Adeladius Makwega-MUSOMA VIJIJINI, MARA.
Hii ni Disemba 5, 2024 Mwanakwetu anatokea eneo la Musoma vijijini ambapo kulikuwa na jukumu la kutayarisha makala mbili ; moja juu ya Kukamilika kwa Hospitali ya Wilaya ya Musoma Vijijini na Kukamilika kwa Jengo la Halmashauri ya Wilaya ya Musoma Vijijini ambapo kwa hakika kazi hii kidogo ilikuwa nzito ambapo mengi yatakuwepo katika makala ya Jengo la Halmashauri ya Wilaya ya Musoma Vijiji itakapotayarisha.
Msafara huo ulikuwa wa watu watatu Ruban Gideon Chilingani, mwananahabari Musa Makamu na Mwanakwetu, walipata bahati njema ya kuambatana na Afisa Habari ya Halmashauri ya Musoma Vijijini ambayo ipo katika Wilaya Musoma yenye Mkuu wa Wilaya makini sana akisimamia Halmashauri mbili ile Manispaa na hii ya Kijijini.
Kwa bahati nzuri Wilaya ya Musoma inaye Mkuu wa Wilya ndugu mmoja makini sana, narudia maneno haya ambaye kwa hakika tulizungumza naye juu ya mambo kadhaa tukiwa njiani kutayarisha makala haya.
Afisa Habari wa Halmashauri ya Musoma Vijiji mwanahabari Endrew Mbasa alitoa ushirikiano mzuri na aliamua kuambatana na akina Mwanakwetu katika miradi iliyopo katika eneo lao ikiwamo huu Mradi wa Maji wa Mgambo , Kiabakali, Butiama..
Mwanakwetu akiwa gari hii akitafakari namna kazi hiyo ilivyokuwa ngumu alichukua kabrasha Kutoka Afisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara Mh Kanali Evans Alfred Mtambi ambalo lilinadi haya,
“MAMLAKA YA MAJI MGANGO KIABAKARI
Serikali ya Tanzania kwa Kushirikiana na BADEA na Serikali ya Saudi Arabia inajenga mradi wa Maji wa Mgango- Kiabakari- Butiama kwa gharama ya shilingi bilioni 70.5. Mkandarasi wa mradi huu ni UNIK Construction Engineering Lesotho (PTY)LTD. Mradi huo ulianza kutekelezwa mwaka 2020 na umewekewa jiwe la msingi na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Februari 6, 2022.
Utekelezaji wa mradi unahusisha ujenzi wa choteo la Maji (Water Intake) lenye uwezo wa mita za ujazo 35,000 kwa siku pamoja na bomba la kusafirisha maji ghafi (raw water transmission pipe) kutoka kwenye choteo hadi kwenye sump; ujenzi wa mtambo wa kutibu Maji (Water Treatment Plant); ujenzi wa tenki la maji safi (Clear Water Tank) lenye ukubwa wa mita za ujazo 2400; ujenzi wa vituo vya kusukuma maji (Pumping Station) tatu;ujenzi wa jengo la ofisi katika eneo la mtambo na nyumba ya watumishi;ujenzi wa jengo la ofisi ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mugango – Kiabakari – Butiama; ujenzi wa Matanki ya kuhifadhia maji ya Kyatungwe 100m3 (Ukarabati); Kong Hill 500m3, Bumangi 1000m3, Butiama 2500m3, Kiabakari 3000m3; ulazaji wa Bomba kuu kilometa 47; ulazaji wa bomba za usambazaji kilometa 140; ujenzi wa vituo 40 vya kuchotea maji na ununuzi wa dira 2000 za maji. Kwa sasa mradi upo katika hatua za ukamilishaji na wananchi wa vijiji vya Wilaya za Musoma, Bunda na Butiama wameanza kupata maji. ”
Mwanakwetu akiwa wenzake hao akiongeza afisa habari wa Musoma DC mwanahabari Mbasa sasa wanaingia katika mradi huu na kupokelewa vizuri na vijana watatu na binti mmoja mhandisi.
Kikosi hiki kwanza kabisa kilizungushwa kuona eneo lote la mradi huu wa kimkakati na kuoneshwa upande wa mwisho wa eneo hilo kukionekana maji mengi na Mwanakwetu alipouliza yale maji ni nini? Alijibiwa kuwa hilo ni Ziwa Victoria maana chanzo cha maji ya mradi huo ni Ziwa Victoria.
Mwanakwetu akiwa anazunguka mradini mara baada ya kuona Ziwa Victoria tu maji yake yakigongagonga katika kingo za mradi huu , akakumbuka makala mbili zilizochapishwa na gazeti la THISDAY la Tanzania mwaka 2007 ukurasa wake wa 18&19 kwa siku mbili tofauti ,
“Hukumu ya Kifo Imepitwa na Wakati-Death Penaty Is Out of Tune by Adeladius Makwega na makala ya pili ni Jirani na Bahari Mbali na Maji-Close to the Sea Far From Water By Tito Mganwa ,
Wakati huo magazeti ya THISDAY&KULIKONI yalikuwa yanachapishwa na kampuni ya MEDIA SOLUTION LTD Jijini Dar es Salaam huku wakiwa mahiri wa habari na makala za uchunguzi. Hata makala hizo mbili zilikuwa zinamdunga mtu sindano ya Kristapeni na yeye bila ya kusikia maumivu.
Tito Mganwa akiwa mwanachuo wa mwaka wa tatu naye Adeladius Makwega akiwa mwanachuo wa mwaka wa pili Chuo Kkuu cha Tumaini Iringa Shahada ya Sanaa ya Habari ya Chuo hiki cha Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) mwka 2007 walifanya kazi hizo mbili.
Makala ya kutilia maanani ni Close to the Sea Far From Water ambayo ilizungumzia hali halisi ya eneo la Mtoni Kijichi Temeke Dar es Salaam , uhaba wake wa maji ikiwa kero kubwa ya wananchi hao huku makadhi yao yakiwa pua na mdomo na Bahari ya Hindi.
Mwanahabari Tito Mganwa akiwa kijana alijipa upofu kuwa maji ya bahari kuwa na chumvi? Akijibu kuwa maji hayo yanaweza kutumiwa kwa kuogea na hata kuoshea vyombo lakini si kwa kunywa huku akinadi kuwa kuogea na kuosha vyombo nazo ni kazi za maji pia, akiomba uhaba wa maji Mtoni Kijichi upatiwe ufumbuzi
Tito Mganwa aliwatetea wakazi wa Mtoni Kijichi hadi makala hayo kutolewa kivuli chake na kupachikwa kuta katika Ofisi ya Mtendaji wa Mtaa wa Mtoni Kijichi wakati huo. Kwa hakika baadaye suala hilo la maji lilipatiwa ufumbuzi wa wananchi wa Mto Mtoni Kijichi-Temeke Dar es Salaam kuondolewa kero hiyo.
Hivi sasa Tito Mganwa ndiye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Chamwino ilipo Ikulu yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.”
Mwanakwetu akajiuliza moyoni kuwa leo ni yale yale ya Tito Mganwa ya mwaka 2007 yaani Close to The Sea Far From Water?
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino, Mwanahbari Tito Mganwa.
Mwanakwetu akakutana na Mhandisi Sofia Gwando ambaye ni mhandisi mzalishaji katika mamlaka ya maji ya Mgango Kiabakari Butiama na yeye kuanza kwa maneno haya,
“Mradi wetu ni wa miaka mingi, awali mradi huu ulikuwa unasambaza maji bila ya kuweka dawa, mradi huu sasa unasambaza maji yaliyowekwa dawa, tangu hapa Mgango, Kiabakari hadi Butiama .Sasa tumepata mtambo mkubwa unaosaidia maji hayo kabla ya kusambaza kuwekewa dawa vizuri kwa uhakika na umakini wa hali juu.”
Mhandisi Sofia Gwando akataja wazi wazi kuwa mitambo yao ina uwezo mkubwa ambapo kwa mwezi wanazalisha kubiki mita 542,500,
“Hesabu yake ni kuwa kila siku tunazalisha kubiki mita 17500 kutoka Ziwa victoria.”
Mhandisi Sofia Gwando hakuwepo peke yake bali wapo wataalamu wengine wanaofanikisha zoezi hilio ili kutatua na kuondoa kabisa dhana Close to the Sea Far From Water. Kwa hakika maji hayo yanazalishwa Mngambo yanasambazwa Mgango pia yanakwenda Kiabakari na kumfikia mwananchi wa Butiama.
Kwa upande wake Emanuel Mwalongo ambaye ni Mkemia alisema maneno haya,
“Nipo hapa kuhakikisha wananchi wanapata maji safi na salama katika maisha yao ya kila siku, tunachukua maji haya kutoka ziwa Victoria kisha tunajatibu, maji yakiwa safi na salama maji haya yanasambazwa.
Maji kabla ya kutibiwa yana wadudu wa aina mbalimbali, wakati mwingine yana tope tele, hasa kipindi cha mvua tukishayatibu ndiyo yanasambazwa kwa wananchi wetu.”
Mwanakwetu aliuliza ni wakati gani hali ya maji huwa ni hatari mno? Mkemia Mwalongo alijibu,
“Kwanza ziwa huwa linatabia ya kujisafisha kwa kutoa uchafu ziwani na kuutupa kando ya kingo lenyewe lakini vimelea vilivyopo katika maji vinabaki hivyo hivyo, kuviondoa ndani ya maji jukumu lake ni kuvitibu kwa kutumia kemikali mbalimbali.
Tunaishukuru Serikali inayoongozwa na Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungnao wa Tanzania kwa kufanikisha kemikali hizi kupatikana kwa wakati mathalani Klorine , Lime na PAC .”
Mwanakwetu akiwa katika mradi huu alikaribisha na mlima wa shukurani na pongezi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano kutoka kwa mhandisi Sophia Gwando naye Mwanakwetu akinukuu maneno hayo kama yalivyo.
“Tunaishukuru kwa serikali kutuletea mradi huu wa shilingi za Kitanzania Bilioni 70.5 hapa Mkoani Mara na umetusaidia hata sisi kupata kazi mradini.”
Desturi inaonesha kuwa jamii kando ya vyanzo vya maji iwe Bahari , ziwa na hata mito ni jambo la kawaida kwenye vyanzo hivyo wananchi kuchota maji kama yalivyo na kuyatumia bila ya shaka yoyote kwa kunywa, kwa kupikia na hata matumizi mengineyo. Jambo hilo limefanywa na jamii nyingi za Kiafrika tangu enzi, hoja ni je maji haya yana athari kweli kwa jamii kama yakitumika kama yalivyo?
Peter Zeno Mulenga ambaye ni mtaalamu wa maabara katika mradi huu wa Mgango Kiabakari anasema haya.
“Kazi yangu ni kuhakisha maji yaliyotibiwa yanatoka salama na kumfiaka mteja, maji haya yanatibiwa kwa kutumia PAC, Lime na Klorine. Kazi ya Lime ni kuyang’arisha, wakati kazi ya Kloride ni kuua vijijidudu vyote ndani ya maji, na kama mtu anadiriki kuyatumia maji yasiyotibiwa ni kuhatarisha uhai wake.”
Mradi wa Maji wa Mgango, Kiabakari Butiama ni mradi mkubwa unahitaji ufuatilia wa karibu wa hatua kwa hatua na ndiyo maana baadhi ya watumishi hawana budi kukaa jirani na mradi huu . hapa Mgango watumishi kadhaa wanakaa hapo wakiwa na nyumba kabisa iliyojengwa kwa ajili yao.
“Mimi ni fundi Mshundo wa mradi huu ninaishi hapa hapa na kazi yangu kubwa ni kusimamia mitando hii na kutatua changamoto kadhaa zinazoweza kutokea wakati wote nikipeana zamu na wezangu saa 24.”
Haya ni maelezo ya Emili Kadasa.
Mwanakwetu aliagana na wataalamu hao na kuanza safari kuelekea Halmashauri ya Butiama.
Mwanakwetu anasema nini siku ya leo?
Kwa hakika bila ya kuuma maneno vijana hawa hapa wanaofanya kazi katika Mradi wa Mgango Kiabakari Butiama wanafanya kazi vizuri wakiwa chini ya usimamizi wa mhandisi Sofia Gwando huku wakishirikiana kwa nguvu na moyo wote, wakichapa kazi vizuri kuhakikisha wananchi wanapata maji safi na salama.
Huu ni mradi mkubwa wa maji wa Kimakakati ambapo Bilioni 70.5 zinalazwa ardhini kuhakikisha Watanzania tunapata maji safi na salama ili kuepukana na maradhi ya tumbo na magonjwa mengine na kulipunguzia mzigo taifa gharama za matibabu na huko ni kulinda uhai wa Watanzania.
Kwa mradi huu na kwa kujionea kwa macho yake Mwanakwetu sasa aliamini dhana yake mpya ya Karibu na Ziwa Jirani na Maji safi na Salama na kuiwek kando dhana ya mwanahabari Tito Mganwa ya Close to the sea far from water.
Msomaji wangu ngoja nikupe siri ya jambo moja ambalo liliibua mjadala mkubwa katika safari yetu baada ya kutoka katika Mradi huu wa Mgango Kibakari, Butiama, mradi wa kimkakati wa mkoa wa Mara.
“Kwa hakika kwa namna mhandishi Sophia Gwandu alivyokuwa anaelezea mradi huu na kuyajibu maswali kadhaa na huku akitoa ushirikiano, jambo hilo liliwavutia mno watu wote wane, al manusura tumuache mdau mmoja hapo hapo mradini.
Tulimwambia ndugu huyu kuwa hapa hauweza kuingia kabisa ndani ya eneo la mradi ukiwa mwenyewe sisi tumepata bahati ya kuingia humu kwa kuwa tunafanya kazi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara Kanali Evans Alfred Mtambi, kinyume chake kama unataka kuingia ndani ya mradi huu kila mara unaomba uhamisho alafu unakuwa mtumishi wa mradi huo lakini kumbuka kada yako lazima iwepo mradini.
Jamaa akawa anacheka tu, jamaa mwingine akasema kama yanayosemwa ya kweli unaenda kuomba uhamisho unahamia mradini alafu unafika kuripoti uliyemfuata anahamishiwa mradi mwingine, hapo mambo yatakuwaje?Katibu Mkuu Utumishi sasa anatoa uhamisho wa kumfuata mwenza. Safarini wadau wakawa wanacheka tu.”
Kwa hakika msomaji wangu hii ni siri usimwambie mtu baki nayo kama ilivyo, hili siku nyingine nikupe siri nyingine.
Mwanakwetu Upo?
Kumbuka kumbe sasa ni,
“Karibu na Ziwa jirani na Maji.”
Nakutakia siku njema.
0717649257
Post a Comment