Adeladius Makwega-MARA
“Tunafanya kazi hii sana, maeneo mengi , yapo makanisa machache yanayojengwa kwa kenchi za chuma na hata tulipofika hapa tukasema, kweli Serikali ya Mama Samia Imejipanga, Kama Inaezeka Kwa kenchi za Chuma.”
Haya ni maelezo ya fundi anayechomelea makenchi ya chuma Shule ya Wasichana Mara, Jioni ya Disemba 27, 2024 ambapo Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo chini ya Usimamizi wa Serikali ya Awamu ya Sita Mkoani Mara , mkoa unaongozwa na Kanali Evans Alfred Mtambi unaendelea kwa kasi kazi zote japokuwa hivi sasa ni Msimu wa Sikukuu ya Krisimasi na Mwaka Mpya.
Haya yamebainika Wilaya ya Musoma, Wilaya ya Butiama, Wilaya ya Bunda na Wilayani Serengeti huku kazi hizo za ujenzi zikifanyika kwa kasi kubwa na Makatibu Tawala wa Wilaya zote walikuwapo katika miradi hii na wananchi wakiendelea kupata huduma.
Masikio ya Mwandishi Wetu yakikaribishwa kwa shangwe ya milio ya nyundo, misumari, mabati na makoleo yanayochanganya mchanga na kufyatua tofali na pia mashine za kuchomelea, karibu hiyo ikiwa sambamba na mafundi wazawa wakichapa kazi,
“Sisi ni mafundi wa kuchomelea, tunatokea Mwanza, tupo hapa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mara, tumepata kibarua cha kuchomelea mabomba ya chuma yanatumika kama kenchi za bwalo kubwa la Shule hii, litatumika kwa kulia chakula na matumizi mengine .”
Fundi huyu kwa furaha tele alisema kuwa makenchi haya ya mabomba ni gharama kubwa, mtu mwenye fedha za wasiwasi na mawazo hawezi kuweka kenchi la chuma na kenchi za chuma ni sahihi kwa miradi ya umma ambapo ni mkataba wa milele.
Kwa utafiti mdogo wa Mwandishi Wetu amebaini kuwa ukumbi huu wa Shule ya ya Wasichana ndiyo utakuwa ukumbi mkubwa wa kisasa Wilayani Bunda, ukikamilika utaisaidia shule hii hata kujiongezea kipato pale utakapokodishwa.
Katika safari hii Mwandishi wetu kutoka Ofisi ya Mkoa wa Mara aliweza kuona miradi kadhaa ikiendelea na kazi kama vile Hospitali za Wilaya, Majengo ya Halmashauri, Shule za Msingi na Sekondari ambapo miradi hiyo yote fedha za Maendeleo zimetolewa na Serikali ya Awamu ya Sita inyaoongozwa na Dkt . Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jmahuri ya Muungano wa Tanzania.
0717649257
Post a Comment