Adeladius Makwega-MBAGALA
Mwanakwetu alikuwa amechoka sana hivyo alijitupa kitandani kwake ili auchape usingizi, akiwa kitandani tu haikupita dakika moja alipokea ujumbe kutoka kwa rafiki yake mmoja na kisha kumuuliza kumbe upo macho? Akajibu eehe MwAnAkWeTu nipo macho. Mazungumzo haya yalibebwa na visa vingi vya matumizi ya sheria, nguvu, mamlaka na hekima huku ikisisitizwa mno umuhimu wa hekima pale mtu anapopewa mamlaka yoyote katika ulimwengu huu maana sote duniani tunapita tu.
Jamaa huyu alimsimulia Mwanakwetu kisa hiki,
“Tulifika kuripoti kazini tukiwa walimu wawili mimi na mwezangu , Mkuu wa Shule akatupokea vizuri akatujazisha Pesoneli Data Fomu na kisha kusaini katika kitabu cha wageni. Shule hii ilikuwa na nyumba za watumishi tukakabidhiwa nyumba kila mmoja na yake ambazo zilikuwa nyumba za walimu wasio na ndoa.
Jioni yake Mkuu wa Shule anakasema jamani twendeni baa tukazungumze kidogo, (Unajua hapo sisi miezi hii na mwezangu hatuna mshahara). Mkuu wea Shule alipofika baa akasema msiwena tabu nyie kila mmoja wenu anywe anachotaka. Hapo hapo zikaagizwa nyama na moja moto moja baridi .
(Mimi nikaagiza soda ya rangi ya njano), mwalimu mwezangu mgeni akaagiza bia na Mkuu wa Shule akaagiza bia. Tukala nyama na mwenye bia zake na mwenye soda na soda zake hadi tunamaliza mazungumozo hayo ni saa tano usiku. (Mimi nimekunywa soda tatu , mwalimu mwezangu mgeni kanywa bia nne na Mkuu wa Shule kanywa bia kadhaa.
Tukawa tunarudi nyumbani , tulipoachana na mkuu wa shule nikamuuliza huyu jamaa yangu kumbe unagonga vitu? Jamaa akajibu haya mambo mimi ni ya siku nyingi, tangu mdogo na tumemaliza shule tumekaa miaka mingi mtaani ajira hakuna , mtaani tunajifunza na ulevi
Tukafanya kazi vizuri sana, mimi nikaenda kusoma, jamaa yangu akabakia shuleni akawa mwalimu wa taaluma na baadaye akawa Makamu Mkuu wa Shule na mwisho Mkuu wa Shule baada ya Mkuu kufariki na huyu jamaa yangu akawa Mkuu wa Shule .”
Shule hii ambayo ilikuwa ni ya wasichana ikapata walimu wageni kadhaa akiwamo mwalimu kijana mmoja. Wakapokelewa vizuri wakaanza kazi. Katika hawa walimu wageni huyu mwalimu mvulana alikuwa na changamoto sana na mabinti. Mwalimu Mkuu huyu rafiki yake aliyeanza naye kaz akawaita walimu wa kiume na kusema nao maneno haya.
“Jamani sisi sote ni wanaume, hapa hakuna aliye mdogo, hapa kazini hizi tabia za huyu mwalimu wetu mgeni za kuhangaika na mabinti sizipendi, natambua mabinti zetu wanapendeza sana, wanavaa nguo zinapendeza mno lakini haturuhusiwi kuwa na mahusiano nao ya kimapenzi sisi ni wazazi sisi ni walezi na hilo ni jukumu la kila mwalimu.”
Kijana huyu akakanywa katika kikao cha walimu wa kiume na kusema ameelewa. Jambo hili lilipofuatiliwa baadaye kijana huyu mwalimu aliendelea kuwalalia vifuani wale mabinti wanafunzi wake kama kawaida. Mkuu wa Shule akafunga safari kwa Afisa Elimu wa Wilaya na kumueleza Afisa Elimu akasema huyu mwalimu afukuzwe kazi, Mkuu wa Shule akasema hapana kwanza ni mwalimu mzuri wa fizikia lakini naomba hamishiwe shule ya wavulana lakini hilo ni gharama, kijana aitwe aombe uhamisho ili kulinda kibarua chake. Kijana mwalimu aliitwa na aliandika barua ya kuomba hilo na kupangiwa Shule ya wavulana ....
Baadaye Mkuu wa Shule alihamishiwa shule nyingine na shule hii kupata mkuu mpya. Mkuu mpya naye aliripoti na akapata ujio wa walimu wapya wanne wakike watatu wakiume mmoja. Wakapangiwa majukumu vizuri wakaanza kazi, kazi hizo zimefanyika ikafika kipindi cha mitihani kumbe katika kundi lile la walimu wanne wako mabinti walevi na huyu kijana mgeni naye mlevi. Siku moja kijana akalewa hadi kapitiliza muda wa kusimamia mtihani, kwa bahati nzuri akawajulisha wenzake jamani mimi naumwa kwa ujumbe mfupi , siri ikavuja kuwa jamaa kalewa mno hivyo anaogopa kufika hapo.
Mkuu wa shule akamfuata jamaa na kumuandikisha maelezo kwanini umelewa wakati wa kazi , huku mchakato wa kinidhamu ukifuata baada ya tukio hilo. Ofisini kukawa na mjadala mkubwa jamani hawa walimu ni wageni mnatakiwa kukaaa nao vizuri , maisha ya sasa yana changamoto nyingi, kwa hiyo ukiona kuna dalili za changamoto zozote kaeni nao karibu mtangundua maana hizo ajira zenyewe za watu wanakaa mtaani miaka zaidi ya mitano, hawana kazi kwa hiyo wanajifunza tabia znigine mbaya.Hapa walimu wakongwe wakakiirejea kisa cha yule mwalimu aliyehamashiwa shule ya wavulana...
Mkuu wa Shule akang’ang’ania juu ya suala la kinidhamu, walimu wakasema sawa, wewe ndiye mwenye mamlaka, wewe endelea.
Mwanakwetu lilitokea tukio ambalo halikufahamika, huyu kijana mwalimu mgeni wa kiume aliumwa siku moja gafla tu, wenzake wakambeba ili kumkimbiza zahanati ya kijiji na akiwa njiani katika bodaboda mwalimu huyu alifariki na huo ukawa mwisho wa uhai wake na Mwisho wa Barua ile ya Nidhamu.
Simu hiyo ilikata na kisha Mwanakwetu kuuchapa usingizi, kulipokucha Mwanakwetu akakumbuka tukio hili la nyumbani kwao Mbagala.
“Eneo la Mbagala Sabasaba-Mbuyuni Jijini Dar es Salaam, Tangu enzi lilikuwa na koo mbili za Kipogolo akina Makwega na akina Kazingoma, koo hizi mbili zote zinatokea kijiji kimoja na kata moja huko wilayani Ulanga, mkoani Morogoro. Kazingoma mwenyewe sasa ni marehemu, kwa asili mzee huyu alikuwa akifanya kazi mbalimbali za mikono lakini pia akifanya kazi moja kubwa sana kwa Wakristo wa eneo hili ya kuziosha maiti zao kabla ya maziko. Nyumbani kwake ni sehemu maaarufu mno kwa uuzwaji wa pombe za kienyeji tangu miaka ya1950 hadi leo hii na kazi hiyo imekuwa ikirithishiwa kutoka kwa kizazi kimoja kwenda kingine. Mara zote nyumba yao haikosi wageni iwe barazani, ndani ya vyumba au uani, kona zote huwa zimejaa wateja. Nyumba hii kwa kuwa ipo jirani na kwetu kila ninapofika Dar es Salaam ninawajibu wa kufika hapo na kuwasalimu kwa heshima zote ndugu zangu hawa.”
Kwa muda mrefu nimekuwa nikijiuliza jambo moja linalonishangaza mno japokuwa tupo nao jirani akina Kazingoma lakini koo hizi mbili hazijaoleana iwe kwa siri au wazi,Akina Makwega kwa asili wana mabinti wengi wakati akina Kazingoma wana vijana wa kiume wengi hawaoleani iwe kwa siri au wazi, hilo linanipa picha kuwa hawa ni ndugu wakubwa sana tangu enzi. Kila wao/sisi linapotokea tatizo la kifamilia vikaoni tunakuwa pamoja tukishirikiana namna ya kulitatua. Kwa majuma kadhaa mwaka 2022 nilikuwa nipo Dar es Salaam, nilifika nyumbani kwa Kazingoma kama adaa yangu na kukaribishwa katika dawati maalumu na kuwasabai. Nilitumia zaidi ya dakika 45 kuongea na ndugu zangu hawa. Mandhari ya Nyumbani kwa Kazingoma ilikuwa ya wateja wengi nje na ndani ya makazi haya, jua kali liliwaka huku wateja wao na mie ndugu yao tukibarizi chini ya mti uliokuwa na kivuli kizuri mno.
“Naona hapa pana hewa inayotoka katika kivuli cha mti huu, Je huu ni Mkungu?”
Walinicheka sana, kijana mmoja akasema,
“Makwega kwa umri wako unapaswa kuifahamu miti yote vizuri sana kwa majina na kazi zake, ili utuambiwe wadogo zako kama huu ni dawa au siyo. Inawezekana wadogo zako tukazunguka huko na kule tukapata shida, tukija kwako, kwa umri wake unatuambia chimbeni mti huu na huo, tunapata dawa tunapona. Sasa wewe hata mti huu ulio usoni kwako hautambui, je tutakuwa salama?”
Mwanakwetu nilisalimu amri kwa hoja hiyo, nikajibu mtakuwa salama tu . Mwanakwetu nikawa katika mtihani.Jamaa akasema
”Huu ni MTOMONDO na majani yake yanafanana fika na ya Mkungu. Unauona kila siku lakini leo Mungu amekupa bahati uulize ili uufahamu.”
Ndugu zangu hawa waliendelea kuuza pombe yao ya kienyeji, nikaulizwa, Umeshawai kusikia jina la Kijiji cha KITOMONDO? Nikajibu ndiyo nafahamu kidogo, ukiwa unakwenda Kisiju Pwani, ukitokea pale Mkuranga kuna kijiji kinatwa Kitomondo na jina hilo linatokana na mti huu, niliokulekeza.
Jamaa akaendelea kuongea.
“Mtomondo unamea sana katika vyanzo vya maji, lakini ni jambo la kushangaza mno mbona hapa umestawi hapa mbali na vyanzo vya maji? Kwa simulizi za Mzee Kazingoma mwenyewe alidai kuwa eneo hili lilikuwa na choo cha shimo, hivyo Mtomondo mmojawapo ulikuwa ni miongoni mwa magogo yaliyotumika kujengea, maji ya kuoga pahala hapa yaliustawisha na hadi leo umekuwa mti mkubwa, kama unavyouona, tunavyopata hisani ya kivuli chake.”
Jamaa aliendelea kusema kuwa ipo miti kadhaa ya Tanzania yenye tabia hiyo mathalani Mjenga Ua inaweza kuota kama huu. Niliendelea kupata darasa la mti huu,
“Kivuli chake kinawasaidia mno viumbe wa eneo ulipoota katika maji kujipumzisha na kuzuia kupigwa na jua moja kwa moja.Nayo majani yake yakiwa kama maboya yanayoeleaelea.”
Kizuri hakikosi kasoro,
”Ukiyachukua majani/magome yake ukayafikicha/kuyatwanga huwa yana madhara kwa viumbe walipo katika maji, baada ya muda machache viumbe kadhaa waliopo humu wataanza kuelea juu wakiwa wamelewa lakini yakianguka katika maji majani /magome yake hayana shida yoyote ile.shida yake ukiyakificha ua kuyatwanga”
Nikajiuliza sasa kwanini mti huu wenye madhara haya unastawi jirani na vyanzo vya maji? Jamaa akajibu
“Unapokabidhiwa bunduki siyo kwamba kila aliye jirani yako unamtandika risasi, ukifanya hivyo tutakuadhibu na tutakupokonya bunduki hiyo .”
Waliniambia ndugu hawa.
Mwanakwetu anasema nini siku ya leo?
Kwa hiyo Mtomondo umepewa madhara unapofikichwa/kutwangwa ili usiliwe na viumbe vinavyoweza kufika eneo hilo na ubaki kuwa salama wakati wote na kulinda mazingira ya maji hayo na viumbe hai wanaoishi. Kwa hiyo katika visa vyote hivyo juu tangu vile vya walimu wakuu, unapewa sheria siyo kwamba ni kibali cha wewwe kumuadhibu kilaa aliiye mbele yako, hata kama wewe ni jaji ni kweli umepewa mamlaka lakini unatakiwa kuonesha hekima ya mahakama katika ujaji wako katika uhakimu wako, ili kujitafauttisha baina ya wewe Jaji A na Jaji B, hata kama wewe ni Askari hata kwa sababu umesomea mafunzo ya kupambana na uhalifu na umepewa bunduki siyo kila aliye mbele yako Unamtandika risasi , tujifunze katika mti wa Mtomondo/
Mwanakwetu upo?
“Unadhani Kila Mtu wa Kuadhibiwa.”
Nakutakia siku Njema.
0717649257
Post a Comment