MARA YAVUKA LENGO UKUSANYAJI MAPATO

 

Adeladius Makwega-Musoma MARA

Mkuu wa Mkoa wa Mara, Kanali Evans Alfred Mtambi, Disemba 20, 2024 ameipongeza Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) kwa namna inavyofanya kazi, huku ikitimza jukumu lake la ukusanyaji wa mapato na Mkoa wa Mara una fursa nyingi mpya.

“Shabaha ya Serikali ya Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, fursa zote mpya zifikiwe kama vile mifugo, uvuvi, madini, utalii, viwanda na biashara.”

Akizungumza kwa sauti ya chini, neno kwa neno kandoni akiwa Kamishina wa Kodi za Ndani Alfred Mredi, Kanali Mtambi alisema,

“Mamlaka ya Mapato Tanzania Mkoa wa Mara inashirikiana vizuri na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara.

Ofisi yangu ipo sambamba na Mamlaka ya Mapato hatua kwa hatua.”

Akizunnguza mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Mara Ofisini kwake Kamishina wa Mlipa Kodi ndugu Mredi alisema kuwa yeye yupo hapa kwa niaba ya Kamishina wa TRA Tanzania,

“Mara kadhaa kumekuwa ugumu wa baadhi ya walipa kodi, kuwa wazito katika kutimiza wajibu wao, kwa hakika Serikali yetu tunaipongeza maana imekuwa ikitushika mkono TRA.”

Kamishina Mredi alisema kuwa ushirikiano huu wa Serikali kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania unaonekana wazi kwa Mkoa wa Mara na matokeo yake tangu Julai 2024, kwa miezi mitano mfululizo, TRA imekuwa ikivuka malengo na huu ni ufanisi  wake kwa 118%.



 

“Shabaha ya TRA kwa sasa inatamlenga kila mlipa kodi alipe kodi kwa amani bila migogoro na watumishi wetu, bila ya majuto. Kama wananchi wakilipa kodi wakiwa na majuto hata kama Serikali itafanya maendeleo kwa kiasi gani, hilo litakuwa halina maana.”

Katika kutambua mchango wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara, Mamlaka ya Mapato Tanzania ilikabidjhi zawadi kadhaa kama kutambua mchango wa Serikali Mkoa wa Mara kufanikisha TRA MARA kuvuka malengo ya ukusanyaji Kodi .

Wakati haya yakifanyika, mandhari ya mitaa ya Musoma Mjini, hali ni ya utulivu, huku Askari wa Usalama barabarani wakiwa makini wakihakikisha Sherehe ya Krisimasi na Mwaka Mpya zinafanyika kwa amani na utulivu kama lilivyo agizo la Mkuu wa Mkoa  Mara lililotolewa Disemba 19, 2024.

 makwadeladius@gmail.com

0717649257

 







 

0/Post a Comment/Comments