Adeladius Makwega-MARA
“Nimetibiwa Hospitali ya Mlongazila miezi 11, ninaleta kero kwako hasa wazee wasiona, binafsi nina cheti cha huduma ya tiba kwa wazee bure, nina miaka 82, hapa ninakuja bado ninatibiwa, nina cheti cha wazee chakutibiwa bure wanasema lipa , hii mkuu inanipa tabu , hii ni kero labda kwangu mimi tu!”
Haya ni maelezo ya Magesa Maseke maarufu kama Gongo la Mboto akiuliza swali hilo kwa Mkuu wa Mkoa wa Mara Mh Kanali Evans Alfred Mtambi Disemba 2, 2024 wakati akifanya mapokezi ya madaktari bingwa karibu 50 ambao wamekita kambi katika Hospitali ya Kanda ya Kumbumubu ya Mwalimu Julius Nyerere iliyopo Musoma Mjini mkoani Mara.
Kukiwa na umati mkubwa wa wananchi wa Wilaya ya Musoma na wengine kutoka wilaya zingine zinazounda mkoa huu, waliojongea kupata huduma za tiba kutoka kwa mabingwa hao, Kanali Mtambi alisema kuwa uwezo wa Watanzania unatafautia wapo vijana wana uwezo mkubwa wa kipato na pia wapo wazee wenye kipato kikubwa.
“Ndiyo maana kwa mujibu wa sera ya afya wazee& watoto wanatibiwa bure na hata wewe mzee Magesa Maseke unatakiwa kutibiwa bure .”
Mara baada ya majibu haya Kanali Mtambi aliimbiwa utenzi na mama mmoja mgonjwa ambaye alikuwa miongoni mwa walifika kupata huduma hiyo ya Madaktari Bingwa.
“Pongezi tunazitoa sana kwa Mkuu wa Mkoa, kuwasili hapa Kwanga.Hatuna la kusema na huba tunaliweka kwako Uongozi wako uwe chanda chema uvishwe pete kidoleni.”
Awali akizungumza kabla ya uzinduzi wa kampeni hiyo Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mara Dkt Zabron Masatu ambaye pia alimuwakilisha Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara alisema,
“Sekta ya afya tumejiandaa vizuri kuifanya kazi hii kwa siku zote tano na tunavyo vifaa vya kutosha kwa zoezi hili.”
Awali mkuu wa Wilaya ya Musoma Mh Juma Chikaka alimshukuru Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungamo wa Tanzania kwa kuipa nafasi hiyo wilaya ya Musoma huku akisisisitiza wananchi wa Wilaya ya Musoma na viunga vyake kujitokeza kwa wingi kuchangamkia hisani hiyo.
makwadeladius @gmail.com
0717649257
Post a Comment