AAAH MAMA NA MIMI NIKUMBATIE

 


Adeladius Makwega Musoma MARA.

“Mwanakwetu kwa upande baba anazaliwa katika ukoo unafahamika kama akina Kazimbaya, huku jina  Makwega lilikuwa ni jina la utani na miongoni mwa koo zilizotoka Sali kuhamia Ikangao Ilonga Ulanga enzi hizo kusaka ardhi yenye rutuba, katika hilo pia ni miongoni mwa koo za awali kuingia Ukristo katika Parokia ya Luhombero ambayo wakati huo ilikuwa Jimbo Katoliki la Dar es Salaam. Hata akina Makwega wa awali walipata elimu kidogo kwa msaada wao na ujirani wa Kanisa Katoliki.

Mwanakwetu anazaliwa na mtoto Fidelis Peter Kazimbaya Makwega aitwaye Francis Fidelis Peter Kazimbaya Makwega. Kwa hakika, baba na shangazi wa Mwanakwetu walizaliwa Mafia, Mbagala na pia Morogoro na wengi kukulia Mafia na Mbagala na Ikangao huko Morogoro.”

Mwanakwetu anazo simulizi nyingi za Wakristo wa kwanza wa Mafia na Mbagala huku wakikutana na changamoto tele za wakati huo katika miji ya Pwani ya Bahari ya Hindi. Vipo visa vingi vya kufunga safari kwa Askofu Edgari Maranta wa Jimbo Katoliki la Dar es Salaam na baadaye kwa Kadinali Laurean Rugambwa kulalamikia namna ndugu hao walivyoshindwa kuabudu kutokana na mazingira ya wakati huo maisha ya kiimani yalivyokuwa magumu. Siyo kwamba kuna mtu alipoteza uhai wake kimwili bali watu walisumbuliwa katika kuufikia uhai wao kiroho

“Zamani ukiwa  na msiba iwe Mkristo au Muisilamu, vyombo vyote vya kulia chakula vilikuwa vinahifadhiwa misikitini kwa hiyo msiba ukitokea mnafuata vyombo hivyo mnapika kisha mnavisafisha vizuri na kuvirejesha msikitini Mungu bahati kuazima huko kulikuwa bure hakukuwa na malipo yoyote.”

Msomaji wangu haya yanayoandikwa tambua kuwa Mwanakwetu anayafahamu vizuri iwe kwa ksimuliwa na ameyaishi kwa kipindi kirefu, sasa yanabaki kama kumbukumbu tu. Kwa desturi ya maisha ya Pwani ya Bahari ya Hindi, Muisilamu akiwa na jambo linamtatiza anamfuata Ustadh au sheikh anayeaminika katika eneo hilo kumuuliza, hivi jambo hili nikifanya je sheria ya dini inaruhusu? Msomi. Sheikh au Ustadh anayeulizwa anatoa fatua katika hilo jambo.

“Jambo hili siyo sahihi lakini litakuwa sahihi kama utafanya kwa namna ya kadhaa kadhaa wa kadhaa.Hili ni kama vile zile safari za kwa akina Edagari Maranta na kwa Kadinali Laurean Rugambwa”

Ninachoweza kusema ni kuwa kama jamii haikuamini, haiwei kuja kwako kukwambia chochote, hadi impate mtu inayomuamini kwa suala husika, lakini haya ni mambo ya wakati huo ya sasa hivi Mwanakwetu hayafahamu.


 

Swali ambalo nimekuwa ninajiuliza ni hii ziara ya hivi karibuni za Rais Samia Suluhu Hassan akiwa Mkoani Tanga ameonekana Rais wa Jamhuri ya Muungano akimkumbatia mh Januari Makamba(mb) Bumbuli.

“Jambo hilo limenipa mshituko mkubwa, nakujiuliza sana je wanazuoni wa dini ya Kiisilamu suala hili lilikuwa sahihi? Je jambo hili liliandaliwa mapema na kufanyiwa tathmini ya imani ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania? Je kulingana na imani ya dini ya Kiisilamu ni Sahihi Mwanamke kumkumbatia hadharani mwanaume asiye na nasaba/ujirani naye? Je Ikulu ya Magogoni kwa sasa haina mshauri wa Rais wa masuala ya dini yake?”

Inawezekana kufanya hivyo siyo kosa kwa mujibu wa dini la Kiisalamu na inawezekana ikawa vinginevyo..

Je kama ni kosa kufanya hivyo, hukumu ya dini ya Kiisilamu kukumbatiana na mwanamke na mwanaume asiye ndugu wa damu ni ipi?

Katika pekuapekua za Mwanakwetu alikutana na na swali hili .

“Mimi ni mwanamke kutoka Marekani na ninaishi Ulaya, nina ndugu zangu wengi. Tangu nilipoingia Uislamu ninapata ugumu wa kuwaelezea watoto wa mjomba wangu kuwa siruhusiwi kukumbatiana nao. Ninatarajia mnifahamishe hukumu ya sheria ya dini katika suala hili.”

Hilo swali linaloulizwa na majibu yake yalikuwa  haya;

“ Nalijibu swali hili kuwa hakuna kikwazo chochote katika kuamkia na kupeana mikono kwa ajili ya kukaribishana tu, kama hakuna matamanio na fitina.

Ushahidi wa hili ni Hadithi iliyopokelewa kutoka kwa Al-Bukhari kutoka kwa Anas Ibn Malik R.A. alisema kuwa:

‘Mjakazi mmoja miongoni mwa wajakazi wa Madinah alikuwa akimchukua Mtume kwa mkono wake mpaka anapomfikisha mahala anapotaka.’

Katika mapokezi mengine kutoka kwa Imam Ahmad, kutoka kwa Anas pia alisema: ‘Mjakazi mmoja kati ya vijakazi wa Madinah alikuwa akimchukuwa Mtume kwa mkono wake naye Mtume hakuwa akiutoa mkono wake mpaka wanapofika mahala anapopataka.’ Mtazamo huu ni kwa mujibu wa walivyosema Wanavyuoni wa siku hizi. Imepokelewa kutoka kwa Imam Ahmad kuwa inachukiza sana kupeana mikono kati ya wanaume na wanawake.’

Al-Bahwati aliusema mtazamo huu katika kitabu cha Kashaf Al-Qinaa [2/154, 155, Darul Kutub Al-Ilmiyah]: Imam Ahmad alisema katika mapokezi ya Ibn Mansur.’

‘Inachukiza kupeana mikono kati ya wanaume na wanawake.’

Wengi wa Wanavyuoni – isiopokuwa Wanavyuoni wa madhehebu ya Imam Shafi – hawaruhusu kupeana mikono kati ya wavulana(wanaume) na wasichana(wanawake), ambapo Wanavyuoni wa madhehebu ya Imam Shafi wameruhusu hivyo kwa masharti mawili: kutokuwepo kwa fitina, na kuwepo kwa kikwazo. Rejea: Tabiin Al-Haqaiq 6/18 Darul Kitab Al-Islami, Hashiyatul Sawi ala Sharhul Saghiir 4/760, Darul Maarif, Nihayatul Mihtaj 6/191, 192, Darul Fikr.

Kama kuna haja ya kukaa wanaume na wanawake pamoja, na hakuna fitina baina yao, basi hakuna ubaya wowote wa kupeana mikono kati yao kama kuna dharura; kama vile ya aliyerudi kutoka safarini na kama jamaa akimzuru mmoja wa jamaa zake, nk. Mola wetu ametukataza tusikaribie mambo machafu kama alivyosema: ‘Wala msikaribie mambo machafu, yanayoonekana, na yanayofichikana.-AL ANAAM: 151’

Miongoni mwa kukaribia mambo hayo ni kufanya mambo yanayoyapelekea kuyafikia na hakuna shaka kuwa kukumbatiana kwa mwanamke na wanaume wasio maharimu (ndugu) zake ni kutokana na sababu za kiuasi zinazopelekea mambo machafu. Ama kuhusu kukumbatiana na kubusu kati ya mwanamke na mwanaume wasio (ndugu) maharimu – kama watoto wa mjomba – basi ni haramu kwa mujibu wa maafikiano ya Wanavyuoni, kwa sababu hao sio (ndugu) maharimu kwa mwanamke, naye siye maharimu kwao. ‘Kumkumbatia inadhaniwa kuwa - kunasababisha matamanio na ufisadi na msingi wa kifiqhi unasema kuwa kinachodhaniwa ni sawa na kilicho kweli na kama ukiwajulisha kuwa sababu za kukataza vitendo hivi ni za kidini, basi pengine wataheshimu hivyo na watajizuia na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni mjuzi zaidi ya wote. Haya yote yanapatikana kupitia ttps://www.dar-alifta.org/sw/fatwa/details/14114/hukumu-ya-kukumbatiana-kwa-mwanamke-na-mwanaume-wasio-ndugu-wa-damu.”

Mwanakwetu anasema nini siku ya leo?


 

Viongozi wa dini wa sasa wakumbuke kufungua milango na wasikilize shida za jamii zetu kama wlaivyokuwa akina Edgari Maranta, jamii ya sasa ina shida nyingi mkimuachie Padri Charles Kitima peke yake atapambana na kisha atachoka. Kazi hii ifanywe na sisi sote.

“Mathalani saula la watu wasiojulikana kanisa linaweza kujiuluza tangu ngazi ya jumuiya, mtaa, kigagoni, usharika/ parokia vikareti hadi jimbo. Jamii inauliuza ndugu yenu alipoteaje je mnamuhisi na je majibu katika vyombo vya ulinzi yalikuwaje?

Je waliyopotea ni wa imani yenu wangapi , wa imani nyingine wangapi na wapagani wangapi?Je kama jina la mtu linatajwa, kwa kushiriki moja kwa moja au kwa kutotimiza wajibu , je anafanywaje kwa miongozi ya kidini?Dini inatoa mwongozo upi?.”.

Mwisho ni juu swali na majibu yake lililojenga makala haya,

“Mimi ni mwanamke kutoka Marekani na ninaishi Ulaya, nina ndugu zangu wengi. Tangu nilipoingia Uislamu ninapata ugumu wa kuwaelezea watoto wa mjomba wangu kuwa siruhusiwi kukumbatiana nao. Ninatarajia mnifahamishe hukumu ya sheria ya dini katika suala hili.”

Miongoni mwa maelezo ya majibu ya swali hilo ni haya;

“Kumkumbatia inadhaniwa kuwa kunasababisha matamanio na ufisadi na msingi wa kifiqhi unasema kuwa kinachodhaniwa ni sawa na kilicho kweli. ”

Mwanakwetu kama Mkristo hana mamlaka kusema kuwa Dkt Samia Suluhu Hassan alikosea na kupatia kwa kumkumbatia hadharani mh Januari Makamba lakini Mwanakwetu anayo haki moja ya kumuonea gere mh JanuariaMakamba kwa kukumbatiwa hadharani na y eye kufurahishwa sana na kitendo hicho cha Dkt Samia Suluhu Hassan kumkumbatia hadharani.

Mwanakwetu anamuomba Rais Samia kwa heshima zote akisema aaah mama basi na mimi nikumbatie......................... hata kwa mbali................................ huku nilipo kwa kuhakikisha kunakuwepo na usalama wa raia dhidi ya watu wasiojulikana na hawa wote wanaotuhumiwa wakamatwe na wapelekwe mahakamani.

“Aah jamani mama basi na mimi nikumbatie.”

Mwanakwetu upo?


 

Kumbuka

“Aaah Jamani Mama na Mimi Nikumbatie.”

Nakutakia siku Njema

makwadealadaius@gmail.com

0717649257


































 

 

 

0/Post a Comment/Comments