Adeladius Makwega-Barabara ya Lobinaa DODOMA
Mwanakwetu katika maisha yake ameingia katika viwanja vya Bunge na ndani ya Bunge kwa namna tofauti’;kwanza kabisa kama Mwanahabari kuripoti Kipindi cha Leo katika Bunge lakini ameingia huko kama Afisa wa Serikali katika Vikao vya Kamati za Bunge na kikao cha mwisho kabisa anachokikumbuka ilikuwa ni Kamati ya Sheria Ndogo.
Siku hiyo kikao hiki kiliongozwa na Mh. Kilumbi Ngenda Mbunge kutoka Ujiji Kigoma. Mwanakweu akiambatana na maafisa kadhaa kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambapo kiongozi wa msafara huo alikuwa mhe Pauline Gekul akiwa Waziri Mdogo.Kikao hiki kilifanyika vizuri ambapo wakati huyu Balozi Humprey Polepole alikuwa hajachaguliwa kuwa balozi alikuwa mjumbe wa kamati hii.
Tulipomaliza kikao hicho Mh Pauline Gekul alitoa kuponi kwa maafisa wote wa serikali tulioambatana naye ili tuweze kula chakula mchana katika mkahawa wa bunge. Kweli Mwanakwetu nilipokea kuponi yangu kutoka Afisa Bunge kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ndugu Songoro na kwenda kula katika Mkahawa wa Bunge ambapoa ndani humu nilikutana wabunge kadhaa ninaofahamiana nao, huku wakinitania
“Makwega uchaguzi umefanyika wapi hadi unaingia humo Bungeni?”
Nikawajibu nikisema nimekuja katika vikao vya kamati na Waziri Wetu Mdogo BI Gekul.
Baada ya kula chakula hicho cha mchana Mwanakwetu alitoka zake hadi Sabasaba ambapo wakati huo basi za Sabasaba Chamwino zinasimama Sabasaba kabla ya kuhamshiwa Makole, kisha kupanda basi hizo hadi nyumbani kwangu Kijijini Chamwino Ikulu.
“Viongozi wanafanya kazi wakimaliza wanakula chakula na hilo ndiyo maana Bunge limewekewa mkahawa kando ili mambo yaweze kufanyika vizuri. Siku ile kama nisigepata kuponi ya Mh Gekul nisingekula chakula katika mkahawa wa bunge , huo ndiyo ukweli, Mwanakweu sikuwa na fedha ya kula mkahawa wa Bunge, ningetoka nje ya Bunge ningepanda basi hadi kwangu kisha kufika kwangu ningepasha viporo vyangu na kula. .”
Kwanini Mwanakwetu amekumbuka tukio hilo?
Mh Pauline Gekul kama kiongozi alitambua kuwa saa nane mchana ulikuwa muda wa kula chakula maana tuliingia kikaoni saa 3.15 ya asubhi na kutoka muda wa mchana, Pauline Gekul kama kiongozi alitambua, hawa maafisa wangu wengine mifuko yao imetoboka, wengine njaa zinawauma wasije kudodoka kisha wakapimwa ikabainika kuwa glukosi mwilini ilishuka ngoja niwape kuponi wale chakula.
Swali ni je viongozi wetu wanafikiria wenzao kwa mtazamo huu? Mtu anapochaguliwa kuwa mbunge/kiongozi je unawafikiriaje watu wako? Mfano wanafunzi je shule zako zote za msingi na sekondari za umma wanakula chakula cha mchana? Kama hawali je unashindwa kuhamasisha wanafunzi wale chakula cha mchana? Hawa watoto wanataweza kusoma vizuri wakiwa na njaa?
Kama sisi watu wazima tunashindwa? Hili Mwanakwetu analisema kwa hasa wa Wabunge wa Dar es Salaam uhamasishaji wa chakula cha mchana haujafanyika kabisa na hilo linawaweka wanafuanzi wa Dar es Salala katika wakati mgumu sana lazima uhamasishaji wa chakula cha mchana ufanyike ili watoto wetu waweze kusoma kwa bidiii.
“Nimeshuhudia mikoani ukiwaona wanafunzi wanakwenda shuleni wamebeba bakuri na vijiko vya kulia kande shuleni, hilo Dar es Salaam halionekani kabisa na hali ni mbaya katika maeneo ya watu masikini mathalani Mbagala, Tandika, Mtoni na hata maeneo ya Kigamboni.”
Swali la kujiuliza kama Bungeni kuna mkahawa wa chakula je kwanini mbunge haujiulizi hivi ndugu zangu watoto /wanafunzi wanakaaje na njaa tangu asubuhi hadi jioni.?
Hakuna haja ya kuwa kiongozi kama hatatui changamoto za jamiii yake na wala hana mbinu ya kuzitatua changamoto hizo. Kwa hili Mbunge Mbagala asijidanganye kuchukua fomu kugombea ubunge wa Mbagala anapoteza muda wake maana kwa tathimini Mwanakwetu hakuna alichoweza kufanya maana watoto na wajukuu zetu wanashinda na njaa shuleni.Watoto wetu hawahitaji mabufee kama ya Bungeni wanahitaji chakula kiasi cha kupoza njaa ili waweze kusoma.
Kama maeneo mengine jamii zinaweza kuhamasishwa na kuchangia chakula cha mchana inakuwaje Mbunge wa Mbagala ameshindwa kulifanya hilo kwa kipindi cha miaka mitano? Je kiongozi tunaweza lipi?
Mwanakwetu upo?
Kumbuka
“WANAFUNZI MBAGALA HAWAHITAJI BUFEE."
Nakutakia siku njema.
0717649257
Post a Comment