubwa chagueni watu wenye mipango, nia na moyo thabiti wa kusaidia wananchi maana wengine wakiongozwa wanakuwa wazuri zaidi.
Mwanakwetu Upo?
Kumbuka-Wengine Wazuri Wakiongozwa
Inawezekana Timiza Wajibu
0717649257
Post a Comment