Adeladius Makwega-Musoma MARA
Mkuu wa Mkoa wa Mara, Kanali Evans Alfred Mtambi amesema kuwa suala la Lishe Siyo Suala la Kujivutavuta na ndiyo maana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan Amejifunga Kibwebwe katika maboresho ya lishe ya kila Mtanzania.
Haya yamesemwa na Januari 24, 2025 na Kanali Mtambi katika kikao cha Lishe Mkoa Mara ambacho kilihudhuria na viongozi wa lishe tangu ngazi ya Halmashauri , Wakurugenzi Watendaji, Makatibu Tawala na Wakuu wa Wilaya wote zote.
“Nawapongeza nyoote kwa kulisisimamia hili kwa nguvu zote, pale ambapo kuna changamoto tuwasiliane huku sheria ndogo zitumike.
Natambua awali hali ya Lishe Mkoa wa Mara ilikuwa Dhohofu li Hali tulikuwa na asilimia 18 tu lakini tukafikisha asilimia 95, binafsi sitomvumilia yoyote atakayesababisha asilimia hii ishuke.
Eneo lenye shida tushirikiane tuone tunafanyaje. nawapongeza Tarime Mji kwa kufanya kazi hii vizuri tujifunze kwao. Viongozi wezangu tumieni ubunifu katika hili.”
Kanali Mtambi akiyasema haya alipigili msumari wake katika maagizo kadhaa ya kikao hiki;
“Kila halmashauri ihakikishe katika bajeti ya fedha wanayoipanga kwa mwaka wa fedha 2025/2026 bajeti zote za lishe zizingatie bajeti ya sasa ili bajeti ya lishe isishuke chini, utoaji wa fedha za lishe zilizopangwa zitekeleze zisisuesue, kila halmashauri itenge shilingi 1000/= kwa kila mwanafunzi na watumishi watakaozembea katika suala la lishe wachuliwe hatua.”
Mkuu wa Mkoa wa Mara alikwenda mbali zaidi katika kusisitiz suala la Lishe.
“Nawaagiza Wakuu wa Wilaya zote za Mkoa wa Mara katika maeneo yote simamieni utekelezaji wa kupatikana Chakula cha Mchana Shuleni.”
Kwa upande wake Katibu Tawala Mkoa wa Mara ndugu Gerald Kusaya awali akimkaribisha Mkuu wa Mkoa alisema kuwa kikao cha tathimini ya utekelezaji kinachofanyika Januari 24, 2025 ni cha tathimini kwa kipindi cha Julai hadi Disemba 2024.
Jambo moja zuri na la kukumbuka katika kikao hiki ambalo mwandishi wa ripoti hii atalikumbuka milele ni kauli hii ya Mkuu wa Mkoa wa Mara Kanali Evans Alfred Mtambi;
“Hoja siyo kusimamishwa mbele ya umma kudhalilishwa kuwa haukufanya vizuri katika lishe au kuchukuliwa hatua kuwa hakufanya vizuri katika lishe, bali jambo la msingi ambalo mimi linaniuma/kunikera kama wewe umepewa jukumu la kusimamia suala la lishe katika eneo lako shabaha uboreshe afya za binadamu wenzako alafu umeshindwa, hilo ni jambo mbaya na silipendi lazima tusimamie jamii yetu ya Mkoa wa Mara iwe ma Lishe bora.”
Wakati haya yakiendelea katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara, hali ya hewa ya Mji wa Musoma ni jua la kadili.
0717649257
Post a Comment