Adeladius Makwega Lushoto&Musoma
Bibi Anna Mkapa, mjane wa Rais wa Awamu ya Tatu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ametembea kaburi la Askofu Mstaafu wa Dayosisi ya Kaskazini Mashariki ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania(KKKT) lililopo kando la Kanisa Kuu la Dayosisi hiyo Lushoto Mkoani Tanga, Januari 4, 2025 na kupokelewa na Askofu wa Dayosisi hii Mchungaji Dkt. Msafiri Mbilu.
Akiwa kando ya kaburi hilo Bibi Anna Mkapa na watu waliombatana nao walishiriki sala fupi ambayo iliongozwa na mchungaji Karata kisha Bibi Anna Mkapa kuwasha mshumaa kaburini hapo ambapo Baba Askofu Joseph Jali alifariki Agosti 14, 2024 na kuzikiwa Agosti 21, 2024 naye Bibi Anna Mkapa wakati wa msiba huo akishiriki ibada zote za mazishi ya kiongozi huyu wa kiroho.
Akizungumza katika shughuli hii fupi Bibi Anna Mkapa alisema,
“Mama Sara Jali nimekuja kukusalimia, pia nimefika nyumbani kwangu nimeangalia shamba langu, linaendelea vizuri.”
Akifunga shughuli hii ndogo ya kiroho Askofu wa Dayosisi ya Kaskazini Mashariki ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Mchungaji Dkt .Msafiri Mbilu alirejea maneno haya.
“Uso wangu Utakwenda pamoja nawe, nami nitakupa raha.”
Yakinukuliwa kutoka kitabu cha Kutoka.
Wakati Rais Mstaafu Benjamin Mkapa akiwa hai mwandishi wa hii ripoti alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto leo anayakumbuka haya,
“Mzee Mkapa alikuwa miongoni mwa wakulima wa mboga mboga aina mbali kama vile kabichi, viazi, karoti, pilipili hoho na brokolini. Kila wakati wa kuvuna mboga mboga hizo, kazi hiyo ilisimamiwa na Karimu Mahanyu aliyekuwa ni Diwani wa Kata ya Lukozi (CCM) sasa ni marehemu, wakishavuna mboga mboga hizo wanazifunga vizuri kisha aliitwa Mtendaji wa Kijiji kuja kukatisha ushuru wa mazao yote ya mboga mboga zilizovunwa siku hiyo na kukatishiwa ushuru wa Mashine ya Elektroniki, huku mazao ya mboga mboga ndiyo chanzo kikubwa cha mapato cha Wilaya ya Lushoto ambayo yanasafrisha hadi nje ya nchi.”
Mwandishi wa ripoti anaongeza kuwa,
“Nilikuwa nayasubiri malori hayo Kituo Cha Ukaguzi cha Mapato Nyasa na hata nilipokaguwa moja baada ya nyingine, malori hayo yote kutoka kwa Benjamin Mkapa yalilipiwa kwa haki ushuru stahiki wa mamlaka hii na hakuna lori hata moja lililodiriki kukwepa kulipa ushuru huo halali hata siku moja.”
Wakati hayo yakiendelea wilayani Lushoto hali ya hewa za Mji huo Mkongwe ni jua na joto la kadili.
0717649257
Post a Comment