Adeladius Makwega-Musoma MARA
Mkuu wa Mkoa wa Mara Kanali Evans Alfred Mtambi, amefanya kikao chake cha kwanza kuugubua mwaka mpya wa 2025 huku Akiipiga Mbiu ya Mgambo ya Pongezi tele kwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kupitishwa kwa kauli moja na CCM kugombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa Uchaguzi Mkuu wa 2025 nchini Tanzania.
“Nampongeza mno Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuaminiwa na chama chake, kwani hakuna ubishi, Mh. Rais Dkt Samia amejitahidi kutoa fursa mbalimbali kwa kila Mtanzania ili sote tuishi maisha bora na ni wajibu wa kila Mtanzania kumuunga mkoni.”
Mkuu wa Mkoa wa Mara alikwenda mbali Januari 22, 2025 na kumpongeza pia Dkt Hussein Ali Mwinyi, Rais wa Zanzibar na yeye kwa kupitisha kwa kauli moja kuwa mgombea wa CCM kwa Urais wa Zanzibar akissema kuwa Dkt Samia Suluhu Hassan sasa atagombea urai huu akiwa na mgombea mwenza Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi
Akizungumza akiwa katika kikao hiki maalumu cha wadau wa afya, kilimo na mifugo Kanali Mtambi alitoa nafasi ya Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mara na wataalamu wake kutoa maelezo ya kina juu ya magonjwa hatari kwa afya kwa wakati huu tulio nao sasa huku ikisisitizwa kinga ni bora kuliko tiba.
0717649257
Post a Comment