Adeladius Makwega-MSAMVU-MOROGORO
Kwa hakika mara baada ya kifo cha Dkt Faustine Ndungulile, Mwanakwetu amepigiwa simu na jamaa zake kadhaa ambao waliwahi kugombea kura za maoni na Dkt Ndungulile tangu mwaka ule wa 2010.
Miongoni mwa matukio ya kuvutia ya mwaka 2010 ni vituko vya watia nia wa CCM ndani ya Coasta ya Wagombea hao na mojawapo ya tukio ni wagombea wote wasiopungua ishirini na mbili walizunguka eneo la Kisarawe A na B na baadaye kufanya mkutano mwisho wa jioni katika eneo la Toa Ngoma ambapo wagombea hao walipigana fitna kweli kweli chupu washikane mashati.
“Mwanakwetu na Thadeus Musembi walipigwa fitna kuwa wao walikuwa wagombea geresha na ndiyo maana hawatoi rushwa na wanatokea vyombo vya ulinzi na usalama, hivyo wanaccm wasiwape kura. Haya yalisemwa ndani ya basi na wagombea wengine na hivyo hata maswali wakati kujinadi yaliulizwa baada ya kupenyezwa na wagombea wenzao.
Mwanakwetu aliulizwa swali hilo mara nyingi na yeye alijibu kuwa ni mgombea wa kweli na nia yake ni kuwasaidia wapiga kura kama wakimpa nafasi ya kuiwakilisha CCM, aliongeza kuwa hana pesa za kuwahongo.
Makwega alinadi kwa yeye anafanya kazi TBC kama Mtanyashajiji Vipindi na siyo askari na hajawahi kuomba wala kuitamani kazi hiyo, japokuwa angekuwa askari angekuwa askari mzuri wa miguu maana miguu yake nyayo zake zipo vizuri haziko kama unyayo wa Tembo na anao uwezo mkubwa wa kutembea kwa miguu umbali mrefu.
Wajumbe na wanachama wa CCM wakawa wanacheka, baadhi ya wagombea walikuwa na watu wao wakawa wanarekodi namna baadhi ya wagombea wanavyojinadi na hiyo ikawa inatumika kujibu hoja za kuwaponda wenzao.
Joto la mashambulizi sijui kwanini yalilenga kwa vijana wawili tu Kazimbaya na Thadeus ambao walikuwa bado vijana mno. Tambo za kutupiana maneno zikahamia ndani ya basi la wagombea.
Nyie si mnasema mie askari mbona, Dkt Faustine Ndugulile Baba yake aliona mambo magumu, akaenda kwa Jakaya kulialia, Jakaya akamuonea huruma, akamuuliza yule mwanao Daktari yupo wapi? Baba yake Dkt akajibu mwanangu yupo Afrika ya Kusini, Jakaya akasema haya haya mwambie arudi mara moja akagombee Ubunge Jimbo la Kigamboni.
Shabashi mpo hapa kwa hisani ya Jakaya tu! Je Jimbo la Kigamboni limekuwa Bara la Afrika wakati wa Berlini Conference? Watu wakawa wanacheka ndani ya basi. Baadhi ya watu wakawa wakali hasa wagombea wenye asili ya Mkoa wa Mara ambao walikuwa wengi akiwamo mh John Makombe Kibaso, akauliza Wewe Kazimbaya unasema nini ? Mwanakwetu akajibu -Jimbo la Kigamboni limekuwa Bara la Afrika wakati wa Mkutano wa Berlini?
John Makombe Kibaso akasema Makwega kwanini mnatunyima raha katika hizi kampeni? Mwanakwetu akamwambia John Makombe Kibaso aaaha na wewe umesahau nini huko Bungeni hadi urudi tena maana ulibahatisha wakati wa Mrema aliyokwenda TLP?
Kibaso unataka ukajisifie kwenu huko Mara ahaa mimi ni Mbunge wa Dar es Salaam. Ubunge wa Ngekewa Temeke haikutosha sasa unaitaka Kigamboni? Nenda kagombea mkoa wa Mara.
Tambo zinaendelea na hili la John Kibaso likaleta maneno makubwa ambapo kukatokea fujo ndani ya basi hilo ili Mwanakwetu apigwe. Kumbuka John Makombe Kibaso ana mwili mkubwa naye Mwanakwetu mwembamba, watu wamesimama wanasema ndani ya basi.
Mwinchumu Abdul Rahaman Msomi na Brigedia Mstaafu Haruni Othuman wakaingilia kati wakasema Makwega hapigwi, mbona nyinyi mnampiga maneno yeye anacheka tu, kuweni wavumilivuu na hizo ndiyo siasa. Ugomvi uliisha salama.
Safari iliendelea na kila mgombea akawa anashuka kituo chake huku magari ya familia zao yakiwachukua vituoni. Mwanakwetu alipofika Kituo cha Mbagala Sabasaba alikuwa ndiye mgombea wa mwisho kushuka na kuwaacha vijana wa CCM Taifa waliokuwa wanasimamia zoezi hilo na Dereva wa basi hili.”
Kwa hakika msomaji wangu hiki kisa kinakumbukwa na Mwanakwetu siku ya leo huku sasa Jimbo la Kigamboni lipo wazi na swali la kujiuliza je nani atakuwa mbunge Kigamboni? Au yale yale ya KIgamboni kama Bara Afrika Wakati wa Mkutano wa Berlini yanarudi tena?
Kulijibu swali hili inaonekana kuna kila dalili kuwa Dkt Faustine Ndungulile hakuwa na nia ya kugombea tena Ubunge wa Kigamboni mwaka 2025 na ndiyo maana akarudi katika mambo ya taaluma yake huko WHO. Hili linaaminiwa na Mwanakwetu na hata nduguye Thadeus Musembi ambao wanazifahamu mno siasa za Temeke, siasa za Mbagala , Siasa Kigamboni na Dar es Salaam.
Wapo wanaoamini kuwa ndugu Paul Makonda anaweza kugombea ubunge Kigamboni hili Mwanakwetu anasema siyo sahihi maana kuna dalili nyingi za wafanyabiashara wakubwa kugombea ubunge wa Jimbo la Kigamboni ambapo kwa hakika ndiyo waliyoweza kupanga matokeo ya kura za maoni CCM Jimbo la Kigamboni mwaka 2020 na pengine walishajipanga mapema kushika kiti hichi.
Nyuma ya pazia kukiwa na dhana kuwa Rais John Magufuli alidumaza Mji wa Kigamboni, hivi sasa ilitakiwa liwe limebadilika kabisa.Swali la kujiuliuza Je Rais John Magufuli alikuwa anafahamu kpi juu ya Kigamboni?
Swali lengine la Mwanakwetu ni je CCM inaweza kuzuia wapiga lura masikini kufanya maamuzi mengine kama wakitambua wanachokita? Je wapiga kura masikini wanaweza kufanya vinginevyo iwe ndani ya CCM au kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA ili kuongoza jimbo hilo? Haya ni naswali lakini majibu lake yatapatikana muda si mrefu.
Ndugu Musembi anaamini kuwa Dkt Ndungulile alionesha uhodari wake kwa kukaa bungeni miaka 14 alafu kurudi katika taaluma yake ambapo wengi wa wabunge ndani ya vipindi viwili wakishatoka bungeni huwa ni vigumu kurudi katika taaluma zao.
Mwanakwetu anatumia makala kuwakumbusha wasomaji wake kuwa eneo la Temeke ambalo awali Kigamboni ilikuwa ndani lilikuwa na Mbunge anayefahamika kama Ali Mchumo ambaye aliongoza jimbo hilo kwa vipindi viwili 1975-1980 na 1980- 1985 akishika vyeo kadhaa kama naibu Waziri wa Mambo ya Ndani na Baadaye Balozi wa Kudumu wa Tanzania Umoja wa Mataifa, huyu akiwa ni Mndengereko mwenye akili.
Kwa Mwanakwetu anatambua wapo wana Temeke kadhaa waliofanya vizuri bungeni na baadaye kutumika kimataifa kama Balozi Ali Mchumo. Kweli Wandengereko watani wangu sasa hivi mnaturudisha kupiga kura na vivuli? Hawa ni Wandengereko wa sasa siyo akina Balozi Ali Mchumo.
Mwanakwetu anasema nini siku ya leo?
Mwanakwetu anakumbuka namna wajumbe wa CCM walivyokuwa wakikimbilia maboresho ya Dkt Faustine Ndungulile wakati wa kura za maoni mwaka 2010, Mwanakwetu anawaomba na kuwakumbushawale waliofanya hivyo wakumbuke kutubu mapema kabisa na hali hii isijirudie tena Jimboni Kigamboni.
Kigamboni, Mbagala na Temeke ni maeneo kwa asili ni ya watu masikini, ambapo kuwahonga ni jambo jepesi sana na kwa mwanasiasa mwenye fedha anaweza kushinda kwa urahisi mno. Wakati wa kampeni watu masikini wanadhana kuwa tajiri anaweza kutumia fedha zake kuwasaidia katika maendeleo ambalo hilo siyo sahihi.Hivyo ndivyo ilivyokuwa inahisiwa hata enzi za marehemu Abasi Ngulamali Mbunge wa Kilombero.
Kwa jimbo la Kigamboni matajiri wapige hesabu zao vizuri alafu wataona, kikubwa kuna usalama mkubwa sana kwa mfanyabiashara akiwa siyo mbunge kuliko akiwa mbunge. Hata kama matajiri na wafanyabiashara wakigombea Jimbo la Kigamboni wapiga kura baadaye watakuwa na nafasi ya kuchambua pumba na mchele kwa uzoefu wa majimbo yaliyowahi kuongozwa na wafanyabiashara je yatakuwa na tofauti na majimbo yanayoongozwa na watu wa kawaida?
Shabaha ya tatu ya makala haya ni kuyakumbuka maisha ya siasa ya Dkt Faustine ndungulile yalivyokuwa wakati huo na wale waliyokuwa jirani yake tangu mwaka 2010- 2024.
Shabaha ya nne ya makala haya , Mwanakwetu anakukumbusha msomaji waku juu ya Balozi Ali Mchumo ambaye ni Mndengereko mwenye akili ambaye alikuwa hawahongi wajumbe wa TANU/CCM na alikuwa anashinda kwa haki jimbo la Temeke wakati huo hadi alipomuachia Ali Masoud Bedui mwaka 1985 na kuwa mbunge mpya wa Jimbo la Temeke.
Shabaha ya tano ya makala haya nakuomba utambue kuwa pale ndani ya Basi la wagombea wa kura za maoni CCM mwaka 2010, John Makombe Kibaso na Dkt Faustine Ndungulile walipokasilika wakataka kumtwanga twanga Mwanakwetu, watu wawili walimtetea Mwanakwetu nao ni mhe Mwichumu Abdul Rahaman Msomi awali alikuwa mtumishi kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais na mtu wapi aliyemlinda Mwanakwetu siku hiyo alikuwa Brigedia Mstaafu Haruni Othumani ambaye awali alikuwa Mwambata wa Kijeshi wa Tanzania nchini Misri, Mwanakwetu alipewa ulinzi siku hiyo na ndugu hao.
Mwanakwetu upo?
Kumbuka,
“KIGAMBONI KAMA BARA LA AFRIKA WAKATI MKUTANO BERLINI.”
Nakutakia siku Njema.
0717649257
Post a Comment