Adeladius Makwega-Musoma MARA
Tulipokuwa wadogo nyumbani kwetu Mbagala kulikuwa na mzee mmoja wa Kichaga aliyefahamika kama Benson Njiu maarufu kama Mzee Ben, kwa wale wageni wa Mbagala na wenyeji, nyumba ya mzee huyu ipo pale kilipo Kituo cha Mabasi cha Mbagala Mpili(Mbagala Sabasaba) kama unakwenda Mbagala ukishuka uwe kama unarudi ulipotoka, nyumba ya tatu hapo ndipo ilipo nyumba ya mzee wangu huyu.
“Benson Njiu alizaliwa huko Moshi–Kilimanjaro na kuhamia Mbagala, hapa alifunga ndoa na shangazi yake Mwanakwetu bibi mmoja wa Kimatumbi-Binti Mkundi, tangu enzi hizo nyumba yake ilikuwa na duka lenye bidhaa kadhaa na kama unakwenda kununua kitu hapo ulitakiwa kwenda kwa nidhamu kinyume chake bidhaa usingeipata, watu wa Mbagala walisema huyu Mzee Ben mkoloni sana kosa tulilofanya kwa Mzee Beni kumuozesha dada yetu.”
Mwanakwetu alizifaidi mno tabia za ndugu huyu kwanza alioa shangazi yake pia alikuwa akisali naye pamoja katika Kanisa la Mtakatifu Antony wa Padua hapo Mbagala Misheni, hilo ni kanisa moja dogo, zuri na kongwe. Kwa umri wa kanisa hilo sasa ni karibu mara mbili ya umri wa Mwanakwetu.
Uzuri wa kanisa hili ni wa mambo mengi, lina mabechi mazuri na imara ya mti wa Mninga na Mvule ya enzi hizo na mabechi hayo tangu yaingizwe humo hayajawahi kutolewa zaidi ya kupigwa msasa na polishi humo humo, huku madirisha ya kanisa hilo ni yale ya kupanga vipande vya mbao na huwa vinaangukaanguka nao ukarabati ukifanyiwa kila mara. Ndani ya kanisa hilo kuna kengele moja kubwa ambayo ikipigwa Mbagala nzima Mtoni Nizama inasikika huku iliwahi kuwarusha juu akina Mwanakwetu enzi hizo kutokana na uzito wake. Altare ya kanisa hilo mkono wa kulia na kushoto kuna picha ya Mtakatifu Antony wa Padua na ile ya Bikira Maria yenye taji la nyota kama inayonadaiwa na Ufunuo wa Yohane 12, 1-6.
“Ndipo ishara kuu ikaonekana mbinguni: palikuwa na mwanamke aliyevikwa jua, na mwezi ulikuwa chini ya miguu yake, na taji ya nyota kumi na mbili ilikuwa juu ya kichwa chake. Alikuwa mjam zito,akilia kwa uchungu kwa kuwa alikuwa anakaribia kujifungua. Kisha ishara nyingine ikaonekana mbinguni: likaonekana joka kubwa jekundu lenye vichwa saba na pembe kumi na taji saba katika vichwa vyake. Mkia wake ulifagia theluthi moja ya nyota zote angani na kuziangusha ardhini. Joka hili likasimama mbele ya yule mwanamke aliyekuwa karibu kujifungua, likiwa tayari kumla huyo mtoto mara tu atakapozaliwa. Mama huyo akajifungua mtoto wa kiume, ambaye atayatawala mataifa yote kwa fimbo ya chuma. Lakini mtoto huyo akanyakuliwa na kupelekwa kwa Mungu, kwenye kiti chake cha enzi. Yule mwanamke akakimbilia nyikani, ambako Mungu alik wisha kumtengenezea mahali pa kumtunza kwa muda wa siku elfu moja mia mbili na sitini.”
Picha hizo mbili zote hizo ni za enzi hizo, picha za kale msomaji wnagu Kanisa letu la Mtakatifu Antony wa Padua zuri, Mwanakwetu anaamini Jimbo Kuu la Dar eS Salaam nzima halina kanis a zuri na kongwe kama hili la Mtakatifu Antony wa Padua la Mbagala Misheni.
Wakiwa wadogo Mwanakwetu na wenzake wanakumbuka kuwa kulikuwa na watoto wa aina mbili; wale walikwenda kusali wakiambatana na wazazi wao na wengine walikwenda kusali wenyewe.tambua umsomaji wnagu katika malezi ya watoto yako ya aina mbili kuna ya kuku wa kienyeji na yale ya kuku wa kisasa. Sasa waliyokuwa wanakwneda kusali wenyewe kama kuku wa kienyeji akina Mwanakwetu walipaswa kuwa makini na maelekezo ya Mzee Ben.
“Watoto wote kanisani mlipaswa kukaa mbele ya yale mabenchi ya kulia na upande wakushoto walikuwa wanakaa wanakwaya na watawa na ukiingia kanisani hakua kutokatoka.”
Wale watoto waliokuwa wanakwenda kusali na wazazi wao wakiingia kanisa tu wazazi wao walitamani kukaa nao pamoja lakini Mzee Ben akawa anawaambia jamani hapa kanisa sisi wote ni watoto wa Mungu na kwenu wazazi mtambue hilo kuwa watoto wote wanapaswa kukaa mbele isipokuwa wale waliokuwa wadogo sana wanaobebwa tu.
Mara zote Mzee Ben alikuwa akisimama sehemu ya kuungamia huku akifuatilia misa hizo na wale wafanya vurugu na waliokuwa wakitokatoka nje ya kanisa kweli walichukuliwa hatua kali ikiwamo kufinywa na bakora. Hilo Iilikuwa linaleta tabu sana lakini mzee huyu alikuwa mkali zaidi hata kuwafinya wale wakorofi waliendeleza utundu.
Mzee Benson Njiu alikuwa mara zote kanisani akija kusali anava kanzu nyeupe na ibada zake zote ni zile za watoto za kila jioni na na ibada za Mtakatifu Antony wa Padua za kila jumanne.
“Ninakumbuka japokuwa Mwanakwetu nilikuw amtundu sana lakini kw abaharti nzuri utundu wangu haukuweza kukutana na bakora za Mzee Bensoni Njiu hata mara moja.”
Kanisa letu hili zamani tulikuwa tunaingia kusali muda wowote ule, ukiwa na tafakari zako za kiroho wewe unaingia unasali zako na kuondoka zako, siku hizi na mambo ya usalama ulivyokuwa na mashaka na ubinadamu juu yake ukitaka kusali huko ujiandae siku za ibada tu ndipo milango inakuwa wazi kinyume sali kwako Ukristo wa Sasa Tafauti na Ukristo wa Zamani..
Pale Mbagala Misheni pana makaburi ya muda mrefu mno katika eneo ambalo lilikuwa wazi miaka mingi na eneo hili lilikuwa linavamia sana na watu wakajenga nyumba zao, Mzee Ben alikuwa mkali kwa wavamizi hao na kulilinda eneo hilo kwa nguvu zake zote ukidhania pale angezikwa yeye na familia yake tu kumbe tunazikwa wote Wakristo wa madhehebu yote.
Mwanakwetu anakumbuka huyu Mzee Benson Njiu yeye mwenyewe akachangua eneo moja ambalo lilikuwa kando nyumba na mpaka na ndugu mmoja ambaye alikuwa akisumbua mno kuiharibu mipaka ya makaburi yetu akasema akifariki azikwe hapo, kweli baada ya muda Mzee Benson Njiu alifariki na kuzikwa hapo hapo alipopachagua na kaburi limekuwa kaburi mpaka lakini kwa sasa makaburi ya Mbagala Misheni eneo hilo hayatumiki tena kuzikia wafu kwani eneo limejaa.
Kwa Historia ya siye wenyeji wa Mbagala Makaburi ya Mbagala Misheni ndiyo Makaburi ya kwanza ya Wakristo maana eno hili lilifikiwa na Wamsonarai wa Kwanza Wabenedikitine wakati wanakwenda Kusini Mwa Tanzania.
Mwanakwetu kila anapokwenda Dar es Salaam huwa anajitahidi mno kusali kanisa hilo japokuwa sasa Mbagala si kijiji ni mji mkubwa lakini wale watoto wa zamani rafiki wa Mwanakwetu wamekuwa watu wazima. Oktoba 2020, Mwanakwetu alikutana na jamaa mmoja miongoni mwao waliokuwa wakicharazwa bakora na mzee Benson na wale watoto watulivu, kama kawaida yake Mwanakwetu alimuuliza kaka huyu naona umerithi kazi ya Mzee Ben ? Jamaa ilibidi acheke sana, akisema kuwa kweli sasa ni wakati wake wa kuwa mkali kama Mzee Ben kwa wale watoto wafanya vurugu kanisani ili waje kuwa na tabia njema kama yeye.
Maisha yaliendelea kama kawaida nayo Disemba 7, 2022 Mwanakwetu alikwenda Dodoma Mjini kuwasalimia rafiki zake kadhaa waliokuwapo katika Mkutano Mkuu wa CCM Taifa alipofika hapo alikutana na rafiki zake kadhaa wajumbe wa mkutano huo kutoka mikoa ya Songwe, Tanga, Kigoma, Morogoro na Dar es Salaam alifanya nao mazungumo mengi akipata simulizi tele.
Hawa wajumbe wa Dar es Salaam mjumbe mmoja alikuwa miongoni mwa wale ambao alikuwa mtoto mtulivu aliyekuwa akikaa mbele kanisani na hakuwahi kuchapwa wala kufinywa na Mzee Ben wakati ule, huyu ni yule aliyeambiwa-Kaka naona umerithi kazi ya Mzee Ben ?
Oktoba 2022, Mwanakwetu kama kawaida yake akasema, kijana wa Mzee Ben upo? Akajibu ndiyo akamwambia kaka bado unataka kumrithi Mzee Ben hadi Dodoma? Jamaa akacheka sana, akamuuliza Mwanakwetu kwani Mzee Ben alikuwa chama chetu?
“Unashangaa ! Wakati huo hapana na ndiyo maana yake ndiyo na hizo ni enzi za Katibu Mkuu wa CCM Rashidi Kawawa 1982-1990 na Horace Kolimba 1990-1995.”
Mrithi wa Mzee Ben aliuliza kwani Lawrence Gama alikaa kipindi gani ? Mwanakwetu alimjibu kuwa Gama alikuwa Katibu Mkuu wa CCM 1995-1997 yeye na Wilson Mukama walikatibu kipindi kifupi mno kati ya mwaka mmoja na miwili tu naye Mzee wetu Philip Mangula alikatibu kwa kipindi kirefu kuliko yoyote yule tangu 1997-2007
Mwanakwetu akiwa hapo akamuombea kura William Lukuvi kwa ndugu yake huyu, jamaa akamjibu kuwa mheshimiwa hajawaona wajumbe hao na kuwaomba kura? Mwanakwetu akamwambia ndugu yake huyu kwa kuwa kura zinaombwa kikaoni? Jamaa akacheka sana. Mwanakwetu akauliza wagombea wengine wameshaomba kura? Mabasi yenu yalisimamishiwa wapi? Mrithi wa Mzee Ben akacheka mno.
Mwanakwetu akaulizwa kwanini anampigie debe mheshimiwa William Lukuvi wakati yeye ni mzee na huo ni muda wake kuwapisha vijana? Mwanakwetu akajibu
“CCM ni chama cha wote na ana uhakika na uzoefu wa kiutendaji wake katika chama na serikali, hata ubunge wake jimboni kwake anafanya vizuri pia alipokuwa UVCCM hakutudhulumu track suit za Chipukizi.Siyo unampigia mtu aliyeluwa anadhulumu track suit za chipukizi , mkiwa kambini mnalishwa maharage tu kumbe bajeti ilikuwa nyama maharege, dhulumati wa track suit akiwa dhulumati wa nafsi za watu utashangaa?”
Jamaa akacheka kwa kuwa alikuwa mjumbe wa kikao hicho wakarudi kikaoni. Mwanakwetu alikaa nje ya ukumbi huo hadi matokeo yanatangazwa .
Mwanakwetu anasema nini siku ya leo?
Kikukbwa Mwanakwetu amemkumbuka Mzee wake Benson Njiu namna alivyokuwa akiwafundisha tabia njema akina Mwanakwetu wakiwa wadogo tu.Pia Mwanakwetu amelikumbuka kanisa lao dogo na Nzuri la Mtakatifu Antony wa Padua Mbagala.
Msomaji wangu usiwasahau wale wanaodhuluma track Suti za Chipukizi na kuwalisha maharage kila siku ni hatari mno maana yake baadaye wanaweza kuja kudhuluma nafsi za watu .
Mwanakwetu upo upo?
Je makala haya yaitwaje?
Simulizi ya mzee Benson Njiu,Malezi ya Watoto Wadogo Kanisani au Hapana ndiyo maana yake Ndiyo?
Mwanakwetu anachagua Hapana Ndiyo Maana Yake Ndiyo.
Nakutakia Siku Njema.
makwadeladius@gmail.com
0717649257
Post a Comment