UONGOZI WA MICHEZO BAADA YA UCHAGUZI MKUU

 


Adeladius Makwega-Kwa Omari Kijana MOROGORO

 

Gafla Mwanakwetu akaona kundi na wanachuo kama 80 hivi wanakuja alipo, wakaingia na kukaa katika viti, Mwanakwetu akatambua kuwa wanakipindi akawa anafunga vifaa vyake ili kuwapisha na yeye ahamie eneo lingine ili mkufunzi aweze kufundisha kwa amani.Wakati Mwanakwetu anafunga vifaa vyake gafla akaingia mkufunzi husika akasema,

“Makwega usiondoke, baki hapa hapa kwani sasa hivi unafanya nini?”

Mwanakwetu akajibu kuwa sasa anasanifu makala yake ya sauti, anaihamisha kutoka maandishi kuwa sauti. Jamaa akauliza si unavaa kiongeza sauti masikioni? Mwanakwetu akajibu naaaam. Jamaa akasema Mwanakwetu baki na wewe ujifunze michezo. Mwanakwetu akabaki na hapo hapo, somo likaanza.Mwanakwetu kwa heshima ya mkufunzi huyu akatoa kiongeza sauti masikioni na akawa anafuatilia somo hilo ambalo lilihusu Contemporary Issuies in Sports

Jamaa akataja mambo kadhaa, anayoyakum buka leo hii Mwanakwet ni Adhabu kwa watazamaji/Mashabiki Michezoni, Matumizi ya madawa ya kuongeza nguvu, Matumizi ya Mitandao ya Kijamii Michezoni, Afya na Magonjwa ya akili Michezoni, magonjwa na madhara yake katika michezo na maamuzi kwa kutumia vifaa vya kieletroniki.

 

Mwanakwetu siku hii akawa mwanafunzi wa kualikwa na kwa hakika siku hii akavutia mno na somo hilo na namna jamaa huyu alivyokuwa anafundisha , kushirikisha wanafunzi wake na ndani saa nzima huku wanafunzi wanacheka huku wakijibu maswali vizuri , baada ya saa moja kipindi kikaisha jamaa akashukuru kwa Mwanakwetu kuwa Mwanafunzi wa somo lake siku hiyo japokuwa hakufanya mtihani wa somo hilo.

Mkufunzi huyu  akatoka na wanafunzi wake naye Mwanakwetu kumalizia kazi yake. Alipotoka huyu jamaa Mwanakwetu akakumbuka hili.

“PEDAGOGY/UALIMU ni sanaa, sayansi na namna ya kufundisha jambo fulani hususani katika nyanja mbalimbali za ufundishaji na kujifunza. PEDAGOGY inajumuisha mambo kadhaa ikiwamo mbinu za kufundishia ambayo ni mikakati inayotumiwa na mwalimu/ mkufunzi /mhadhili ili kuwasilisha maudhui kulingana na mtaala. Shughuli yenyewe ya kujifunza hapa ni mambo yanayosaidia mwanafunzi kujifunza kwa wepesi mada husika, unaweza kuita nyenzo.Pia ni jinsi mwalimu  /mkufunzi au mhadhili anavyopima uelewa wa wanafunzi wake bila kupendelea , wala ubaguzi.Ufundishaji unaweza kuwa unaomlenga mwalimu au unamlenga mwanafunzi. Ule unaomlenga mwalimu hapa mwalimu anawatafunia wanafunzi mwanzo mwisho mada hiyo lakini ule unaomlenga mwanafunzi ni kwa kuwaongoza wanafunzi kutoka jambo wanalolielewa kuelekea kule wasikokuelewa hapa wanafunzi wanashugulika pamoja na mwalimu wao kwa pamoja.

 

Msomaji wangu unaweza kujiuliza Mwanakwetu anayasema haya kwa mamlaka gani? Haya anayatoa wapi?Nikupe jibu kuwa Kuwa  Mwanakwetu aliwahi kuwa AFISA ELIMU MSAIDIZI DARAJA TATU na katika kozi ya Stashahada ya Ualimu mwaka 2001-2003 Chuo Cha Ualimu Kasulu miongoni mwa wanafunzi bora wa Mbinu Bora Za Ufundishaji waliotambuliwa mwaka 2003 alikuwepo Annastazia Kapufi na Adeladius Makwega na kutunukiwa cheti cha Uhodari katika PEDAGOGY.

 

Kumbuka Mwanakwetu alikuwa anafanya kazi katika chumba kile kilipofanyika somo hili, 


 

Kumbuka Mwanakwetu aliondoa kiongeza sauti masikioni na kusikiliza somo hilo kwa dakika 60, hapo hapo Mwanakwetu akasema maneno haya,

 

“Huyu mhadhili ana uwezo mzuri na mkubwa wa PEDOGOGY kutoa elimu, hata kuliongoza darasa lake na ndiyo maana katika dakika 60 amefundisha somo lake vizuri kwa kutumia mbinu bora za ufundishaji huku darasa zima wakisafiri pamoja naye kwa amani na furaha huku hata mimi mwanafunzi mwalikwa nimeielewa vizuri mada hii.”

 

Mwanakwetu haya yote akayahifadhi katika shajala yake na kuendelea na maisha yake. Kuna wakati watu wanalikuwa wanahangaika kutafuta fagio, majembe , makwanja ya taasisi na kwa suluhu ilikuwa ni kwenda taasisi jirani kuazima kila mara usafi ulipohitajika kufanywa kama vile makanisani, gerezani na vyuo jirani.Hapo ikaulizwa jamani kweli watu wazima tunafunga safari kuazima fagio, kuazima majembe?Je huku tunapokwenda kuazima wamepataje na wewe ushindwe?Jamaa mmoja akasema ngoja mimi nitakwenda kuuliza na nitawapa mrejesho Jamaa akaenda na aliporudi akasema,

 

“Familia hata iwe masikini vipi lazima utakuta nyumba inalo fagio, hauwezi kusema sina fagio, sina jembe, sina panga, sina kwanja kisa sina pesa. Wenzetu vifaa hivyo vinaingizwa katika fomu ya kujiunga na kila mwanafunzi anakuja na kifaa hicho ili aweze kukitumia akiwa katika taasisi husika na hivyo ndivyo wanavyofanya wenzetu  huko tunapoenda kuazima na sisi tuige mfano huo. Kikubwa vifaa hivyo vitunzwe, shida unaweza kumkabidhi mtu kutunza vifaa hivyo lakini yeye haoni umuhimu wa vifaa hivyo .”

 

Msomaji wangu vifaa hivyo kweli viliagizwa na taasisi hii kupata vifaa tele na umasikini wa fagio ulikwisha mara moja na kuomba omba kukafilia mbali. 


 

 

Natambua msomaji wangu unalo swali huyu jamaa ni nani?

 

Huyu ndugu anaitwa Alex Mkenyenge ambaye ndiye Mkurugenzi Msaidizi wa Miundombinu Idara ya Michezo ya Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Msomaji wangu unapofanya tathimini ya Kiongozi unampima maisha yake na kila anavyoishi kila siku inayokwenda kwa Mungu na hakikisha kiongozi huyo awe na Shauku ya maboresho ya pahala alipo.

Mwanakwetu anatambua kuwa kwa hakika Tanzania bado haifanyi vizuri katika Sekta ya Michezo na tatizo kubwa mara nyingi Serikali inafuatili sekta hiyo lakini mabadilko yamekuwa ni ya nafasi za juu tu ambapo haya hayo mabadiliko wanaopewa nafasi wengi wao za juu siyo wanamichezo na siyo watu wanaofahamu Sekta ya Michezo ili kuiboresha lazima Idara nzima ya michezo nashauri serikali  ichukue vijana kutoka wenye elimu ya michezo kutoka JWTZ na Jeshi la Polisi waongeze nguvu kwenye idara ya Michezo alafu kila hata Maafisa Michezo Mikoa wote nchini nzima watoke huko JWTZ na Jeshi la Polisi Tanzania waongeze nguvu.


 

Kwa kuwa Tanzania inakwenda kwenye uchaguzi mkuu wa 2025, Katibu wa Mkuu wa sasa na Waziri wake wamalizie ngwe yao alafu tukirudi Novemba 2025 Ndugu Alex Mkenyenge apewe nafasi kubwa ashawishie agombee ubunge ili awe waziri au kama inashindikana awe Katibu Mkuu wa wizara hii, kwa hakika Tanzania tutaondokana na aibu maana yeye anaifahamu hii idara na anatambua hata watu wenye uwezo wapo ambao hawatumiki ipasavyo , nawaambieni  michezo Tanzania itapaa, vinginevyo Tanzania tutakuwa mabingwa wa ndoto zisizokamilika.

Kufanikisha jambo lazima uwepo pahala penye tukio, jambo liwe kero na yule linayemkera afanya jitihada la kutafuta suluhu.kwa kutumia  rasilimali zilizopo na kwa kushirikisha rasilimali zilizopo, ambapo Mwanakwetu anaamini jina Alex Mkenyenge linaweza kuivusha Tanzania katika kiwango kingine kimichezo.Maana tunapohangaika kutafuta Rais wa 2025 basi tunapaswa kutazama huku na kule kutafuta na mawaziri wake.

 

Jamani kwa leo inatosha, ngoja nimeze mate.Maboresho  ya Michezo Baada ya Uchaguzi Mkuu wa 2025..


 

 

Mwanakwetu Upo?

 

Kumbuka;

"Uongozi wa Michezo Baada ya Uchaguzi Mkuu."

 


 

Nakutakia siku Njema.

 

makwadeladius@gmail.com

0717649257


 




0/Post a Comment/Comments