MBAGALA & KIGAMBONI AMKENI

 


Adeladius Makwega-Musoma MARA

Kuna swali moja dogo nimekuwa nikuulizwa na ndugu zangu wa majimbo ya Mbagala na Kigamboni kwa majuma matatu mfululizo juu ya Uchaguzi Mkuu wa Wabunge wa majimbo haya ya Dar es Salaam, jambo la kusikitisha kwa muda mrefu uwekezaji wa wagombea kwa majimbo haya unafanywa kwa wajumbe wa CCM kupatiwa maboresho na kisha kuelekea uchaguzi mkuu na CCM kushinda.

Kwa hakika ndani ya Kura za Maoni CCM kukiwa na malalamiko mengi waliogombea kura za maoni wakilalamika ndani ya vikao vya CCM na hata hadharani na wengine kususia hata kampeni hadharani na kuendelea na shughuli zao binafsi baada ya kuona hakuna kinachofanyiwa kazi mara baada ya malalamiko ya rushwa ndani ya CCM.

Mwanakwetu nimekuwa mzito kuyajibu maswali hayo si kwamba sina majibu yake hapana kikubwa ni kukerwa na siasa zinavyofanyika na hakuna dalili ya hali hiyo kubadilika na hali hiyo ikitoa nafasi kwa mwenye mzigo mkubwa (fedha) kufanya atakavyo.

Ushahidi wa hili ni kauli ya marehemu Kitwana Kondo (KK) alipokuwa mbunge akisema,

“Ninashinda Ubunge kwa fedha zangu mwenyewe naomba msinisumbue.”

Jambo hilo liliwakera watu wa Kigamboni na Mbagala hadi kuamua kumpigia Kura Frank Magoba CUF(UKAWA) na kisha kuwa Mbunge wa Kigamboni baada ya KK kubwagwa chini.

Ni jambo la busara anayesema hadharani maana hilo liliwafumbua macho wakazi wa majimbo haya wakati huo likiwa jimbo moja la Kigamboni lakini mwingine, haramia hasemi lakini utendaji wake wa kazi kama mbunge iwe kachaguliwa kwa wananchi au viti maalumu inatoa taswira ya kauli ile ile ya KK,

“Ninashinda kwa Fedha zangu msinisumbue.”

Nakuomba msomaji wangu nitoe udhaifu wa Mbunge wa Mbagala na viongozi wa wilya ya temeke kwa sasa katika kuhamasisha elimu ndani ya shule zote za Mbagala za Msingi au sekondari za umma kupatikana chakula cha mchana , je kinapatikana kwa asilimia ngapi?


 

Kwa bahati nzuri binafsi namfahamu Mkuu wa Wilaya ya hata Katibu Tawala wa Wilaya ya Temeke, kwa hakika Mbunge na viongozi hao hawajatimiza wajibu wao ipasavyo wanapaswa kuwajibika na watubu kwa mola wao wakati wilaya za vijijini watu maskini kabisa watoto wao wanakula chakula cha mchana shuleni.

“Hii ilikuwa kazi ya Mbunge kuhamasisha jamii na viongozi wachache kuwatia moyo wazaai na wadau kazi inakuwa nyepesi, ukiona kwenye TV unamuona Mbunge anatoa jezi anatoa mipira, kaka Watoto hawali chakula cha mchana shuleni. Jezi hizo siyo mihogo ya kula watoti shuleni.

Mimi binafsi nimekula chakula cha mchana shuleni miaka ya 1990 akina Mary Chipungahelo na akina Masoud Ali Masoud walihamasisha hilo na ndiyo maana tukapata elimu yetu ya kawaida.

Chakula cha mchana Shuleni ni uhamasishaji tu lakini Mbunge Viti maalumu na Mbunge wa Mbagala mmeshindwa, miaka mitano inafikia ukingoni tukisema mnatumbia mnashinda ubunge kwa fedha zenu tutakuwa tumekosea?”

Historia inadokeza kuwa Mbagala na Kigamboni ni majimbo mtoto wa Jimbo la Temeke Dar es Salaam huku Jimbo la Mbagala limeanza mwaka 2015. Kwa hakika siasa za majimbo haya mawili zinaonesha kuwa kura za maoni ndani ya CCM huwa kuna wagombea wengi ambapo mara nyingi hawapungia chini ya 23 huku wagombea wa vyama pinzani mara nyingi kura za vyama vyate baada ya kupigwa ukizijulimsha zinazidi kwa mbali kura za mshindi wa ubunge wa CCM.

Kwa tathimini ya Mwanakwetu watu wa Mbagala na Kigamboni msilale usingizi, amkeni viongozi wazuri wa hili eneo walikuwa zamani yaani Balozi Ali Mchumo, Masoud Ali Masoud Kidogo na ndugu yangu Mwinchumu Abdul rahaman Msomi, wengine ni viongozi wanaofanya mambo yao lakini hoja za umma wamezipa kisogo kisa cha mfano ni chakula cha mchana shuleni.


 

Mwanakwetu anasema nini sku ya leo?

Kwa makala haya nashauri kwa mwaka huu wa 2025 watu wa Mbagala na Kigamboni tengenezeni watoto wenu kwa umasikini wenu, wawe viongozi wenu ili wakahangaikie shida za jamii yetu.

“Hao hao ambao hawana pesa za kuwahonga, ndiyo watoto wenu maana Mbagala na Kigamboni hatuna visima vya mafuta, hatuna dhahabu , sisi tuna mikorosho na minazi yenyewe sasa haizai na siku hizi soko la nazi limepungua sisi ni masikini, watengenezeni vijana wenu msiamini wanaokuja na mafurushi ya fedha. Waaminini watoto wenu waje kututoa aibu.

Hata hivi vyama vya siasa msiviamini sana, maana wako binadamu wenye maslahi yao, nyinyi watu wa Kigamboni na Mbagala angalieni maslahi yenu na vizazi vyenu tengenezeni watoto wenu muwapigie kura.”

Kwa hakika siyo siri kwa muda mtrefu Mwanakwetu anaamini wanaoshinda ubunge wamekuwa ni watu wanaotafuta fursa tu hata huyo Dkt Faustine Ndugulile ni marehemu simsimangi lakini hajahamasisha chochote juu ya chakula cha mchana  katika shule za umma, Je watoto wale hawali chakula cha mchana shuleni?Wanakula katika hayo mashule ya kimataifa.

Wananchi wenyewe pimeni kama mnabisha tazameni takwimu za Wilaya ya Mushi Mjini Chakula cha Mchana shule za Umma ngapi kinatoa chakula hicho linganisha na chakula cha mchana Mbagala na Kigamboni ni jibu lake ni aibu.

“Ukifuatilia mjukuu wa Mbunge wa Mbagala shule anayosoma ambayo ni binafsi Mjukuu wake anakula chakula cha mchana shulen,i vipi kwa hawa akina yakhe wa Shule ye Msingi Majimatitu, Shule ya Msingi Nzasa Shule ya Msingi Kongowe Shule ya Msingi Mtoni Kjichi na Shule ya Sekondari Mbagala?Watoto wanaaibika tu.”

Kumbukeni mwaka wa 2025 ni mwaka wa Jimbo la Mbagala na Kigamboni Kujitafakari na Kufanya Maamuzi sahihi.

Madiwani kutoka Mbagala?Kigamboni wanajitahidi lakini wanahitaji wabunge mwenye uwezo wa kutambua jamii ina shida gani na je tunatatuaje?

“Viongozi mtambue kuwa kesho mtaulizwa haya watu Mbagala watoto wao wlaikuwa hawali chakula cha mchana shuleni wewe ulifanya nini?Mwanakwetu akiulizwa hili yeye atajibu mimi niliona hilo ni tatizo nikaandika makala. Haya wewe mbunge na wewe mwingine, hakuna majibu hapo.”

Kumbuka,

“Mbagala na Kigamboni 2025 Amkeni .”

Nawatakia siku Njema.

makwadeladius@gmail.com

0717649257


 



 

 


0/Post a Comment/Comments