Adeladius Makwega-Musoma MARA.
Kampeni hii inafanyika kwa miaka mitatu kuanzia mwezi Machi, 2023 hadi mwezi Februari, 2026 katika mikoa yote ya Tanzania Bara na Zanzibar.
“Kampeni imejikita katika kutoa elimu ya kisheria kwa wananchi hususani katika masuala ya ukatili wa kijinsia, migogoro ya ardhi, mirathi, usuluhishi wa migogoro kwa njia mbadala, na masuala yahusuyo haki za binadamu kwa ujumla.” Utekelezaji wa kampeni unafanyika kwa kushirikiana na Wizara na Taasisi za Serikali, Asasi za Kiraia, Wanazuoni na Wadau wa Maendeleo.
Shabaha kuu la Kampeni ni kulinda na kukuza upatikanaji wa haki kwa wote kupitia huduma ya msaada wa kisheria nchini.
Katika kufikia lengo hilo, kampeni inaongeza uelewa wa kisheria na haki za binadamu kwa jamii hususani haki za wanawake na watoto; Inatoa huduma ya ushauri wa kisheria na unasihi kwa waathirika na manusura wa ukatili wa kijinsia; kuongeza uelewa kwa wananchi kuhusu elimu ya sheria, masuala ya haki na wajibu na misingi ya utawala bora.
“Matokeo ya muda mrefu wa Kampeni hii ni kuchangia katika kuboresha upatikanaji wa haki kwa watu wasiojiweza, hususan wanawake, watoto na makundi mengine yaliyo katika mazingira hatarishi. Vilevile, itachangia kuimarisha amani na utulivu, kuongeza kipato cha mtu mmoja mmoja na kuleta utengamano wa kisiasa hapa nchini.”
Matokeo ya kati ni kuimarika kwa mfumo wa utoaji wa huduma ya msaada wa kisheria katika ngazi za Serikali Kuu hadi Serikali za Mitaa.
Matokeo ya muda mfupi ni kuongezeka kwa idadi ya watu wanaotoa taarifa za matukio ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto; kupungua kwa idadi ya migogoro na matukio yanayotokana na ukosefu wa uelewa wa sheria; Kuimarika kwa uwajibikaji na uwezo wa taasisi za Serikali na zisizo za kiserikali zinazotoa huduma za msaada wa kisheria.
“Kampeni ilianza kutekelezwa Jijini Dodoma tarehe 28 Mei, 2023 baada ya kuzinduliwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa (Mb) tarehe 27 Mei, 2023 Jijini Dodoma.”
Ratiba ya utekelezaji wa Kampeni hiyo tangu mwaka 2023 katika Mikoa imezingatia usawa wa Kikanda.-
Kwa utaratibu wa sasa, ratiba inalenga kufikia Kata kumi (10) kwa kila Halmashauri na Mitaa/Vijiji vitatu (3) kwa kila Kata. Kuna maeneo ambapo idadi ya Vijiji/Mitaa inapungua kutokana na mazingira nje ya uwezo wa watoa huduma.
makwadeladius@gmail.com
0717649257
Post a Comment