Adeladius Makwega-Musoma MARA
“Baadhi ya akinamama wajawazito wakikaribia kujifungua wanatumia miti shamba kuharakisha uchungu na wengine wakishatumia inaleta madhara makubwa mathalani tunashuhudia wanafikishwa hospitali wakiwa wamechanika, hilo ni hatari wakati wa kujifungua.”
Haya yamesemwa na Bi Leah Daniel ambaye ni Mratibu wa Huduma ya Afya ya Mama na Mtoto Mkoa wa Mara katika Kikao cha Thathimini ya Utekelezaji wa Mkataba wa Lishe kwa Kipindi cha Julai hadi Disemba 2024 kilichofanyika Januari 24, 2025 mkoani Mara.
“Wakunga wa Jadi ni muhimu sana na wametoa mchango mkubwa kwa miaka mingi, lakini kwa utaratibu wa sasa bado tunawahitaji lakini ni vizuri watumike kuwasindikiza mama mjamzito wakati wanakwenda kujifungua hospitalini, hilo linasitizwa kulinda afya ya mama na mtoto kutokana na hali ya magonjwa ya binadamu nyakati hizi.”
Kwa upande wao watumishi wa afya katika kikao hichi walisema kuwa ili mkulinda afya ya mama na mtoto ni vizuri changamoto za watumishi wa afya ziambatane na ripoti za afya ya mama na mtoto ili mambo haya yaende pamoja.
Akizungumza katika kikao hicho kuitimisha, Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara ndugu Geofrey Kusaya alisema kuwa suala la afya ya mama na mtoto lazima, lazima., lazima lizingatiwe na kila mmoja wetu, awe mtumishi wa afya na jamiii nzima, shabaha ni kuondoa vifo vya mama na mtoto.
“Katika kulitatua hili Mkuu wa Mkoa wa Mara Kanali Alfred Mtambi ameniagiza kila kifo cha mama au mtoto lazima sababu yake ifahamike ili kijulikane cha kufanya huku akiagiza pia viongozi wa dini washirikishwe katika vikao vyote vya afya vya mama na mtoto ngazi zote. Watumishi timizeni wajibu wenu maana Tusifanyie Majaribio ya Uhai wa Binadamu .”
Kikao hiki kilimalizika saa 6.na dakika 41 ya mchana huku hali ya hewa ya Musoma Mjini bado ni jua la kadili.
0717649257
Post a Comment