Adeladius Makwega-MBAGALA
Kwa hakika Mwanakwetu nimekuwa nafuatilia kauli za CHADEMA juu ya No Reform no Election zinazotolewa huku CHADEMA wakinipa matumaini kidogo kwani japokuwa wanayasema haya huku wakiwaita wanaohitaji kugombea ubunge kupitia chama hiki. Kauli ya No reform No election ingekuwa na mashaka zaidi kama CHADEMA wangekuwa na ganzi ya kufanya chochote kuelekea Uchaguzi Mkuu.
Hoja mojawapo ya CHADEMA ni juu ya Uwepo wa Tume Huru ya Uchaguzi, ambayo ipo lakini tume hii wanatilia shaka kuwa ni tume huru kwa jina lakini siyo huru kwa namna inavyofanya kazi.
Je hoja hii ina kweli yoyote au CHADEMA wanapoteza pumzi zao bure?
Mwanakwetu amelitafakari sana jambo hilo na kuamua kuingia kuicheza ngoma hii, kwanza akitazama ipi ni shabaha ya kufanyika uchaguzi?
“Tunakuwa na Uongozi unaosimamiwa na watu wenye ridhaa ya wananchi wenyewe na hilo linaondoa dhana za tawala za Kijeshi , Kidikteta, kifalme na kichifu, hii aina ya mwisho uongozi kwa Tanganyika uliondoka mwaka 1962 kwa sheria na Zanzibar kuondolewa mwaka 1964 kwa mapinduzi.”
Hili linafanyika kuonesha kwamba siyo kwamba fulani anaongozwa kwa kutaka yeye, bali kwa ridhaa ya wananchi walio wengi.
“Hapa ndipo ule ugomvi wa Kigunge Gombale Mwiru na CCM juu ya kauli mbiu ya Kidumu Chama Cha Mapinduzi-Kidumu Chama Tawala , huku kauli sahihi ni ile ya awali ya Kidumu Chama cha Mapinduzi-Kidumu Chama cha Mapinduzi , maana yake kama unasema kidumu chama tawala kama ukishindwa uchaguzi inakuwaje? Chama Tawala ni cha Miaka mitano tu kisha kinaomba ridhaa na wananchi na hapa wanaweza kuamua vyoyote vile, maana wao ndiyo watoa ridhaa.”
Kila uchaguzi unapofanyika lazima wananchi walio wengi watoe ridhaa iwe kuogoza Kijiji, kata Jimbo na Taifa.
Siku ya leo msomaji wangu tuseme huku kutoa ridhaa ya uongozi kuwe ni sawa na kuupanda mlima Kilimanjaro , wenye theruji tele na ridhaa hiyo kwa sasa Tanzania imekabidhiwa Tume huru ya Uchaguzi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yenye wajumbe hawa;
“Mhe Dkt Zakia Mohammed, Mhe, Magdelena Kamugisha, Mhe Balozi Omari Ramadhan Mapuri, Mhe Jaji wa mahakama Kuu Asina Omari, Mhe Jaji wa Mahakama ya Rufaa Mbarouk Salim Mbarouk na Mhe Jaji wa Mahakama ya Rufaa Jacob Mwambegele.”
Kwa kuyatazama majina ya wajumbe wa tume hii kwa muundo wa majina yao na dini zao utabaini wazi kuwa wajumbe wanne wanatoka dini moja na wajumbe wawili wanatoka dini nyengine.
Tanzania ni taifa ambalo halina dini, hilo ni sawa lakini taifa letu raia wako wapo wenye dini na wasiyo na dini, Je uteuzi wa wajumbe hao hatuoni kuwa unajenga dhana kuwa Tanzania ni taifa lenye dini mbili Wakristo na Waislamu? Hili ni kosa kumbwa kwa aliyeshauri na aliyefanya uteuzi huo, mbona Wapagani hawana mwakilishi wao, Wahindu na Mabahai vipi na Mashahidi wa Yehova Je ?
Ukiwatazama wajumbe sita wa tume huru ya uchaguzi utabaini kuwa wajumbe wanne, watano ni watu wanashugulika masuala ya sheria yaani majaji watatu na huyu mama Kamugisha kutoka TLS , hili siyo taifa la mambo ya sheria, hili taifa sasa ni mahakama au limekuwa kitivo cha sheria cha Chuo Kikuu Huria, taifa hili lina taaluma mbalimbali kama kuna hoja ya kisheria hakukuwa na haja kuwa wajumbe wote wanasheria maana tume inao wanasheria wake katika idara zake.
“Kibaya zaidi ukiwatazama wajumbe watatu wote wanatoka katika kuta za mahakama; Jaji Mwabengele, Jaji Mbarouk na Jaji Asna, hilo ni tatizo kubwa jaji anayesimamia uchaguzi kisha baada ya uchaguzi Mwanakwetu anakwenda mahakamani kupinga matokeo ya uchaguzi wa jimbo lake, jaji anaweza kumshawishi jaji mwenzake chini kwa chini na kuyapindisha matokeo mahakamani.Afadhali jaji hao wangekuwa wastaafu. Watanzania wengi wavivu kutoa sadaka ajira zao , ajira inakuwa kama dini ya wafanyakazi wengi serikalini.”
Pia kuna hoja ya mjumbe Balozi Omari Ramadhani Mapuri yeye anayo kadi ya CCM na hajairejesha hata kama amekula kiapo cha kuukana uanachama wake, hilo bado ni tatizo katika kutenda haki kwa vyama vingine, ambapo hili ni tatizo kubwa ambalo lilileta ugomvi katika kikao kimojawpao cha Tume ya Uchaguzi nakumbuka enzi ya Rais Magufuli kati ya aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Bumbuli Kapteni Mstaafu Peter Nyalali na Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi huyu huyu ndugu Ramadhan Kairima na kibaya zaidi ndugu Kairima hakulitatua kwa hekima jambo hilo na kutumia ubabe na kwa bahati mbaya walimtoa nje ya ukumbi Kapteni Mstaafu Peter Nyalali na kisha nafasi yake ya Msimamizi wa Uchaguzi kupewa mtu mwingine.
Kwa hoja hii Mwanakwetu anamlitia shaka hata Mkurugenzi wa sasa wa Tume huru ya Uchaguzi ndugu Ramadhan Kairima kubaki kwake katika nafasi hiyo maana yeye atalenga kukamilisha uchaguzi tu na siyo kuhakikisha uchaguzi huu unafanyika bila ya kuacha vidonda kwa taifa letu, kama hiki kidonda cha kapteni Mstaafu Peter Nyalali Ukumbi wa Kambarage Hazina Dodoma mwaka wa 2018.
Kwa hakika msomaji wangu makini naomba niseme wazi kabisa katika majaji watatu ni Jaji Asna Omar ipeke yake ni jaji ninayefahamu moyo wake anavyolipenda taifa letu la Tanzania na hilo linanifanya binafsi nimuheshimu sana Jaji Asina kwa maana ni mfanyakazi mzuri , ni mkweli , mpenda haki,kama kubadilika abadilike leo, kwa hakika nimeshawahi kufanya naye kazi za uchaguzi katika mazingira magumu sana na yenye fujo na haki ilisimamiwa vizuri.
Jaji Asna huyu ni dada wa Mwanakwetu, hilo lazima lisemwe lakini jaji wa Mahakama Kuu ametanguliwa na walio juu ambao ni majaji wa Mahakama ya Rufaa, kwa hakika dada wa Mwanakwetu hawezi kufanya kaz vizuri huku akiwa na Mkurugenzi wa uchaguzi Kairima , rejea kisa cha Kapten Mstaafu Pater Nyalali mwaka 2018 Ukumbi wa Kambarage na pengine Mweenyenzi Mungu alituonesha matukio haya ili leo hii yarejewe.
Kwa hiyo, kwa mawazo ya Mwanakwetu mjumbe ambaye kidogo ananafuu ni Dkt Zakia Mohammed na Jaji Asina Omari peke yao hawawezi kuifanya kazi hii vizuri katika kuzongwazongwa na miiba na mbigili zote hizo.
Mwanakwetu anasema nini siku ya leo?
Haya ni mawazo ya Mwanakwetu tu pale anaipotazama Tume huru ya uchaguzi ya Tanzania mwaka huu 2025, Tume ya Uchaguzi siyo Kitivo cha Sheria cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, hii ni tume inayotoa ridhaa ya uongozi wa taifa. Ndiyo maana nasema wajumbe wazuri ambao ni Dkt Zakia Mohammed na Jaji Asina Omari peke yao tutaweza kuupanda mlima Kilimanjaro? Tutaweza kufikia kutoa ridhaa ya haki ya uongozi kwa Tanzania? Tutaweza kufikie kilele cha mlima ule na tuweze kupiga picha salama? Binafsi nina mashaka makubwa.
Mwanakwetu upo ?
Kumbuka
“Hatuwezi Kuukwea Salama Mlima Kilimanjaro.”
Nakutakia Siku Njema.
0717649257
Peter Nyalali Kapteni Mstaafu
Post a Comment