Adeladius Makwega-Tarime MARA
Serikali imesema mkoa wa Arusha sasa ndiyo kinara wa vitendo vya Ukali wa Kijinsia, ukifuatIwa na mkoa ya Manyara, huku Mkoa wa Mara ukishika nambali tatu. Hayo yamesemwa na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Dkt. Doroth Gwajima alipokuwa akihitimisha siku 16 za kupinga ukatili wa Jinsia katika Viwanja vya Shule ya Sekondari Ingwe Tarime Mkoani Mara.
“Arusha ina 43%, Manyara ina 43% nanyi ndugu zangu nyinyi Mara mna 28% na Singida 20% , Tanga 19% na Dodoma 18%. Nawaombeni ili Kuondokana na hili janga tu natakiwa kupambana na hali hii kwa kupeleka elimu kwa kila mmoja wetu kama alivyosema mbunge wa jimbo hili mh Waitara.”
Mh Gwajima pia alilishukuru Jeshi la Polisi Tanzania kwa kufanya kazi hii kwa kujitoa mhanga hususani ASP Faidha Seleiman ambaye anafanya kazi naye kwa karibu.
Akizungumza wakati akimkaribisha mh Waziri Gwajima, Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara Erasto Gerald Kusaya alisema ,
“Disemba 9, ni siku ya uhuru wa Iliyokuwa Tanganyika na Sikukuu hii kwa Mkoa wa Mara inatumika kwa kutumia uhuru tulinao kupinga Ukatili wa Kijinsia maana mapambano haya ni yetu sote, Viongozi wote wa Mkoa wa Mara Shabaha yetu ni moja kumlinda mtoto wa Mkoa wa Mara na huko ni kumuunga mkono Rais wa wa Jmahuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye amenui kufa na kupona kumlinda mtoto wa Tanzania. Mtoto wa Kitanzania atalindwa kwa gharama yoyote ile.”
Akizungumza katika hitimisho hilo la siku 16 za kupinga Ukatili wa Kijinsia Meneja Mradi wa Kampuni ya Madini ya Barrick Apolinary Lyambiko amenadi kuwa mgodi wake unatilia maana kupinga Ukatili wa Kinjisia huku akisema kuwa wamepokea tuzo saba katika kusimamia dhamira yao ya uwajibikaji katika jamii ikiwamo Kupinga Ukatili wa Kijinsia nchini Tanzania.
Kwa upande wake Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Kipolisi ya Tarime Rorya Afande Mark Nyera alimthibitishia Waziri Gwajima kuwa kampeni ya Kupinga ukatili wa Kinjisia, siku hizi 16 zimetumika vizuri kupaza sauti juu ya hilo huku akisema kuwa makosa haya ya Ukatili wa Kinjisia kwa sasa yanapungua kutoka mwaka mmoja kwenda mwingine mathalani kutoka mwaka 2023 kwenda 2024 yakiwa chini ya matukio 2000, Kamanda Nyera akisema kuwa siku hizo 16 zinahitimishwa siyo kwamba Jeshi la Polisi Tanzania linaweka silaha chini bali linaongeza nguvu katika mapambano hayo kwa kasi zaidi.
Kwa Upande wake ASP Faidha Seleiman akizungumza kandoni mwa shughuli hii amesema kuwa anashukuru kwa Waziri Gwajima kutambua mchango wake lakini huku pia ni kutambua mchango wa Jeshi la Polisi Tanzania na kutambua mchango wake yeye kama mwanamke nay eye kama afande.
Kwa hakika haya maadhimisho ya Kupinga Ukatili wa Kijinsia yaliyoanza mwishoni mwa mwezi Novemba, 2024 yanahitimishwa huku katika vitongoji, mitaa na vijiji vya mkoa huu mara baada ya shule kufungwa wananchi wa wakishiriki katika zoezi la tohara la vijana wao wa kiume, mwandishi wa ripoti hii ameshuhudia sherehe hizo za Tohara ambapo vijana kadhaa wakiambatana na familia zao wakitoka katika huko huku wakitembea kiukakamavu mitaani, wakipewa zawadi, mataji na vitu vya thamani wakiwa wamejifunga shuka ambazo zimeloana damu, nazo ngoma za asili, muziki vigegelele na ndelemo na vifijo kila kona na hayo yote yakitoa ishara kuwa tohara kwa wananchi wa mkoa wa Mara ni shughuli muhimu sana ambapo hata kupambana na tohara kwa mabinti wa mkoa huu hata namna ya kuiendea inahitaji umakini mkubwa.
0717649257
Post a Comment