INVIROMENTO LIDA WA NYUMBA NYEUPE

 


Adeladius Makwega-Musoma MARA.

KRISIMASI(NOELI) ni mojawapo wa Sikukuu kubwa kwa dini ya Kikristo ambapo Inakumbuka siku ambayo Yesu Kristo, Mkombozi wa huu ulimweegu alizaliwa pale Bethelehemu ya Uyahudi miaka zaidi ya 2000 iliyopita.

“Sikukuu hii inayofanyika kila Disemba 25 ya kila mwaka huwa inatambulishwa na maneno hayo mawili KRISIMASI kutoka Kiingereza Christ’s Mass-Ibada ya Kristo huko neon la pili NOELI linatokan ana neon la Kiingereza Noel, pia neon la Kifaransa Noel ambalo asili yake ni neon la Kilatini ufupisho wake Natalis ikimaanisha Siku ya Kuzaliwa.”

Kwa hakika kila mmoja wetu kama anahifadhi taarifa zake anaweza kuwa simulizi nyingi za kila siku anaposherehekea sikukuu hii tangu azaliwe.

Mwanakwetu siku ya leo anakumba asafiri nawe msomaji wake katika safari fupi ya miaka miwili tangu Krisimasi ya Disemba 25, 2022 hadi Disemba 25, 2024 ndani yake kukiwa na visa viwili.

Krisimasi ya mwaka 2022 Mwanakwetu alisali Kanisa la Bikira Maria Imakulata, Parokia ya Chamwino Ikulu Jimbo Kuu Katoliki la Dodoma, huku misa hiyo ikiongozwa na Padri Paulo Mapalala.

Kwa hakika Kanisa la Bikira Maria Imakulata lilijaa pomoni, Mwanakwetu na aliombatana nao walikaa nje, huku wakifuatilia misa hiyo kupitia spika ya mkono wa kulia nje ya kanisa hilo maana spika ya mkono wa shoto haifanya kazi muda mrefu. 

Misa hii ilipomalizika Mwanakwetu na aliombatana nao wakaanza safari ya miguu kuelekea kwao.Siku hii Mwanakwetu hakuripoti Misa ya Noeli na wala hakurekodi chochote, lakini usiku kuamkia Krisimasi aliripoti mahubiri ya Padri Mapalala.

 Kwa desturi Mwanakwetu huwa haripoti Sikukuu za Noeli na Pasaka kama Misa aliyosali imeongozwa na Katekista au Padri hufanya hivyo ilikutoa nafasi ya ujumbe wa Pasaka wa Jimbo husika uliyotolewa na Askofu au Kadinali usambae ujumbe huo tu.


 

Kwa hakika nyaraka ya Kanisa Katoliki Ulimwenguni ya Mtaguso wa Pili wa Vatikani inayojulikana kama INTER MIRIFICA iliyotolewa Disemba 4, 1963 inapigia chapuo Uinjilishaji kwa  kutumia vyombo vya habari.

Ukiisoma ibara ya nane ya waraka huu inaliongezea na hili.

Kwa kuwa maoni ya umma yana nguvu na mamlaka makubwa zaidi leo katika kila nyanja ya maisha, ya kibinafsi na ya umma, kila mwanajamii lazima atimize matakwa ya haki na hisani katika eneo hili. Kwa hiyo, wote lazima wajitahidi, kupitia vyombo hivi vya habari pia, kuunda na kueneza maoni ya umma yanayofaa.”

Kumbuka msomaji wangu Mwanakwetu anarudi kutoka kanisani huku akiwa amebeba tepu rekoda na Kamera kubwa maana ilikuwa kama tahadhari kama anaweza kukutana na stori njiani lakini pia hawa aliombatana nao walihusudu kupiga picha na twiga wa saruji mbele ya nyuma nyeupe.Nakuomba msomaji wangu ufahamua kuwa Kanisa la Bikira Maria Imakulata lipo Barabara ya Lobina , wakiwa jirani na Barabara kutoka Ikulu kando yao kuna mkahawa alafu ukuta wa nyumba nyeupe.Kundi na vijana wadogo wanaotokea Kanisani wanaongea kwa Kiingereza wakionesha upande wa Ukuta.

“Eee Inviromento Lida kagua mazingira kabla kengele haijalia.”

Mwanakwetu akawa anawafuatilia hawa watoto wanaongea nini? Inviromento Lida inaonekana huku shule kwani ni kiongozi wa mazingira wanamuuliza atoe maksi za mazingira kando ya ukuta wa nyumba kabla kengele haijalia, yaani wanalinganisha mazingira ya shule na hapo walipo.

“Huku mbele kuko vizuri sana lakini huku uchochoroni hakujafanyiwa usafi sasa usiingie darasani hadi huko kote uchochoroni kumefyeka vizuri, umechoma moto majani na matawi ya miti yawe yamepunguzwa.”

Inviromento lida akamaliza kuongea.


 

Mwanakwetu anatamani kucheka lakini ningefanya hivyo hawa vijana wangetambua mzee huyu nyuma anatusikiliza, nikawa nachekea moyoni tu.Tulipofika pahala walipo Twiga wa Saruji vijana hawa wadogo wakagawanyika makundi kadhaa wnegine kushuka na Barabara ya TANESCO huku Mwanakwetu akiombwa awapige picha jamaa aliombatana nao

Mwanakwetu akawapiga picha alipomaliza akaambaamba na Barabara ya Julius Nyerere alafua Maguo kisha Mtaa wa Talama.

Msomaji wangu 2022 ikapita 2023 ikapita na ukaja wakati wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa mwaka 2024, kumbuka Mwanakwetu yupo Kijijini Chamwino Ikulu huwa ana desturi ya kutembea kwa miguu umbali mrefu mida ya jioni kama kufanya mazoezi tu. Siku moja akapitia njia hiyo hiyo Maguo, Talama, Julius Nyerere kuelekea Barabara ya Lobina, akiwa njiani gafla akasikia njaa hivyo kuamua kuingia  katika mkahawa mmoja wa uliopambwa vizuri, kwa mbao za marembo marembo kadhaa kando kukiwa na Bucha. Akaingia na kuagiza chakula na kuanza kula, akiwa anakula macho yake mbele yakitazam ukuta wa nyumba nyeupe akaona ile ile mandhari ya eneo mbele sehemu limefanyiwa usafi vizuri lakini kona ya ukuta huu kukiwa na eneo kama kichaka kidogo kisichofanyiwa usafi, hapo hapa hapa akawakumbuka vijana wale wakati wa Sikukuu ya Noeli ya mwka 2022 na Inviromento Lida wao.Mwanakwetu akiwa hapo mkahawani akaja kijana mmoja ambaye ndiye mmliki wa huu mkahawa anaitwa Remmy ambaye alikuwa ni Kiongozi katika Kamati za Serikali ya Kijiji cha Chamwino.

“Mzee Makwega kwema?Vipi mbona hatuonani?”

Mwanakwetu akajibu ni mwema, nipo, vipi Renny umegombea uongozi wa kijiji mwaka huu?Jamaa huyu alijibu kuwa sijagombea. Mwanakwetu alipomaliza kula akatoka zake kurudi nyumbani kwake, njiani akakutana na baadhi ya watu ambao walikuwa katika harakati za uchaguzi huu, wakiuliza Mwanakwetu unatokea wapi? Akajibu anatokea kula katika mkahawa wa Renny. Jamaa mmoja akawa anacheka mno , kumbe yule ni rafiki yako? Mwanakwetu akajibu eehh yule ni kijana ninayemfahamu hapa Kijijini Chamwino Ikulu. Jamaa mmoja akasema ee Kura za maoni CCM ulikuwepo? Mwanakwetu akajibu kuwa hakuwepo. Jamaa akasema aah mwandishi wa habari ulikosa mambo.

“Rafiki yako Renny alikuwa miongoni mwa watia nia wa Uenyekiti wa Kijiji cha Chamwino Ikulu, mchakato wa kuomba kura ulivyoanza tu kijana ana nyota yake ilikuwa inang’aa mno, chama kikatoa ratiba ya kuzunguika matawini kuomba kura. Tulipofika katika tawi la kwanza Renny alishangiliwa mno na kila alipokuwa anaongea yeye, wanachama wa CCM wakawa wanamshangili mno baada ya kuongea wanaccm wakawa wanatoka mkutanoni wakisema mwenyekiti wetu ni Renny,hakuna mwingine, hali ilikuwa hivyo matawi ya awali na kivumbi ikawa siku iliyofuata cha kustajabisha, Renny aliitwa jukwaani kuomba kura kwa wanaccm wenzake, akiwa anashika kipaza sauti, sauti iligoma kutoka ukumbi ukapata taharuki Renny akaanguka chini, kwa hali yake ilivyokuwa mbaya siku hii hakuweza kuomba kura , wagombea wengine waliomba kura na hadi kura za maoni zinapigwa Renny alikuwa amelazwa  hospitalini.

Kilichotokea kilishangaza mno lakini ndicho kilichokea, jambo hili limewatisha sana wagombea vijana kwa nafasi hii ya Uenyekiti hapa Kijijini Chamwino Ikulu, wakiamini kuwa watu walikwenda kufanya mambo ugangani kumdhibiti kijana Renny ambaye upepo wake ulikuwa unavuma vizuri.”

Mwanakwetu akawaambia hawa jamaa kuwa namna alivyokutana naye mkahawani na alivyomuuliza juu ya uchaguzi.Mwanakwetu akaagana na hawa ndugu kisha kurudi zake kwake.

 


Mwanakwetu anasema nini siku ya leo?

Kwa hakika kijana Renny aliaguka jukwaani na kitendo hicho kiliwapa nafasi mgombea mwingine kushinda. Mwanakwetu anaona ni jambo la kawaida kisiasa mgombea kuanguka jukwaani maana hata wakati wa uchaguzi Mkuu wa 2005 mgombea Urais wa CCM Jakaya Kikwete katika Mkutano wa Jangwani alianguka lakini mwisho siku alichaguliwa kuw Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Jamii hapaswi kuogopa kama mgombea wake ameanguka jukwaani ikumbukwe kuwa sisi ni binadamu lolote linaweza kutokea muda wowote ule kama kumetoka changamoto hilo lifuatiliwa na mambo mengine yangoje huyu aliyepata changamoto akikaa sawa ndipo mambo mengine yaendelee.

Shabaha ya pili ya makala haya ni juu ya wale wanaofanya kazi katika ukuta mweupe wajaribu kuzungukia eneo lao nje ya ukuta wetu ili kuondoa utata wa mazingira yale maana Inviromento Lida na wenzake waanatarajia kuwepo eneo hili wakati wa mwaka mpya 2025 ili akute mambo mazuri.Kufuatilia hili kwa kina linatoa ishara njema kwa wanaofanya kazi nyumba nyeupe kama wakipewa majukumu zaidi nje ya nyumba nyeupe wataweza kuifanya vizuri.


 

Mwanakwetu anatumia Krisimasi hii ya mwaka wa 2025 kwa kisa cha wanafunzi wale juu ya Ivironmento Lida namna walivyokuwa wanaigiza juu ya eneo la ukuta wetu mweupe kufanyiwa usafi ili kuibua hoja ya utoaji wa maoni bila woga kama Intermirifica nyaraka ya Mtaguzo wa Pili wa Vatikani iliyotolewa mwaka 1963 inavyoagiza.

Mwanakweu upo?

Je makala haya Mwanakwetu hayaiteje? Kijana Renny Aliyedondoka Jukwaani au Inviromento lida Wa Nyumba Nyeupe?

Mwanakwetu anachagua Inviromento Lida wa Nyumba Nyeupe.

Nakutakia Krisimasi Njema.

makwadeladius@gmail.com

0717649257


 


 


 

0/Post a Comment/Comments