Adeladius Makwega-MWANZA
Ni majira ya jioni ya Novemba 10, 2024 Mwanakwetu anasikia sauti za shangwe katika viwanja vya Ndani Vya Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya (MCSD)Kwimba hapa Mwanza na anajongea katika ukumbi huo mkubwa wa kisasa.
Alipoingia na kuuliza mbona kuna shangwe kubwa? Aliumwa sikio kuwa Wanachuo wa Chuo cha MCSD wamehitimsha mashindano ya ligi ya mpira wa kikapu yaliyoanza Novemba 2, 2024.
Katika viunga hivyo huku zawadi zao kadhaaa chini ya udhamini wa Mtweve Kayanda zikiwa hadharani , ndugu Kayanda ambaye ni miongoni mwa wakufunzi wa taasisi hii ya Umma akasema,
“Jamani tunaomba utulivu, mgeni rasmi amefika awagawie zawadi zenu.Chuo chetu kinatoa mafunzo ya michezo kadhaa ikiwamo mafunzo ya Mpira Kikapu natambua mmetumia vizuri siku kumi za mashindano haya, huku mkishiriki mafunzo ya nadhalia na vitendo kwa masomo yangu na masomo ya wakufunzi wengine, nawapeni hongera kubwa, nimeamua kutoa zawadi kwa kuwa mmeonesha moyo wa kimichezo wa kutokata tamaa, leo wameshinda wenzako na kesho utashinda wewe msikate tamaa.”
Akizungumza katika kukabidhi zawadi hizo Makamu Mkuu wa Chuo cha hiki anayeshuhgulikiwa Utawala Mkufunzi Denisi Kayombo amesema kuwa amefurahishwa na mashindano haya na moyo huo unaonesha kweli sasa chuo kimefunguliwa na masomo yamepamba moto.
“Nawapongezeni sana kwa mashindano haya, nilikuwa nafuatilia vizuri na nikiziona jitihada zenu michezoni, hongereni kwa mashindano na hongereni kwa waliopata zawadi.”
Wakipokea zawadi hizo timu ya Wonders ilijinyakulia Mbuzi beberu wa thamani ya shilingi za Kitanzania 170,000/-, timu Miracles ikajibebea sanduki kadhaa za soda na timu ya Frazon ikijinyakulia dazani kadhaa za juisi.
Zawadi zingine zilizotolewa katika mashindano haya ni pesa tasilimu ambapo Jamada Musa alipokea shilingi 10,000 kwa kuwa MVP (Most Valuable Player ) Naye Mbeche Samweli amepokea shilingi 10,000 ya (BR)Best Rebounder naye Ruben Bernad akipokea shilingi 10,000 ya Three Points .
Kandoni mwa tukio hilo wakati wa hutoaji wa zawadi hizo mtayarishaji wa makala haya ameshuhudia baadhi ya wanamichezo waliyoumia mchezo akipokea huduma ya kwanza huku kundi la wenzake likipokea zawadi zao, hiyo inatoa ishara kuwa michezo kila inapofanyika wengine wanaumia na wengine mabingwa wa kulaumu na kushangilia ushindi.Michezo inahitaji mno afya ya mwili kwa kila anayeshiriki michezo hiyo nayo mahitaji ya dawa yanatakiwa kuwa kando.
Mpira wa kikapu ni mchezo unaochezwa na wachezaji wa 5 uwanjani huku wachezaji wa kando karibu 7 wanayo nafasi ya kuchukua nafasi ya mchezaji mwingine muda wowote ule.
Mchezo huu uliannzishwa na mwalimu James Naismith kwenye chuo cha Sprinfield huko Massachusetts mwaka 1891, ukibuniwa na msomi huyu nia yake kwa wanafunzi ili waweze kufanya mazoezi hapo chuoni, Wakati wa msimu wa kipupwe Mungu bahati mwaka 1936 mchezo huu ulikubaliwa kuchezwa katika mashindano ya Olimpiki.
0717649257
Post a Comment