Adeladius Makwega PWANI
Mbunge wa Malinyi Mkoani Morogoro Mhe. Antipas Zeno Mngungusi ametelembea Ofisi ya CCM ya Mji wa Kibaha hivi Karibuni na kusema kuwa kwa mujibu wa Bainokulasi yake amebaini kuwa Chama cha Mapinduzi CCM chini ya utekelezaji wake wa Ilani ya 2020-2025 ikiongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan wananchi wanakikubali chama hiki na kitashinda kwa ushindi wa kishindo zaidi ya ule wa mwaka wa 2020.
Ndugu Mngungusi alisema kuwa ushindi wa CCM kwa ngazi zote kwa uchaguzi Mkuu wa 2025 unabebwa na mambo kadhaa;
“Kwanza Utekelezaji wa ilani,Pili umahiri wa namna miradi ya maendeleo iliovyotekelezwa na tatu aina ya mgombea urais wa sasa ambaye ni mwanamke akiwa na mgombea mwenza Balozi Dkt Emmanuel Nchimbi .”
Akiongea hayo kandoni ya Ofisi hii ya CCM Kibaha Mjini, Mbunge Mngungusi aligusia kwa Jimbo lake la Malinyi na Mkoa Mzima wa Morogoro kwa Bainokulasi yake ushindi wa CCM ni wa asilimia 90 .
Akimaliza kuyasema haya aliwakumbusha wana CCM wenzake nchi nzima;
“Kwa sasa siyo wakati wa kuliacha lindo wazi kisa mie Kitukuu wa Kalembwana nimeyasema haya, bali sisi wana CCM tusiweke silaha chini bali sasa ni wakati wa kupambana kufa na kupona kuhakiksha wapiga kura wetu wanajitokeza kujiandisha, wajitokeza katika mikutano ya chama chetu na pia wajitokeze wakati wakupiga kura siku ya uchaguzi mkuu.”
Mh Mngungusi ni mbunge anayeliongoza Jimbo la Malinyi lililopo Halmashauri ya Malinyi yenye wakazi karibu 250,000 mkoani Morogoro na shughuli yao kubwa ikiwa kilimo.
0717649257
Post a Comment