OFISI YA MUUNGANO NA MAZINGIRA HAIPASWI KUWEPO

Adeladius Makwega-MBAGALA

Mei 20, 2022 Shiriki la Utangazaji la Ujerumani lilipachika maelezo haya chini katika ukurasa wake mmoja wa Mitandao ya Kijamii.

“Wakati vuguvugu la madai ya katiba mpya likiendelea kufukuta, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoundwa na pande mbili, Zanzibar na Tanganyika, imekiri hii leo bungeni kuwa bado kuna masuala kadhaa ya Muungano ambayo hayajapatiwa ufumbuzi ikiwa ni pamoja na mgawanyo wa mapato unaotokana na hisa za Zanzibar.”

Shiriki hili la utangazaji lilitoa ripoti iliyofanywa na Deo Kaji Makomba na kueleza maelezo ya Waziri Jafo na maswali ya wabunge wawili. Baada ya msikilizaji kusikiliza ripoti hii ilitolewa nafasi ya maoni kwa kila msikilizaji wa shirika hilo kuandika la mayoni.

“Kama wanalitambua hilo warekebishe kwanza, mimi naona hakuna maana ya muungano huu, ukinunua kitu Zanzibar kukileta bara tozo yake ni kubwa kama umenunua nje ya nchi sasa huu muungano, uko wapi hapo?”

Haya ni maoni ya Priskus Sambaya.

“Afadhali Zanzibar imekumbukwa katika muungano, maana Wazanzibari wananyanyaswa sana, wanateseka na muungano, siku ya uchaguzi wanauliwa, wanapigwa wananyimwa haki zao, hawana raha hata kidogo.”

Haya ni maoni ya Salum Haji.

“Bora Zanzibar wawe peke yao maendeleo yatakuwa makubwa sana, kwa Zanzibar ndani ya muda mfupi pia Oman itashirikiana nao.”

Haya ni ya Asas Zame.

“...huu muungano waufanyie marekebisho tuwe pamoja Tanzania Bara na Visiwani, amani iwepo.”

Haya ni ya Yusufu Sahani.

“Busara kati ya viongozi ifanye kazi maana wakiwa wazembe kwa kiasi fulani huenda jambo hilo likasababisha mengine makubwa.”

Haya ni Antonie Kataya.

“Kero zinazomalizwa ni zile nyepesi, ila vigongo bado,”

Haya ni ya Jeremia Malisa.

“Hatutaki kabisa Wazanzibar, hakuna cha kizingiti wala nini hivyo vizingiti haiviishi kila Leo?”

Haya ni maoni ya Wahida Hussein.


 

Hayo juu ni msomaji wangu ni moani saba kati ya maoni yanayokaribia 30 yaliyotolewa na wasomaji na wasikilizaji wa shirika hilo katika ripoti ya Deo Kaji Makomba ambapo kwa hakika maoni haya yote ukiyatazama ni kutoka pande zote  za muungano huu.

Mwanakwetu anasema nini katika mazingira kama haya?

Kwa hakika jambo la nchi lazima liwe na utetezi wa wengi katika nchi husika, ukiyatazama na kuyasoma kwa umakini maona haya utabaini madhaifu makubwa ya Muungano huu kubwa utetezi wa muungano ni kwa wale wenye nafasi katika Muungano huo tu.

Ukitaka kupima kisanyansi kwa muungano huu kutetewa na viongozi tu  ni uwepo wa  Ofisi ta Makamu wa Rais ya Muungano na Mazingira yenyewe inatatua hizo zinazoitwa kero za muungano. Kwa hakika uwepo wa Wizara yoyote unapaswa kushugulikia mashida ya watu kama vile Afya, Kilimo, Mifugo , Biashara, Stima, Miundombinu nakadhalika.Mwanakwetu anaamini ni kosa kitendaji kuwa na Wizara inayoshughulikia tu muundo wa serikali na jina lake.


 

Kweli tunakusanya kodi badala iongezwe kwenye Kilimo, Afya na mambo mengine tunaunda wizara ya kutatua kero za muungano?

“Muungano na Mazingira ni wizara kamili ambayo ipo chini ya Ofisi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania: kwa hivyo Waziri wake anaitwa waziri wa Nchi Ofisi ya makamu wa Rais Muungano na Mazingira.

Kimsingi Makamu wa Rais huendelea na majukumu yake ya umakamu wa Rais na hivyo yeye kuwa ni msimamizi tu wa wizara hii ambayo mojawapo ya majukumu yake ni kuratibu shughuli za muungano na mazingira chini ya Waziri mwenye dhamana pamoja na Naibu Waziri. Hao ndio wasimamizi wa Wizara hiyo. Hivyo hii ni wizara miongoni mwa Wizara za Serikali ya Tanzania.”

Mwanakwetu upo?

“Ofisi ya Rais Muungano na Mazingira Haipaswi Kuwepo.”

 

Nakutakia siku Njema.

makwadeladius@gmail.com

0717649257

 


 









0/Post a Comment/Comments