Adeladius Makwega-Musoma MARA
Msomaji wangu nakualika tena katika makala ya katuni siku ya leo, kumbuka haya ni makala ya uchambuzi wa katuni nne ambazo ziteuliwa katika kapu lenye katuni tele , kisha kuelezewa namna zilivyo alafu mwishoni ndipo katuni hizo moja baada ya nyingine uchambuliwa kwa jicho la mtayarishaji wetu. Kuyaanza makala haya Mwanakwetu anaikamata katuni ya kwanza ambayo inaonesha picha kivuli iliyochorwa na Alwataani Masoud Kipanya, hapa kunaonekana mama mmoja anamtoto mgongoni huku akikata mbuga, mama huyu wa Kitanzania akipanda eneo kama la gogoni(Kilimani) na nyuma ya mama huyu mzazi, mama mlezi wa wana, mama analiyefanana na ndege hondohondo nyuma yake kuna ngombe anayekokotwa naye kuelekea huko huko gongoni.
Kumbuka msomaji wnagu neno gogoni maana yake kilima kidogo na neno hili ni maarufu maeneo ya Pwani ya Mkuranga.
“Ukisikia Mzaramo anasema, Yakhe mie nakwenda gogoni, maana yake yupo kondeni(bondeni) sasa anakwea mlima kwenda kilimani.”
Huyu mama katika katuni hii ameshika kamba ya ng’ombe na katika kilima hiki kwa chini kunaonekana anga mithili jua ambalo linazama na haya ni majira ya jioni maana yake huyu mama pengine anarudi kumchunga mnyama huyu , au anatokea kumnunua mnyama huyu na pengine mnyama huyu anamsaidia mama huyu kupata maziwa ya kunywa , yeye mwenyewe, mtoto wake na familia yake pia.
Mwanakwetu anapoitazama katuni hii kwa umakini anabaini kuwa huyu mnyama aliyepewa jina BIMA ina maana kuwa Watanzania hasa wanawake wana BIMA mbalimbali lakini BIMA hizo zimekuwa mzigo kwa jamii. Mchoraji wa katuni yetu alwatani Masoud Kipanya anahimiza wajibu wa serikali kutambua kuwa Bima zote ziwe za afya, ziwe za elimu , ziwe za magari, zisiwe mzigo kwa jamii, maana jamii yenyewe inayo mzigo mingi ikiwamo malezi ya watoto, elimu yao, lishe yao, makazi yao, mavazi yao na kadhalika. Jukumu kubwa la BIMA liwe kuleta taafifu kwa jamii na siyo kuiongozea mzigo jamii husika.
Mwanakwetu sasa anaikamata katuni ya pili ambayo imechorwa na ndugu wa Mwanakwetu King Kinya, hapa kunaonekana jamaa wapo ulingoni, katika mandari ya kwanza kunaonekana jamaa wanapigana huku jamaa mwenye glovusi za kijani akimshambulia vizuri adui yake. Kwa kando jamaa mwenye shati la kijani anashangilia. Katika mandhari ya pili jamaa aliyekuwa akipigwa sasa kapata ahueni naona anampa kipigo vizuri huyu jamaa mwenye glovusi za kijani, huku huyu wa glovusi za kijani anajibu mapigo Upepo huwa unageuka, hauwezi kuvuma upande mmoja tu. Jamaa mwenye shati la kijani bingwa wa kushangilia mapambano yu kando anashangilia jamaa, sasa huyu jamaa anakuwa kama kinyonga kila upande yeye yupo, Mwanakwetu anamwambia huyu jamaa achague upande.
“Katuni hii inaonesha hali ya Siasa za Tanzania mwaka 2025 ambapo suala lile la Uchaguzi wa viongozi CHADEMA baina ya Mbowe na Lissu mpambano wao ulikuwa kivutio pia kwa CCM na hata Watanzania wote, cha kushangazi huyu jamaa mwenye shati la kijani yaani anashangaza yoyote anayepigwa yeye anayo furaha, hii inatoa picha kuwa kwenywe siasa chama tawala chochote kinahitaji vyama pinzani kuwa na changamoto na hiyo ni pona pona ya chama tawala maana Vita ya Nzige Furaha ya Kunguru.”
Mwanakwetu anaikamata kutuni ya tatu iliyochorwa na King Kinya ambapo kunaonekana Kamera saba, hizi ni Kamera Jongefu zimesimamishwa zikiwa kazini, ukitazama kamera hizo vizuri kamera moja ya mkono wa kulia kwako msomaji imeelekezwa Mkutano MKUU WA CCM Taifa na Kamera Sita zineelekezwa Mkuutano Mkuu wa CHADEMA Taifa. Kwa mtazamo wa Mwanakwetu anaona kuwa mchoraji wa katuni hii anatilia maanani kuwa vyombo vya habari vilivutiwa na Mkutano Mkuu wa CHADEMA kuliko Mkutano Mkuu wa CCM. Haya pengine ndiyo mawazo ya mchoraji wa katuni hii ndugu King Kinya. swali la kujiuliza je jambo hilo lina ukweli wowote? Mwanakwetu anasema maneno haya,
“Jambo hilo lina ukweli na kwa hakika CCM ni chama kikubwa kusema kuwa vyombo vya habari kuelekeza nguvu zao vikao vya CHADEMA kumesaidia kuiweka mizani ya habari katika usawa ambalo hilo ni jambo sahihi na ushahidi wa hili ni hata JUKWAA LA WAHARIRI Tanzania , nduguze Mwanakwetu waliipongeza CHADEMA kwa namna ilivyoendesha mkutano wao.”
Katika hili wanasiasa wa Tanzania wawe CCM, CHADEMA,NRA, CHAUSTA, ACT nakadhalika wanapofanya jambo baya au zuri jamii inajifunza, mnajua siasa namna zinavyofanyika hapo jamii ya watoto na vijana inarithishwa ujuzi wa kufanya siasa za kiungwana, siasa za kiistarabu . Kwa maana hiyo hiyo kwa wanasiasa wote weupuke kufanya siasa za kihuni hii inarithisha uhuni kwa kurithiwa na watoto na vijana na uhuni huo kuja kutumika hapo baadaye.
Mwanakwetu sasa anaikamata katuni ya nne na mwisho ambayo imechorwa na King Kinya, katuni hii inaonesha basi linaloendesha barabarani kwa kasi huku mbele ya basi hilo kunaoneka kaburi na juu ya basi lenye kasi kubwa kuna maneno ‘ajali za barabarani' ambazo kwa hakika zinasababisha vifo vingi ulimwenguni.
Katika suala hili Vyombo vya Habari vinapuliza zumari lao kwa athari za ajali na vinakumbusha haya,“Duniani kote, inakadiriwa kuwa watu milioni 1.2 hufa kila mwaka kutokana na ajali za barabarani, huku mamilioni wakipata majeraha makubwa, athari kubwa ya ajali za barabarani ulimwenguni kote mnamo 2024. Kwa mujibu wa taarifa za mwaka 2025, Tanzania ilipata ajali nyingi za barabarani mwaka 2024, takwimu zikionyesha ajali 1,735 zilizosababisha vifo vya watu 1,715 wastani kifo kimoja nukta 01 kwa kila ajali .Kwa majeruhii 2,719,wastani w amajeruhi mmoja nukta 16 kwa kila ajali ndiyo kusema wastani wa kila ajali inakuwa kifo cha binadamu na kila ajali ina kuwa na majruhi wawili.
Huku sababu kuu ikihusishwa na uzembe wa kuendesha gari na makosa ya kibinadamu kama mwendokasi na uzembe wa madereva; data hizi zinatoka Jeshi la Polisi Tanzania. Mambo muhimu kuhusu takwimu za ajali za mwaka 2024 za Tanzania:Jumla ya ajali: 1,735, Waliofariki: 1,715, Majeruhi: 2,719, Sababu kuu: Kuendesha gari bila uangalifu na makosa ya kibinadamu . Kuendesha gari kwa uzembe kunachangia asilimia 73.7 ya ajali za 2024 Kuendesha gari bila kujali kunachangia asilimia 73.7 ya ajali za 2024 na MNAMO Disemba 2024, Tanzania ilishuhudia ongezeko la kuhuzunisha la ajali za barabarani tele na kusababisha vifo vya binadamu.
Kwa hakika nchini Tanzania ajali zinagharimu vifo vywa watu wengi bila kujali nyadhifa aliyonayo , vifo vya mfano ni cha Edward Moringe Sokoine aliyefariki aliyekuwa waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alifariki kwa ajali gari Aprili 12,1984 na kifo kingine cha pili ni cha marehemu Jumaa Jamadil Akukweti (Januari 4, 2007) aliyewahi kuwa Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Akukweti alifariki kutokana na majeraha aliyoyapata katika ajali ya ndege Disemba 16, 2006 huko Mbeya Mjini na Januari 4, 2007 akafariki dunia.
Hali hii si ya Tanzania tu hata ulimwenguni ajali zinatokea , kifo kinachokumbwa na wengi kwa ajali ni cha Princess Diana ambaye alikuwa mke wa kwanza wa Mfalme Charles III wa Uingereza.Swali ambalo Mwanakwetu anakuomba msomaji wake alijibu leo hii je ajali ya Princess Diana iliyotokea agosti 31, 1997 ilikuwaje?
Asubuhi ya Jumapili, Agosti 31, 1997, Princess Diana alikufa katika ajali ya gari kwenye handaki ya Pont de l'Alma huko Paris, Ufaransa. Katika gari hilo Princess Diana alikuwa pamoja na mpenzi wake , Dodi Al Fayed; Henri Paul, dereva wa gari hilo; na Trevor Rees-Jones, mlinzi wake. Rees-Jones mlinzi wa Diana ndiye pekee aliyenusurika kifo ajalini.Diana na Dodi walikuwa wamekaa pamoja kwa siku 10 kwenye boti ya Mohamed Al Fayed, Jonikal, kisha wakasafiri kwa ndege kutoka Sardinia hadi Paris mnamo Agosti 30, 1997. Alikuwa arudi London mnamo Agosti 31, 1997, ambapo wanawe, Prince William na Prince Harry, walikuwa wanarudi kutoka Balmoral Castle.Wawili hao walifika Paris saa 3 usiku, na wakatoka uwanja wa ndege hadi Villa Windsor, nyumba ya zamani ya Duke na Duchess ya Windsor ambayo Mohammed Al Fayed alinunua. Kutoka hapo, walikwenda Ritz Paris, inayomilikiwa na familia ya Fayed. Wakati huu,
Princess Diana alizungumza na wanawe kwenye simu. Akiwa Ritz, Dodi alitembelea duka la vito la Repossi huko Place Vendome. Mapema jioni, waliondoka Ritz hadi kwenye nyumba ya Dodi kwenye Rue Arsène Houssaye.Wenzi hao walipanga kula chakula cha jioni huko Chez Benoit saa 3.39 ya usiku, lakini kwa sababu ya umakini wa paparazzi, waliishia tena kwenye Ritz. Walijaribu kwanza kula kwenye mgahawa wa L'Espadon, lakini dakika 10 baadaye, walikwenda kula kwa faragha katika Imperial Suite. Kulingana na Shirika la Habari la Associated Press, ‘Diana aripotiwa kuagiza appetizer ya uyoga na parachichi.’Muda mfupi baada ya saa sita usiku, waliamua kuondoka hotelini kwenda kwenye nyumba ya Dodi.Henri Paul, mkuu wa usalama wa Ritz, aliwaendesha kwa gari la Mercedes S280 ambaye kwa matokeo ya uchunguzi baadaye yalifichua kwamba Paul alikuwa amelewa. Waliondoka saa 6:20 usiku kupitia lango la nyuma la hoteli. Ingawa walikuwa wamejaribu kutumia gari la kudanganya huko Ritz, paparazi walishituka na kuanza kuwafuatili nyuma yao. Ndani ya gari, si Princess Diana wala Dodi walikuwa wamefunga mikanda; Rees-Jones, aliyeketi kwenye kiti cha abiria, aliripotiwa kuvaa mkanda peke yake.Saa 12:25 ya usiku gari liliingia kwenye handaki ya Pont de l'Alma kwa mwendo wa kasi wa hatari.
Kama Asossiated Press (AP) inavyoripoti, ‘Sekunde baada ya gari kuingia kwenye handaki katika njia ya kushoto ya kuelekea magharibi gari hilo likagonga nguzo ya 13 ya zege inayogawanya handaki, kuviringika na kurudi kwenye ukuta wa kulia. Kisha kuzunguka. gari likasimama, kutazama mashariki mwelekeo lilikotokaWakati huo huo ajali hiyo ilipotokea, daktari Mfaransa, Dk. Frederic Mailliez, alikuwa akiendesha gari kwenye mtaro huo na kushuhudia ajali hiyo, harakaharaka akakimbilia eneo la tukio.‘Nilitembea kuelekea kwenye mabaki. Nilifungua mlango, na nikatazama ndani,’ alikumbuka miaka mingi baadaye. Aliona ‘watu wanne, wawili kati yao walikuwa wamekufa, hakuna majibu, hawakupumua, na wengine wawili, upande wa kulia, walikuwa hai lakini maututi. Abiria wa mbele alikuwa akipiga kelele, alikuwa akipumua. Dakika chache abiria wa kike, yule mwanamke mchanga, alikuwa amepiga magoti kwenye sakafu ya Mercedes, alikuwa na shida ya kupumua.Alikimbilia kwenye gari lake, akapiga simu za dharura, na kuchukua begi la kupumua.
‘Alipoteza fahamu. Shukrani kwa mfuko wangu wa kupumua... alipata nguvu kidogo zaidi, lakini hakuweza kusema chochote.’Huyu ni Princess Diana alipelekwa katika Hospitalini na Saa 6:27 , Jeshi la Zimamoto na Uokozi walipokea simu ya kuomba msaada, na polisi walifika saa 6:40 Mashahidi baadaye walitoa ushahidi kwamba paparazi waliendelea kuchukua picha, na wapiga picha saba waliwekwa chini ya ulinzi wa polisi.Sajenti Xavier Gourmelon, kutoka zima moto, ambaye alikuwa kwenye eneo la tukio, alisema maneno ya mwisho ya Princess Diana yalikuwa ‘Mungu wangu, nini kimetokea?’Wakati Princess Diana alitolewa kwenye mabaki ya gari, aliingia kwenye mshtuko wa moyo. Washiriki wa kwanza walimfanyia CPR, na kumpeleka hospitalini. Karibu saa 8 ya usiku .Princess Diana alitangazwa kuwa amekufa karibu saa 4 asubuhi huko Paris mnamo Agosti 31, 1997; alikuwa na umri wa miaka 36. Saa 6 asubuhi, Dk. Alain Pavie, mkuu wa idara ya magonjwa ya moyo katika Hospitali ya Pitié-Salpêtrière, alifanya mkutano na waandishi wa habari, akitangaza kifo cha Binti wa Kike wa Wales. Balozi wa Uingereza nchini Ufaransa, Michael Jay, alikuwepo. Alisema, ‘Kifo cha Binti wa Mfalme wa Wales kinatujaza sote na mshtuko na huzuni kubwa.’ Baadaye siku hiyo, Prince Charles alipanda ndege hadi Paris na dada wa Diana, Lady Sarah ili kuuchukua mwili wa Princess Diana kabla ya kuwa mke wa Prince Charles, Princess Charles alikuwa na mahusia ya kimapenzi Lady Sara dada wa Princess Diana ambaye walikwenda naye kuchukua mwili huku Ufaransa. Mazishi ya Princess Diana yalifanyika Septemba 6, 1997.
Mara baada ya kifo hicho kilichosababisha na ajali Malikia wa Uingereza Elizabeth wakati huo alitoka hadharani na kusema maneno haya,
“Tangu Jumapili iliyopita, habari za kutisha tumeona kote Uingereza na ulimwenguni kote, maneno mengi ya kusikitishwa na kifo cha Diana, sote tumekuwa tukijaribu katika maisha yetu. njia tofauti za kukabiliana nalo si rahisi kueleza hisia ya kumpoteza kwani mshituko wa awali ni mara nyingi huwa na mchanganyiko wa hisia, zingine kutokuamini kutokuelewa na hasira na pia wasiwasi.Kwa tuliobaki sote tumehisi hisia hizo katika siku chache zilizopita, kwa hiyo ninachowaomba sasa kama malkia wenu na kama bibi nasema kutoka moyoni mwangu kwanza
Tulipe heshima ya maisha ya Princes Diana.
Diana mwenyewe alikuwa mwanadamu wa kipekee na mwenye vipawa katika nyakati nzuri na mbaya, kote huko hakuwahi kupoteza uwezo wake wa kutabasamu na kucheka na wa kuwatia moyo wengine, kwa uchangamfu na fadhili zake tunastahili kumuheshimu kwa nguvu na kujitolea kwake kwa wengine na hasa kwa kujitolea kwake kwa watu wengine sasa tumekuwa tukijaribu kuwasaidia William na Harry kuja kukubaliana na hasara kubwa ambayo wao na sisi wengine tumepatwa na hakuna mtu ambaye alijua kwamba Diana angesahau mamilioni yake ya watu wengine ambao hawakuwahi kukutana naye lakini waliona kuwa wanamjua watamkumbuka.
mimi naamini kuna mambo ya kujifunza kutoka kwa maisha yake na kutokana na mwitikio wa ajabu na wa kusisimua wa kifo chake ninashiriki katika azimio lake la kumuenzi.
kumbukumbu hii pia ni fursa kwangu kwa niaba ya familia yangu na hasaPrince Charles (King)na William na Harry kuwashukuru ninyi nyote ambao mmeleta maua, ujumbe na kutoa heshima zenu kwa njia nyingi.
Natoa pole kwa familia ya Diana na familia za waliokufa pamoja naye, najua pia watapata nguvu kutokana na kile kilichotokea tangu. wikendi iliyopita huku wakitafuta kuponya huzuni yao na kisha kukabiliana na wakati ujao bila wapendwa wao, natumai sote tunajumuika kuelezea majonzi yetu kwa kuondokewa na Princess Diana na shukrani kwa maisha yake mafupi sana ni nafasi ya kuuonyesha ulimwengu mzima Umoja wa Uingereza kwa majonzi na heshima waliofariki wapumzike kwa amani. Princess Diana alijitahidi kila mmoja wetu amshukuru Mungu kwani alikuwa mtu aliyefanya wengi
Wawe na furaha.”
Katika kisa hiki cha ajali ya Prncess Diana inaaminika kuwa mpenzi wa Princes Diana Dodi Alfayed alikaa na Princess Diana siku kadhaa kwa mficho nia ikiwa kupata ujauzito na kuzaa na huyu Dodi mtoto wa tajiri wa Kiarbu hapo Uingereza. Princess Diana alijisahua kuwa aliolewa na familia ya kifalme ambayo inamfahamu vizuri hata hali ya afya yake mizunguko ya mwili kwa hiyo ilibainika kuwa ziara hiyo ilikuwa na hila kwa aufalme wa
Uingereza.Swali ambalo lilikuwepo kama kweli Princess Diana angezaa na Dodi hivyo Mfalme Uingereza angekuwa na udugu wa damu na Waarabu ndiyo kusema ajali hii ilikatisha shabaha hiyo ya Princess Diana na Dodi Al Fayedi na ndiyo maana wengi wanaamini ajali hii ilikuwa na mkono wa mtu,KILA AJALI INA MKONO WA MTU..
Mwanakwetu upo?
Kumbuka siku ya leo Mwanakwetu alikuwa na katuni nne, ile ya BIMA na Mama Mkokota Ng’ombe mgongoni, ile ya CCM kushangili pambano la CHADEMA n ktuni ya tatu ni ile ya Kamera saba za wahanahari wa Tanzania na katuni ya mwisho ni hii ya ajali za barabrani iliyomuibua kifo cha Princes Diana huko Ufaransa.
Kumbuka
“KILA AJALI INA MKONO WA MTU.”
Nakutakia Siku Njema.
0717649257
Princess Diana na Dada yake Lady Sara.
Princess Diana &Dodi picha tatu juu.
King Charles na mkewe Queen Camila
Post a Comment