TUISHI KWA KUMTUMAINI MUNGU-PADRI MSIGALA

 


Adeladius Makwega-Barabara ya Lobina DODOMA

“Hizi nguvu tulizozana leo, hizo fedha, jamani hivyo vyote havitakuwa chochote kwako. Ipo siku utaletewa chakula hata kula utashindwa.

Mwenzenu juzi nilikwenda huko Manyoni, kijijini kabisa nikakutana na bibi mzee amelala kando ya zizi la ng’ombe, tupo na mtoto wake ana ng;ombe tele.

Nikauliza yule nani? Huyu jama akasema yule ni mama, nikasema twende nikamsalimie, akasema Padri unafikiri ataweza kukuelewa ? Nikasema twende.Nilipofika nikauliuza huyu ni mama yako mzazi? Jamaa akasema kweli kabisa.

Tukiwa pale jamaa akamuita mama yake wee mama wa watu wala hakuelewa ch ochote.Kijana wake akasema huwa tunamtoa ndani tunamleta hapa anakaa wewe, leo nashangaa hata hapa sijuhi amefikaje? Nikauliza  tena haongei, huyu jama akajibu haongei.

Yaani hata chakula anakula vijiko vichache tu. Mama huyu amekwisha kabisa nikauliza ana miaka mingapi, huyu kijana wake akasema mama ana miaka zaidi ya 100, mimi nina miaka zaidi ya 70 na mimi ni mtoto wake wa nne. Unatuona hivi hata hizi ng’ombe zote hizi tulipewa na yeye.

Wakristo wezangu nawaambieni leo hii itafika siku hata chakula hauwezi kula, tukumbuke kuishi kwa kumtegemea Mungu, hapa kuna njia mbili tu njia ya Ole na njia ya kumtumaini Mungu. Tijihaitia kumtamnia Mungu. Vile tunavyoachacharika navyo tuviweka katika matumaini ya Mungu.

Kila Jumapili Sali, Jumuiya nenda , fungu la kumi lipa, sadaka toa, kile kinachamuhusu Mungu fanya kadili ya Mungu alivyokujalia maana ni heri maskini wa roho.”

Haya yasemwa na Padri Gidieon Msigala katika mahubiri yake Jumapili ya sita ya mwaka C wa Liturujia ya Kanisa, katika Kanisa la Bikira Maria Imakulata, Parokia ya Chamwino Ikulu Jimbo Kuu Katoliki la Dodoma Februari 16, 2025.


 

Padri Msigala pia alisisitiza kuwa, katika maisha binadamu unafika kipindi unakata tamaa huku kila kona unasongwa lakini tujihidi katika yote hayo tumaini letu liwe kwa Mungu na si kwingine kokote kule.

Awali Padri Msigala alianza kupuliza Mbiu yake ya Mgambo ya mahubri ya dominika hii akisema kuwa suala la waamini kuchelewa ibada za misa siyo jambo zuri na ndiyo maana kanisa liliweka utaratibu wa misa zaidi ya moja katika dominika na sikukuu zote za Kanisa, hivyo basi kama muumini anashindwa kuwahi ibada ya kwanza fursa inatolewa katikaa ibada ya pili.

“Tumenza ibada hii kukiwa na waaamini 104 tu na sasa  tupo watu karibu 2000 na ushehe maana yake nusu nzima ya kanisa imechelewa nawaombeni viongozi wa Parokia yetu Chamwino Ikulu mlisema, hapa mi umbali mchache na  Dodoma Mjini ukisali Parokia  zote za Mjini saaa 12.30 shapu ibada inanza ,inakuwaje  hapa Chamwino Ikulu.?”

Maagizo haya ya Padri Msigala kwa waamini yanaingiza katika makala haya ilikuonesha kuwa suala la uchelewaji katika ibada linaweza kutokea eneo lolote lile na majibu ni kama alivyoeleza Padri Msigala kuwa kama umeshindwa kuwahi ibada ya kwanza  Sali misa ya pili.

MIsa hii pia  iliambatana na nia na maombi kadhaa huku mojawapo ni hili,

 

“Utusaidie kuamini kuwa mali ya dunia hii haiwezi kutusaidia kupata heri na furaha ya kweli Ee Bwana Twakuomba Utusikie.”i

 

Wakata haya yakiendelea katika mafurufaa, altare , mimbari na kuta za kanisa la Bikira Maria Imakulata, hali ya nje ya kanisa hili ni jua la kadili ikizungukwa mazingira yote ni kijani kibichi.

makwadeladius@gmail.com

0717649257









 

0/Post a Comment/Comments