MUSOMA WAPOKEA HISANI YA MAGODORO

 


Adeladius Makwega MUSOMA

Serikali Wilayani Musoma, Mkoani Mara imepokea karibu dazeti tatu ya magodoro ya kisasa kutoka kwa Wakfu wa Dkt. Wilson Mukama mbele ya viongozi wa Wilaya ya Musoma, huku shughuli hiyo ikishirikishwa viongozi kadhaa wa jamii ya watu wa Musoma na Kamati ya Ulinzi na Usalama  ya wilaya hii iliyo kando ya Ziwa Victoria, Aprili 3, 2025

Akizungumza katika hafla hiyo fupi mbele ya jengo la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara, Mkuu wa Wilaya ya Musoma Jumaa Chikoka alisema kuwa anaushukuru Wakfu wa Dkt Wilison Mukama maana wamewasaidia watu wa Musoma na kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan ambaye ndiye aliyefungua dimba kuwasaidia watu wa Musoma na Mkoa wa Mara, mara baada ya mvua kubwa kunyesha ikiambatana na upepo mkali na kusababisha madhara makubwa ya mali, makazi na miundombinu mwishoni mwa Machi 2025.

“Ninawaomba wale walioguswa kwa namna moja au nyingine, muendelee kutoa chochote, milango ya ofisi zetu ipo wazi maana bado kuna uhitaji wa misaada hiyo.”

Akizunguma wakati akikabidhi vifaa hivyo Dkt Mukama ambaye  ni kiongozi wa Wakfu huo alisema kuwa kama Mtanzania mwingine yoyote, amegushwa na ndiyo maana akanunua dazeti tatu ya magodoro hayo na sasa anayakabidhi kwa serikali nia ni kuwasaidia watu wachache sana ambao ni waathirika wa tukio hilo.

“Mchango wangu ni sawa na tone la maji katika Ziwa Victoria, hivyo na wezangu changieni chochote katika hili.”

Kwa mujibu wa utafiti mdogo wa mtayarishaji wa makala haya, uharibifu wa mvua na upepo huo ni mkubwa ambapo madhara ni kwa mali za watu binafsi, mitaji ya watu binafsi, madhara kwa taasisi za umma na wananchi mmoja mmoja.

makwadeladius@gamail.com

0717649257





 

0/Post a Comment/Comments