WASIFU WA WAFANYAKAZI WOTE WA TUME HURU YA UCHAGUZI UBANDIKWE KATIKA VYOMBO VYA HABARI

 


Adeladius Makwega-MBAGALA

“Enyi watumwa, watiini wao walio bwana zenu kwa jinsi ya mwili, kwa hofu na kutetemeka, kwa unyofu wa moyo, kana kwamba ni kumtii Kristo.”

 

Haya maelezo kutoka katika Bibilia kitabu cha Waefeso 6, 5. Huku utii likiwa neno la msingi katika aya hii.Mwanakwetu anakubaliana kabisa na aya hiyo lakini ana hoja juu ya matumizi mbaya ya utii kwa yule anayepata hadhi hiyo ya utii. Kwani utii mbele ya Mungu hauna shaka lakini utii kwa mwanadamu una shida nyingi.

Katika mambo ya kiserikali kuna Kiapo cha Utii ni kiapo ambapo mhusika au raia anakiri wajibu wa utii na kuapa uaminifu kwa mfalme au nchi au rais au taifa husika. Kwa mfano, maofisa nchini Marekani, hula kiapo kinachotii Katiba ya Marekani. Walakini, kwa kawaida katika ufalme wa kikatiba, kama vile Uingereza, Australia, na maeneo mengine ya Jumuiya ya Madola, viapo huapishwa kwa mfalme na rais.


 

Vikosi vya kijeshi kawaida huhitaji kiapo cha kijeshi ambapo kwa Tanzania wanakula kiapo cha Utii kwa Rais wa Jamahuri ya Muungano wa Tanzania na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye ndiye Amiri Jeshi Mkuu.

 

“Mimi naapa kwamba nitakuwa mwaminifu kwa Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa majeshi ya Ulinzi na Usalama Na kwamba nitailinda, nitaihifadhi na kuitetea katiba ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania kwa mujibu wa sheria zilizowekwa. Ewe Mwenyezi Mungu unisaidie!”

 

Makasisi katika makanisa nao wanakula kiapo cha utii Kwa Maaskofu na kwa Maaskofu wa Kanisa Katoliki hula kiapo kwa Baba Mtakatifu huku Bibilia Takatifu ikikaza sukurubu yake kwa aya nyingi katika hoja hii ya utii mathalani;

 

Waebrania 11:8 Kwa imani Ibrahimu alipoitwa aliitika, atoke aende mahali pale atakapopapata kuwa urithi; akatoka asijue aendako. (Angalia yale Mungu aliyotuagiza yaliyoandikwa katika Biblia Je unatii? Anasema mpende jirani yako kama nafsi yako-je unampenda jirani yako, unampenda mfanyakakazi mwenzako, anasema mpende adui yako, Pia Mungu anasema umpende yeye kwa moyo wako wote, roho yako, nguvu zako zote na akili zako zote, Je unafanya?

 

Anasema wazazi msiwachokoze watoto, pia watoto wawatii wazazi, wake wawatii waume zao na mengine mengi yaliyoandikwa, Je unafanya hivyo. Basi rudi kwenye utii. Kutokutiini ni asili ya shetani Lusifa ndio sababu iliyomuondoa Mbinguni, Kutokutii kulimuondoa Adamu bustanini. Wewe mama mtii mume wako ndio kumtii Mungu usikubali roho ya Lusifa ikutawale. Achana na misimamo kutaka kuwa sawa na Mume wako hiyo ni roho ya shetani/Lusifa inayoshambulia ndoa, kwani anajua mambo mazuri katika jamii iwe kiongozi, kanisa, mtaa, mwanafunzi n.k yanaanzia katika ndoa-familia.

 

Waefeso 5:22-24 Enyi wake, watiini waume zenu kama kumtii Bwana wetu. Kwa maana mume ni kichwa cha mkewe, kama Kristo naye ni kichwa cha Kanisa; naye ni mwokozi wa mwili. Lakini kama vile Kanisa limtiivyo Kristo vivyo hivyo wake nao wawatii waume zao katika kila jambo. Kwa hiyo Mtu yoyote ukiona una ukakasi hali ya kutomtii bosi wako, kiongozi wako, mchungaji wako, mzazi wako, mume wako ujue hiyo ni roho ya Lusifa pambana nayo rudi kwenye kunyenyekea utapona.

 

Waefeso 6:5 Enyi watumwa, watiini wao walio bwana zenu kwa jinsi ya mwili, kwa hofu na kutetemeka, kwa unyofu wa moyo, kana kwamba ni kumtii Kristo.”

Kwa hakika Bibilia katika hili imeikaza sukurubu na nati na nina hakika msomaji wangu pia tupo.


 

Mwanakwetu anasema nini siku ya leo?

Jambo hili limenipa tafakari kubwa siku ya leo baada ya kupitia ibara ya 211, 212,213, 214 na-215 ya Rasimu ya Marekebisho ya Katiba ya Jaji Warioba ambapo walieleza kwa kina juu ya Tume huru ya Uchaguzi na ibara ya 216 na 217 juu Nafasi ya Mkurungezi wa Tume Huru ya Uchaguzi.

Ukizisoma ibara zote saba vizuri wamejitahidi mno kulieleza jambo hilo lakini Jaji Warioba wenzake kuna itilafu moja sijuhi kama waliibaini, wangeongeze kuwa Mwneyejikiti wa Tume huru ya Uchaguzi, Wajumbe wake wote na Mkurugenzi wa Uchaguzi na watumishi wote wa tume ya huru ya Uchaguzi wasiwe Watanzania ambao waliwahi kufanya kazi kwa mkataba au ajira ya kudumu kutoka vyombo vya ulinzi na usalama.

Hawa wote wanakiapo cha Utii kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo mara nyingi anakuwa mgombea wa urais, mathalani huu mwaka wa 2025, hakuna mipaka ya mgombea urais na utekelezaji wa majukumu yake ya urais, kw ahiyo mgombea urais ananufahika na kiapo cha utii kutoka vyombo vya ulinzi na usalama wakati huo huo akiwa mgombea.


 

Hivyo basi kama mwenyekiti wa tume, wajumbe wa tume, Mkurugenzi wa tume au mtumishi wa tume ya uchaguzi kwa nafasi yoyote ile kama aliwahi kula kiapo cha utii, anawajibika kutii lolote atakalo agizwa maana anamlinda hadi kifo.

Kwa hiyo wasifu wa Mwenyekiti wa tume huru ya uchaguzi, wasifu wa wajumbe wake na Wasifu Mkurugenzi wa tume huru ya uchaguzi na watumishi wote utangazwe katika gazeti la Serikali na vyombo vya habari mapema kabla ya zoezi hilo kuazna kama yupo aliyedanganya apokwe ajira au uteuzi wake.

Kama Rais akiwa ni mgombea wa urais shughuli zote za utendaji wa Rais husika akabidhiwe Jaji Mkuu mpaka uchaguzi Mkuu utakapfanyika na rais kuchagulia ili kuondoa manufaa ya urais kwa mgombea urais ikiwamo Kiapo ya utii

 


 

Kwa maana Bibilia inasema Kipimo cha Imani yako ni Utii.

Mwanakwetu upo?

Je makala haya niyahitaje? Kipimo cha Imani Yako Utii? Ibara Saba za Rasimu ya Mabadiliko ya Katiba?Wasifu wa Wafanyakazi Wote Tume Huru ya Uchaguzi Ubandikwe Katika Magazeti ya Serikali.

Mwanakwetu anachagua Wasifu wa Wafanyakazi Tume Huru ya Uchaguzi Ubandikwe Katika Vyombo vya Habari.

Nakutakia siku njema.

makwadeladius@gmail.com

0717649257












 

 

 

0/Post a Comment/Comments