SERIKALI YA MAMA NZURI DOA UTEKAJI-PADRI MSIGALA

 



Adeladius Makwega-BARABARA YA LOBINA-CHAMWINO

“Tulikuwa Mapadri kadhaa tumekaa kwenye treni tunasafiri, tukawa tunazungumza juu ya ya Yule Bongo walioyoshindwa kumteka, tukiwa tunaongea hapa hapa katika gari moshi, mtu mmoja ndani ya treni ambaye hakuwa Padri mwenzetu akanishika begani, Padri mmoja kando yangu akanikonyeza kwa macho akasema angalia sana na wewe usije ukawa miongoni mwa watakaotekwa baadaye. Jamani hili jambo ni mbaya, nawaomba tuliombee, hiki ni kidoa kibaya, hili doa baya, Serikali ya mama(Rais Samia) ninaipenda lakini hili ni doa baya, baya sana, tumuombee mama. Na vyombo vyote (vya ulinzi)! Huko mnapokaa jamani angalieni hili jambo, sijui wanajeshi , uhamiaji, hili jambo baya, ni jambo baya. Kweli kila serikali inayo mabaya yake na hata serikali ya Magufuli ilikuwa na mambo yake lakini hili ni baya baya bay a sana, kama vyombo vya ulinzi vipo vifanyie kazi, vitokomeze, vifanyia kazi suala hili. Nchi yenu wenyewe mnakosa hata uhuru wa kusema ? Kama wakati wa akina Daniel, watu walikuwa hawana uhuru wa kusema huo ni ushamba. Kibaya utekaji sasa unagharimu damu damu za watu.”

 

Haya ni maelezo ya Padri Gidion Msigala katika mahubiri ya Jumapili ya Novemba 17, 2024 dominika ya 33 ya mwaka B wa Kanisa katika Kanisa la Bikira Maria Imakulata Parokia ya Chamwino Ikulu Jimbo Kuu Katoliki la Dodoma. 


 

Padri Msigala kabla ya mahubiri hayo alisomaInjili kutoka Muinjili Marko 13;24-32 ambapo somo hili lilitanguliwa na masomo mawili; Danieli 12:1-3 na Waebrania 10:11-14,18. Akiendelea kuhubiri Padri Msigala alisisitiza juu ya mapambano ya Watanzania dhidi ya watu wasiojulikana.

“Hata Daniel alikuwa akiogopa kusema alikuwa akitumia lugha ya picha. Hata nilipokuwa naangalia ile klipu ya Yule bonge kweli Watanzania tumekuwa namna hiyo tunashindwa hata kusema? Jamani unyenyekevu ukizidi unakuwa upumbavu. Akinamama sita wameshindwa hata kupiga kelele ? jamani ebu tuache hizi tabia, juzi baadhi yetu tumekuwa katika hiyo hali, hauwezi kuona mwenzako anaumizwa wewe umenyamaza tu, tunasema heri wapatanishi watamuona Mungu kukaa kimya unakosa upatanishi lazima uende ukaamue.Mikinikuta na mimi katika hali kama hiyo mnitetee, hapa naweza kuibia nikapiga kelele alafu watu wasije na ninaweza hata kugonga kengele, kesho yake mniulize ati Baba Paroko ulipiga kengele! Hata tukio la marehemu Ali Kibao mtu anachukuliwa kwenye basi watu wapo kimya! Mkiyaacha mambo kama haya hivyo hivyo tambue sasa Wakristo tunajibu majibu ya Kaini baada ya kumuuwa nduguye Abeli. Watanzania sasa tunatoa majibu ya Kaini hii ni jambo la aibu. Hata huyo anayeteka watu anateke wenzake kwa kuwa yu salama, kila mmoja wetu asali Salama Maria, Baba Yetu na Atukuzw, hili ni jambo chafu, baya kwa nchi yetu, dalili ya kumwaga mwaga damu inaweza kumwagwa damu kubwa.”

Awali akianza mahubiri yake Padri Msigala aliwataka waumini wake kuulizana kila mmoja je mwisho wake utakuaje? Akisema mwisho wa mwanadamu una mambo mengi yaweza kuwa elimu, kazi, ndoa, familia, uhai na hata kazi akiwaomba waamini hao kila mmoja aombee awe na mwisho mzuri.


 

Kwa hakika hali ya hewa ya Chamwino Ikulu ni baridi kiasi huku miti ikichanua na hali hii inatoa ishara kuwa mikoa ya Kati ya Tanzania Mvua zinakaribia kuanza kunyesha.

Kwa hakika majira ya usiku eneo hili lilnapamba na milio ya sauti fisi na ngoma ya singeli.

Nayo hali ya kisiasa ya eneo la Chamwino IKulu ni utulivu mkubwa lakini cha kusikitikishwa mtayarishaji wa makala haya hajaona harakati zozote za kuonesha kuwa kuna Uchaguzi Serikali za Mitaa, mitaani hakuna tambo, hakuna hata bendera zinaonesha kupepea majumbani mwa watu na wala hakuna harakati za kupita majumbani kuomba kura.

Hilo limemtia shaka mtayarishaji wa makala haya na alijaribu kuuliza majina ya wagombea wa nafasi hizo kwa tiketi ya CCM kwa watu wanne watu watatu hawakufahamu jina la mgombea wa CCM lakini mama mmoja alitaja jina la mgombea huyu,

“…ndiye alishinda kura za maoni kugombea uenyekiti wa Kijiji cha Chamwino Ikulu.”

Wakati mtayarishaji wa makala anamtambua mgombea wa CCM wa Mtaa wa Kizinga Kata ya Mbagala Wilaya ya Temeke Dar es Salaam kwa tiketi ya CCM anaitwa Mbaraka Iddi huku hivi sasa anazunguka majumbani kuomba kura.


 

 

Athari ya hili ni mara baada ya uchaguzi wananchi kutowatambua viongozi wao na wananchi kutoshiriki katika kuchangia katika miradi ya maendeleo na inaweza kuwa ngumu kuvikia shabaha zinazolengwa na serikali.

 

makwadeladius@gmail.com

0717649257








 Mbaraka Iddi Mgombea mtaa wa Kizinga CCM Mbagala Temeke Dar es Salaam huyu mwneye Kofia.

0/Post a Comment/Comments