Adeladius Makwega-Bweri-Musoma MARA
Disemba 9, 2024 Serikali imehitimisha siku 16 za kupinga Ukatili wa Kijinsia na shughuli hizo zilifanyika Tarime mkoani Mara, huku shughuli hii ilifungwa na Mh Dkt Doroth Gwajima ambaye ndiye Waziri mwenye dhamana nayo nchini Tanzania. Kwa bahati nzuri Mwanakwetu alikuwa miongoni mwa Watanzania walioshiriki tukio hilo.
Miongoni mwa mambo mengi yaliyoongewa na serikali ni haya,
“Wanawake na wasichana mara nyingi hupata athari za unyanyapaa au kutengwa wakiwa hawajakeketwa. Siku ya leo katika mtandao wakati nakuja Tarime katika shughuli hii ya kupinga Ukatili wa Kijinsia, niliandika katika mtando juu ya safari yangu. Kijana mmoja akaandika maneno akisema ndiyo maana tunaona huko alafu baadaye tunaacha na kwenda kuoa kwingine.
Jamani eeh ile shughuli inahitaji ujiachie, yaani wewe unataka (tendo la ndoa) mwenzako anasema anaumia, mle ndani mnagombana, haya mambo yanahitaji mtu aseme ukweli ili tuelewane. Wewe unakakamaa mithili ya umewekewa zege, jamani eeeh nyie mnaongeaongea tu, hii limekaaje?
Ule ulimwengu wa sayansi, ulimwengu wa sayansi, Mungu ameutengeneza. Sisi tunauharibu na matokeo yake mnaniambia mimi watoto wako mtaani, baba yupo kushoto na mama yupo kulia, huyu anatafuta amani zake hapati, huyu anakwenda kutafuta kule… mnakuja kwa Gwajima, kumbe kuna mengi yaliyomo humo ndani…mama yake na baba yake wapo wapi ?
Tusiongee kwa kuogopaogopa, mle mle ndani kuna homoni , mamirija maunyevunyeuvu sasa mnaviaribu hovyo hovyo alafu mnasema…. vurugu kwa nini tunajitafutia vurugu ? Wakati maisha yenyewe mafupi?”
Mwanakwetu akiwa katika shughuli hii, huku maneno haya yakitamkwa alikuwa akitazama sura za watu waliyokuwa kando wakimskiliza waziri huyu, jambo hili la tazama tazama ya Mwanakwetu lilifanywa kwa umakini mkubwa kwa upande walipokuwapo machifu na hata upande walipokuwa wamekaa akina mama watu wazima wa Tarime ambapo mwishoni walipewa mitungi ya Gesi ya Taifa.
Sura zao hazikuridhika kabisa na maneno hayo huku wakawa wakiongea kwa sauti ya chini ambapo sura zao zilimpa tafsiri kubwa Mwanakwetu ambapo Waziri Dkt Doroth Gwajima aliyekuwa umbali wa mita karibu Sabini hakuweza kujaliwa kulitambua hilo.
Swali la Mwanakwetu alilojiuliza je Serikali inaliendea kwa umakini suala la Ukatili wa Kijinsia hususani ukeketaji?
“Kwa mujibu wa Taarifa ya Umoja wa Mataifa inadai kuwa kati ya wanawake milioni 100 waliokeketwa duniani, milioni 92 wanaotokea barani Afrika, huku milioni 8 tu ndiyo mkusanyiko kutoka mabara mengine .”
Kwa mtazamo wa Mwanakwetu anaona kuwa jambo hili haliendewi vizuri kwa namna linavyochukuliwa kwa kudhalilisha kundi kubwa la wanawake waliokekeketwa ambao jamii husika inawaheshimu , wakiwa na hadhi juu kuliko wanawake wasiokekeketwa na hapa tunapaswa kuwapa heshima yao kama makamanda wa mapambano haya, wangekuwa mawakala wazuri kwa kulisemea jambo hili.
Mwanakwetu akiwa katika shughuli hiyo alijiuliza juu ya yule kijana aliyesema maneno yaliyonukuliwa na Dkt Doroth Gwajima katika kuhitimisha siku hizo 16 ya kupinga ukatili hio kutoka mtandaoni je kijana huyu anatambua wazazi wake kama hawakupitia hali hiyo? Kama atatambua hilo hapawi kuzipa heshima hisia zake tu bali akumbuke na pengine mzazi wake alipitia huko.
Hilo ni swali la kujiuliza mimi na wewe, ili kuwapa heshima wanawake na mabinti walikwisha keketwa nia waweze kushiriki mapambano haya vizuri, maana matumizi yoyote ya lugha ya dharau kwao yanawadunisha na kuwaweka kando katika mapambano dhidi ya ukeketaji.
Mwanakwetu anasema,
“Wanawake waliokeketwa wana thamani kubwa ambayo ni sawa na wanawake ambao hawajakeketwa, ambapo ni vigumu kila mmoja kutambua kuwa anazaliwa na wazazi waliyopitia mila hii au laa, maana kutaka kujua hili ni matusi kwa mujibu wa mila za Kiafrika.
Tanzania inawajibu wa kumlinda mtoto wa kike ambaye hajakeketwa lakini pia ina wajibu mkubwa kuhesmimu thamani ya mwanamke bila kujali ana kilema gani iwe katika jicho ,iwe jino , iwe sikio , iwe mguuu au hata viungo vya uzazi.”
Mwanakwetu analitazama jambo hili kwa jicho la pekee mno maana namna linavyoendewa anaaminitunaweza kushindwa mapema huku wapiganaji walio mstari mbele wamejitwika silaha zinazotumika kuwasukuma kando wapiganaji wengine ambao wanaofahamu ramani ya vita , hao ni wasichana na wanawake waliokeketwa.
“Akinana mliokeketwa nawapa heshima zenu tele nikiwaomba kwa heshima taadhima mnahitajika katika mapambano haya natambua mna upendo kama akina mama wengine , wapo mliozaa vizuri au kwa tabu kama akina mama wengine, mpo ambao mnatunza vizuri ndoa na familia zenu kama wanawke wengine na mpo ambao ndoa zenu zipo imara kama ngome ya dola ya Rumi.”
Kwa hiyo Serikali Tukufu yetu inawajibu wa kupima namna sahihi ya kuliendea, maana akina mama waliokeketwa wanayo nafasi ya kufaniksiha binti zao kukeketwa au kutokeketwa lakini kama tukiwazungumzia kwa heshimu bila kuwa na maneno ya kebehi na dharau akina mama hawa watatoa ushirikiano mkubwa katika mapambano dhidi ya ukeketaji na Ukatili wote wa Kijinsia nchini Tanzania.
Kwa hakika Mwanakwetu anatambua fika kuwa,
“BInadamu anayo mahitaji ya aina mbili ya kiroho na kimwili lazima tumpe mafundisho ya kiroho na kimaadili kwa heshima ambayo itakayomsaidia namna sahihi ya kumfikia muumba wake, hata kanisa linapinga vitendo vya ukatili wa kijinsia.”
Huku haya yakisemwa pia na Sista Petroni Bahaa ambaye alikuwa mwakilishi wa , madhehebu ya dini hapo Tarime Disemba 9, 2024.
Mwanakwetu anasema nini siku ya leo?
Kikubwa hasa upande wa serikali kujitahidi mno kulikemea suala hili la ukeketaji ambalo ni baya lakini huku ikikumbuka kutumia lugha sahihi na heshima kubwa huku kuwashirikisha akina mama waliyopitia huku .
Nakuuma sikio msomaji wangu kuwa makala haya ya uchambuzi yametayarishwa kwa heshima ya Askari wawili wa Jeshi la Polisi Tanzania ambao ni ASP Faidha Seleiman na Afande Exaud Waya ambao Mwanakwetu alikutana nao hapo Tarime Disemba 9, 2024 katika maadhimisho haya.
Mwanakwetu Upo?
Kumbuka
“Mapambano dhidi ya Ukeketaji Hatuyaendei Vizuri.”
Nakutakia siku Njema.
0717649257
Post a Comment