Adeladius Makwega-Musoma MARA
Kwa siku mbili mfululizo yaani Disemba 10 na 11, 2024 Mwanakwetu amekuwa jirani na timu ya Wizara ya Katiba na Sheria waliokita kambi Mkoani Mara katika Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Dkt Samia Suluhu Hassan ambaye ndiye Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Taifa hili la Mashariki ya Afrika.
Hapa Mkoani Mara uzinduzi wa kampeni hii umefanyika Disemba 11, 2024. kwanza kwa kuimba wimbo wa Taifa la Tanzania ambapo linatarajia kufanya uchaguzi wake Mkuu mwishoni mwa mwaka wa 2025.
Baadaye aliakwa Shekhe wa Mkoa wa Mara Ustadh Msabaha Bini Kassimu na kisha kusomwa sala la ufunguzi, kutoka madhehebu ya Kikristo .
Kwa hakika mambo kadhaa yamefanyika na serikali katika tukio hilo la uzinduzi huku zoezi hilo linaendelea katika ngazi za Halmashauri za Mkoa wa Mara.
Mgeni Rasmi wa shughuli hii alikuwa mh Jumanne Abdallah Sagini ambaye ni Waziri Mdogo wa Katiba na Sheria nchini Tanzania. Katika zoezi hilo Mwanakwetu alitembelea banda la Ofisi ya Taifa ya Mashtaka ambapo kulikuwa na watumishi wasiozidi watano ambapo watumishi watatu wanawake wawili na mwanaume mmoja walikuwepo hapo muda wote.
Kwa hakika wageni waliotembelea banda la Ofisi hii ya umma walipewa maelezo ya kina japokuwa aliyetoa maelezo aliohofia kurekodiwa, akisema wao siyo wasemaji wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka.
Kwa bahati nzuri kipepeprushi cha taasisi hii kulionesha majukumu matano ya Ofisi ya Taifa ya Mashtaka ;
“Kusimamia Uendeshaji wa Mashtaka yote nchini, kusimamia na kuratibu shughuli zote za upepelezi, uchunguzi wa mashauri yote ya jinai, kutoa ushauri wa kisheria kwa mamlaka mbalimbali katika masuala ya jinai, kuendesha na kusimamia mashauri ya utaifishaji wa mali zinazohusiana na uhalifu na kuratibu mashauri yanayohusiana na uhamishaji wa wahalifu kutoka ndani na nje ya nchi na kusaidia mamlaka za ndani na nje katika masuala ya jinai.”
Kwa hakika kazi hizo tano zinazonadiwa na Ofisi ya Mashtaka, kazi hii ya tatu ndiyo kinachofanywa na Waziri Mdogo Sagini hapa mkoani Mara na ndiyo Kampeni hii ya msaada wa Kisheria ya Dkt Samia Suluhu Hassan.
Kwa tukio hili mengi yamezungumzwa na kuelezwa na vyombo vya habari lakini nakuomba msomaji wangu nikupe jambo moja ambalo nina hakika vyombo vingi vya habari hawakuripoti na hili jambo ni agizo la Serikali kwa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka;
“Mimi ningetamani nyinyi watu wa sheria msikwepe sana haya mambo, wakati mwingine hii Migogoro, hata ya ardhi inasababishwa na wataalamu au kuna uonevu unataka kufanya na hata kufanywa dhidi ya wanyonge, mathalani hata kule Njombe Waziri wa Ardhi alipoona hivyo alituma wataalamu wake na mwisho wa siku mtaalamu husika akachukuliwa hatua , sasa angalieni muwashauri vizuri viongozi kwa ngazi ya Mikoa kama vile Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya katika haya mambo.”
Afisa Mashtaka aliyekuwepo alijibu sawa, maana yake anawajibu wa kutekekeza agizo hilo la Serikali kwa eneo lenye mamlaka yake, kama lilivyotolewa Mkoani Mara lakini mhusika anawajibu wa kumjulisha Mkurugenzi wa Mashataka nchini Tanzania Slyvester Mwakilatu ili agizo hilo lizifikie Ofisi zote za Mashtaka kwa Tanzania Bara.
Mwanatakwetu anaipongeza Serikali kwa kauli hii na nia yake ni kuonesha wazi kuwa Serikali Awamu ya Sita imeamua kwa dhati kuutua mzigo wa mateso yao, Watanzania kudai haki zao mahakamani.
Mwanakwetu anampongeza Naibu Waziri Jumanne Sagiji kwa moyo wake huo na hili Mwanakwetu anatambua hata Kitendo cha kuhusisha na kushirikisha Serikali za Mitaa, hii linagonga kengele yenye mlio mzito kuwa la kukusudia kuwafikia Watanzania huko walipo yaani Mitaani na Vijijini.
Mwanakwetu anashauri Ofisi ya Taifa Mashtaka kujitahiadi kuipa nafasi na hadhi sawa kazi ya tatu ya kutoa ushauri kama wanavyoipa nafasi ya kwanza kazi ya kusimama uendeshaji mashataka yote nchini.
Mwanakwetu pia katika Ofisi ya Taifa ya Mashtaka anatambua kuwa kwa sasa kuna mpaka na kizuizi kwa Ofisi ya Mashtaka kushugulikia makosa katika Mahakama ya Kijeshi, lakini Mwanakwetu anaona na kushauri kuwa sasa umefika wakati Ofisi ya Taifa ya mashtaka iweze kupenya hata katika Mahakama ya Kijeshi kikubwa anapopelekwa mtuhumiwa huyu mwanajeshi mwenye tuhuma anakuwa sawa kama alivyo raia
Baada ya yote haya ndiyo Waziri Mdogo Wa Katiba na Sheria wa Tanzania alipozindua kampeni hii.
Mwanakwetu anasema nini siku ya leo?
Kwa hakika Kampeni ya Msaada wa Kisheria ni jambo la msingi na hakuna budi kampeni hii iendelee hili Watanzania hao hao waweze kupata taarifa sahihi katika kujua na kupata haki zao mbalimbali .
Mwanakwetu Upo?
Kumbuika tu,
“Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Dkt Samia Suluhu Hassan Iwe Endelevu.”
Nakutakia siku Njema.
0717649257
Post a Comment