MISINGI THABITI NA TIMILIFU 4

 

Adeladius Makwega-MBAGALA

Katika matini ya kwanza juu ya “MASJID RAHMAN BUTIAMA” nilizungumzia suala la Safari ya Mwalimu Nyerere kwa Mfalme wa Kuweiti wa wakati huo mara tu baada ya Mwalimu kutoa Ahadi ya Nadhiri yake ya kuwajengea Msikiti Waisilamu wa Kijiji cha Butiama.

Sheikh Azizi Rubare aliniambia kuwa Mwalimu Nyerere alifunga safari mara mbili kwa Mfalme wa Kuweiti ambapo safari ya kwanza alimkosa lakini safari ya pili pia mwalimu hakujaliwa kumuona Mfalme wa Kuweit wa wakati huo.

Kwa maelezo ya Sheikh Aziz Rubare safari zote za mwalimu kwa mfalme wa Kuweiti si kwa kwamba hakukutana na watu la hasha alikutana na wasaidizi wa mfalme huyo, lakini Mwalimu Nyerere alisema bayana kuwa aliona si hekima jambo hilo kuwaeleza vijana wadogo ambao walikuwa ni wasaidizi wa mfalme huyo.


 Gamael Abdel Nasser

Hoja kubwa ilikuwa ni juu ya kuomba fedha za ujenzi wa Msitikiti wa Waisilamu wa Kijiji cha Butiama.

Safari hizo mbili zilifanyika mwaka 1998 ambapo ni kipindi cha tangu Mwalimu Nyerere kutoa ahadi ya kuwajengea msikiti Waisilamu wa Butiama na kipindi cha ujenzi wa msikiti kuanza.

Mfalme wa Kuweiti wa wakati huo alikuwa ni Sheikh Jabal Al-Akmad Al-Sabah ambaye alizaliwa Juni 29, 1926 na alifariki Januari 15, 2006.

Ili kumfahamu vizuri Mfalme huyu mwaka 1962 alikuwa Waziri wa Uchumi na Fedha Kuweiti, miaka mitatu badaye (1965) aliteuliwa kuwa Waziri mkuu wa Kuweiti. Mwaka 1977 akawa mfalme wa 13 wa katika mlolongo wa ukoo wake.

Mahusiano baina ya Mwalimu Nyerere na Rais wa Misri wa kwanza Gamal abdel Nasser yalikuwa mazuri huku wakiwa wanasiasa wenye tabia zinazofanana katika mambo mengi likiwamo hata mitazamo ya kisiasa.


 



 Anual Sadat

Hilo linathibitishwa na ushiriki wa karibu wa Misri katika harakati za ukombozi wa bara la Afrika.

Huku mahusiano baina ya Misri na Kuweiti tangu enzi yakiwa mazuri sana. Nadhani hata mahusiano ya baina ya Tanzania na Kuweiti yalikuwa imara zaidi na mahusiano ya udugu baina ya Misri na Kuweit wa tangu enzi.

Ikumbukwe kuwa Gamal Abdel Nasser alifariki Septemba 29 1970, Misri ikaongonzwa Anuar Sadat hadi Oktoba 31,1981 alipouwawa na Spika Bunge aliogoza misri kwa siku chache kasha Hosni Mubaraka makamu wa Rais akawa Rais  na. Kwa mwaka 1998 Misri wakati Nyerere anakwenda Kuweit  Misri  ilikuwa inaongozwa Rais Hosn Mubarak.

Japokuwa mwaka 1998 Gamal Abdel Nasser alishafariki mwalimu hakusita kuifikiria safari ya kwenda Kuweiti kukamilisha ahadi yake kwa wanakijiji wenzake.Hata mfalme wa Kuweiti wa wakati huo alikuwa akifahamiana na Mwalimu Nyerere.


 Hosni Mubarak

Ndiyo maana mwalimu alianza na Kuweiti, lakini baadaye wazo hilo likapelekwa kwa Rais Mummar Ghadaf na yeye alifanikisha na Waisilamu wa Butiama wakajengewa msikiti huo ambao mpaka hii leo unatumiwa kusaliwa na Waisilamu hao wa Butiama.

 Mwanakwetu anasema nini?

 Maswali yalikuwepo mengi kwanini Julius Nyerere hakumuweka kipao mbele Gadafi na kumuweka mbele mfalme wa Kuweit je mwalimu hakumsamehe Gadafi ulishiriki wake kumuunga mkono Iddi Amini katika Vita vya Kagera? Swali hili ni jepesi inaonanekana kuwa Mwalimu Nyerere alikuwa msamaha na alimsamehe Gadafi na ndiyo maana alimfuata na kumuomba msaada na nduguze kujengewa msikiti.

 Kwa kuwa Aprili 13, 2022 inatimia miaka 100 tangu Mwalimu Nyerere azaliwe binafsi nilimua kuandika juu ya “MASJID RAHMAN BUTIAMA”ambapo Mwalimu Nyerere aliweka nadhiri ya kuujenga, japokuwa alifariki ukiwa katika hatua za mwanzo lakini kazi hiyo ilikamilika katika kipindi kifupi tu.


 Mfalme wa Kuweit wa wakati huo

Msomaji wangu naomba kwa leo niweke kalamu yangu chini hapo lakini kwa heshima ya pekee kwanza namshukuru Sheikh Azizi Magambo Rubare kwa kutumia muda wake wa biashara akiwa dukani kwake kuyajibu baadhi ya maswali niliyoyauliza huku wateja wakihitaji bidhaa dukani kwake.

 Pili namshukuru Sheikh Ahadi Saidi Mswaki ambaye ni Amir wa Wilaya ya Butiama chini ya Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiisilamu Tanzania, ambaye aliniongoza kuwatambua ndugu kadhaa ambao walishiriki zoezi la ujenzi wa msikiti huu.

 Nakutakia siku njema.

Kumbuka

“Misingi Thabiti na Timilifu.”

 

makwadeladius@gmail.com

0717649257





 



 Wake wa Marais wa zamani wa Misri

0/Post a Comment/Comments